Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2018

UHAKIKA MEDIA

    Wapendwa wafuatiliaji wa blog yetu ya UHAKIKA MEDIA tunaomba ladhi kwa usumbufu ulo jitokeza leo kwa kuchelewa kuwaletea habari. Kuanzia sasa hali imekuwa vizuri karibu sasa ushiriki nasi upate habari mbalimbali za ulimwengu.       www.uhakikamedia.com

MAGAZETI YA LEO 31/3/2018

MAGAZETI YA LEO 31/3/2018 Uhakika media · 7 hours ago

Azam Fc yatuma salamu Mtibwa Suger

Azam FC yatuma salamu Mtibwa Sugar Uhakika media 2  · 4 hours ago Kazi ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports inasubiriwa kwa hamu kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam wakati Azam FC ikiikaribisha Mtibwa Sugar.  Tayari wageni wameonekana kujiamini na kusisitiza wako tayari kwa ajili ya mchezo huo.  Lakini Azam FC nao wamesisitiza hawatakuwa na utani na mtu na wanachotaka ni kuituliza Mtibwa Sugar na kuivurumisha nje ya michuano hiyo.  Kocha Msaidizi wa Azam, Idd Cheche amesema wamejipanga vizuri tena sana.  “Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi katika mechi hii, kwani kwa sasa FA ndiyo michuano pekee ambayo tunaitegemea katika harakati zetu za kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa.  “Kwa hiyo, tutapambana kufa au kupona ili tuweze kupata ushindi katika mechi hiyo,” alisema Cheche.  Mechi nyingine ya robo fainali ya FA itakayochezwa leo itaikutanisha Prisons dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, wakati Yanga itakuwa mgeni wa

Ibrahimovic afurahia maisha LA Galaxy

Ibrahimovic afurahia maisha LA Galaxy Uhakika media  2  · 4 hours ago Mshambuliaji mkongwe wa Sweden, mwenye umri wa miaka 36, Zlatan Ibrahimovic akifurahia kwenye mazoezi ya LA Galaxy jana baada ya kujiunga nayo rasmi kutoka Manchester United ya England kwa kusaini mkataba wa miezi 18. Ibra anaweza kuanza kucheza Ligi ya Marekani, MLS leo dhidi ya mahasimu wa Los Angeles, LAFC.

Mke wa Roma ahofia kumpoteza mumewe

Mke wa Roma ahofia kumpoteza mumewe Uhakika media2  · 4 hours ago Kila mdau wa muziki nchini Tanzania kwa sasa anahamu ya kusubiri wimbo mpya wa rapa Roma Mkatoliki hii baada ya mkali huyo wa Hip Hop kupitia katika kipindi kigumu cha kufungiwa wimbo wake na yeye mwenyewe kupigwa marufuku ya kutojihusisha na muziki.  Sasa habari nzuri ni kwamba jina la wimbo wake mpya ambao unatarajiwa kuachiwa limeshavuja na sio lingine ni  “NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU” jina ambalo limevujishwa na mkewe.  Mkewe na Roma Mkatoliki, Nancy amesema anajua magumu anayopitia mumewe na anawaza endapo ataachia wimbo huo wa “NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU” maisha yake yatakuwaje? kwani ugumu wa mashairi yaliyomo kwenye wimbo huo yanamtia hofu.  “Dah Nawazaa Sijui Baba Ataimba Nini Sasa Round hii! Kila Angle Wanakukazia!! Nawaza Ukiachia Ile “NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU.“ameandika Mke wa Roma kwenye ukurasa wake wa Instagram.  Hata hivyo, Nancy amemshauri Roma asiuachie wimbo huo kwani bado anampe

Utafiti unaonyesha jinsi Smart phone zinavyo haribu kumbukumbu za binadamu

Utafiti unaonyesha jinsi ‘Smartphone’ zinavyoua kumbukumbu za binadamu Uhakika media 2  · 4 hours ago Utafiti mpya kutoka nchini Uingereza unaonesha kwamba ongezeko la simu aina ya smartphone na mitandao ya kijamii linalosababisha tabia wa watu kupiga picha mara kwa mara linasababisha watu kupoteza kumbukumbu.  Utafiti huo unaeleza kuwa kupiga picha muda wote kunasbabisha watu kupoteza kumbukumbu ya vitu ambavyo wanaviona na hii ni athari kubwa kwa ustawi wa mtu.  Wanasayansi hao ambao wamechapisha utafiti huo kwenye jarida la Journal of Experimental Social Psychology wameeleza kuwa ongezeko la mitandao ya kijamii halijawa tu athari kwa afya za watumiaji bali hata maisha yao ya kawaida.

Urusi yalipiza kisasi Kwa Marekani

Urusi yalipiza kisasi kwa Marekani Uhakika media 2  · 4 hours ago Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov  amefahamisha kuwa  ubalozi mdogo wa Marekani mjini Saint-Petersburg umefungwa na kufukuzwa wanadiplomasia 60.  Hatua hiyo imechukuliwa  na Urusi kama jibu kwa Marekani na Magharibi  na washirika wao kuhusu sumu aliopewa jasusi wa zamani wa  Urusi Skripal.  Uingereza imewafukuza  wanadiplomasia 23 wa Urusi na wengine 150 katika mataifa 25 ya mataifa ya Ulaya. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa kama jibu kwa huatua zilizochukuliwa  mataifa ya Magharibi dhidi ya Urudi.

Mtibwa Suger yajigamba kuinyoa Azam Fc leo

Mtibwa Sugar yajigamba kuinyoosha Azam FC leo Uhakika media 2  · 3 hours ago Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema wamejiandaa vilivyo kuhakikisha wanaitumia Azam FC kama njia na kusonga mbele katika mechi yao ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports. Mtibwa Sugar inacheza mechi ya robo fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam na Katwila anaamini wamejiandaa hasa. "Azam wana timu nzuri lakini kweli tumejiandaa sana na tuko Dar es Salaam kutafuta matokeo ya mechi hiyo," alisema. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwezo wa wachezaji wa timu hizo ambao wamekuwa wakiuonyesha katika mchuano hiyo na Ligi Kuu Bara msimu huu. Mshindi katika mechi hiyo ataingia nusu fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake atapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Anthony Joshua na Joseph Parker nani mbabe

Anthony Joshua na Joseph Parker nani mbabe Uhakika media 2  · 45 minutes ago Leo Wales na dunia nzima itasimama kwa muda kuangalia pambano la wanamasumbwi wawili mahiri wa uzito wa juu duniani (heavyweight), Anthony Joshua wa Uingereza na Joseph Parker wa New Zealand.  Pambano hilo la kuwania ubingwa wa Dunia wa uzito wa juu katika mikanda minne ya WBA ,IBF, IBO na WBO , litapigwa uwanja wa Principality Cardiff nchini Wales, uwanja mbao Joshua mwaka jana alitetea mikanda yake dhidi ya Carlos Takam,  Wakali hao wa ndonga wameunganisha mikanda yao Joshua akiweka mezani mikanda yake ya ubingwa wa dunia wa WBA,IBF na IBO huku Parker akiweka mezani mkanda wake wa dunia wa WBO.  Mabondia hao wote ni mabingwa wa dunia na wote  hawajapigwa hata pambano moja, Joshua akiwa na rekodi ya 20-0 akishinda yote kwa KO huku Parker akiwa na rekodi ya 24-0 akishinda 18 kwa KO na 6 kwa pointi.  Pambano litaanza majira saa 4:30 usiku kwa saa za Wales (Saa 6 usiku kwa saa za Afrika mashariki) na bing

Ngorongoro Heroes kusaka tiketi ya AFCON Leo

Ngorongoro Heroes kusaka tiketi ya AFCON leo Uhakika media  2  · 45 minutes ago Kikosi cha timu ya taifa chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes kinashuka Uwanja wa Taifa kukabiliana na Congo (U20) katika mchezo wa kwanza wa kufuzu kutafuta tiketi ya kushiriki mashindano ya AFCON (U20).  Ngorongoro itakuwa inacheza mechi yake ya kwanza kabla ya kurudiana na Congo bada ya wiki mbili huko Kinshasa nchini humo.  Kocha wa kikosi hicho, Ammy Ninje, amesema tayari vijana wameshajiandaa na wapo kamili kwa ajili ya pambano hilo dhidi ya wapinzani wao.  Mchezo huo unataraji kuanza majira ya saa 10 kamili jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba kuweka kambi Iringa kuwawinda Njombe Mji

Simba kuweka kambi Iringa kuwawinda Njombe Mji Uhakika media 2  · 32 minutes ago Simba SC wameondoka asubuhi ya leo majira ya saa moja kuelekea Iringa kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya safari ya Njombe kwa ajili ya mchezo wa ligi.  Kikosi hicho kitaweka kambi Iringa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na Njombe Mji kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara.  Mechi hiyo ya ligi, itachezwa Aprili 3 2018 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe huku wenyeji wakiwa wametoka kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la FA dhidi ya Stand United jana.  Wekundu hao wa Msimbazi wataondoka Iringa Jumatatu ya wiki lijalo kuelekea Njombe, tayari kwa mchezo huo utakaopigwa siku ya Jumanne.

TFF yafunguka baada ya kupokea CECAFA

TFF yafunguka baada ya kupokea ya CECAFA Uhakika media 2  · 25 minutes ago Kufuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupokea barua kutoka Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ikiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya KAGAME, TFF wamesema watafikiria ombi hilo.  Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario, amesema kuwa ni kweli wamepokea barua hiyo, ila watakaa wajadili kama taasisi ili baadaye waweze kuja na majibu rasmi ya michuano hiyo kama itafanyika au kutofanyika.  Clifford ameeleza kuwa watahitaji kufikiria ombi hilo kulingana na hivi sasa ina ratiba ya mashindano ya soka la vijana kuelekea kufuzu AFCON chini ya miaka 20, hivyo watakuja na jibu rasmi baadaye.  CECAFA imetuma barua hiyo ikiiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Kagame kwa ngazi ya klabu ambayo yanataraji kuanza mwezi Juni 2018. 

DRC Congo: Mapigano yasababisha shule kufungwa

DR Congo: Mapigano yasababisha shule kufungwa Uhakika media2  · 19 minutes ago Takriban shule ishirini zimechomwa moto kutokana na mapigano yanayoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.  Kwa mujibu wa habari,ndani ya wiki mbili zilizopita shule za msingi na sekondari zimekuwa zikiangamizwa kwa moto katika mapigano ya kikabila kaskazini mashariki mwa DRC.  Afisa polisi Ivan Legu amekiambia kituo cha habari cha Anadolu kuwa zaidi ya shule 60 zimefungwa katika vijiji sita eneo la  Djugu,Ituri.  Hii ni kutokana na mapigano na mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa kati ya jamii za Lendu na Hema.  Zaidi ya watu arobaini wamepoteza maisha katika mapigano hayo,hali iliyoilazimu serikali kutuma majeshi kutuliza ghasia lakini bado haikusaidia. Eneo la Ituri linaongoz katika mapigano ya kikabila na kusababisha vifo vya wengi.

Nape Nauye awapa somo viongozi wa siasa

Nape Nnauye awapa somo viongozi wa siasa Uhakika media 2  · 12 minutes ago Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye(CCM) amesema kuwa viongozi wa kisiasa wasipojijengea utamaduni wa kuvumiliana Tanzania itakuwa nchi ya ovyo kabisa kuishi.  Nape amesema hayo kwenye mtandao wa kijamii huku akitoa salamu za pole kufuatia cha Mzee Victor Kimesera huku akieleza kuwa kwa mzee huyo wanajifunza siasa za kuvumiliana.  “Pumzika Mzee Kimesera, kwako tunajifunza siasa za kuvumiliana! Viongozi wa kisiasa tusipojenga Utamaduni wa Kuvumiliana Tanzania itakuwa nchi ya hovyo kabisa kuishi!,“ ameandika Nape katika ukurasa wake wa Twitter.  Victor Kimesera alikuwa ni mmoja wa waasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Arnold Schwarzenegger afanyiwa upasuaji wa moyo

Arnold Schwarzenegger afanyiwa upasuaji wa moyo Uhakika media 2  · 11 minutes ago Mwigizaji maarfu wa Hollywood Arnold Schwarzenegger amefanyiwa upasuaji wa moyo.  Arnold Schwarzenegger ambae amecheza katika filamu takriban 50 na alikuwa gavana wa zamani wa California amefanyiwa upasuaji wa moyo ambao umemalizika salama usalimini.  Meneja wa nyota huyo amesema kuwa mnamo mwaka 1997 Arnold Schwarzenegger aliwekewa "pulmonary valve",na upasuaji huu umefanywa ili kumuwekea "pulmonary valve" mpya.  Kama kawaida katika filamu zake Schwarzenegger hutumia sana neno la "I'll be back"na baada ya upasuaji amerekodiwa akisema, "I am back".  Arnold Schwarzenegger, ambaye alianza kujenga mwili wakati wa umri wa miaka 15.  Alishinda tuzo ya Mr.Universe akiwa na umri wa miaka 20.

Mpiga picha wa Diamond aacha kazi

Mpiga picha wa Diamond na WCB ‘Kifesi’ aacha kazi Uhakika media 2  · 6 minutes ago Mpiga picha wa msanii Diamond Platnumz na WCB kwa ujumla, Kifesi ameamua kuachana na kazi hiyo.  Kifesi ameeleza kuwa muda aliyofanya kazi WCB wa takribani miaka mitano unatosha ila kilichomsukuma zaidi kuacha kazi ni kutaka kujiajiri na kuwa karibu na Mungu wake kwani kazi aliyokuwa anaifanya ilimbana zaidi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kifesi ameandika;  Leo ikiwa ni siku takatifu na siku ya ibada kwangu ni siku nilioamua kufanya maamzi yatayobadili maisha yangu, nimeamua rasmi kuacha kazi kama mpiga picha wa Diamond na mwajiriwa wa WCB.. Well It’s insane to be leaving a stable job u love But that’s reality for me naacha kazI kwa mtu alikuwa zaidi ya Rafiki kwangu, naacha kazi ambayo ni ndoto ya vijana wengi out there but to me..i see miaka yngu 4/5 ya kufanya kazi hapa inatosha niachie nafasi kwa vijana wengine nimeamua kufata moyo wangu.  Ni uamzi niliokua nao karibu mwaka sasa but kama i

Misingi bora ya ufugaji wa mbuzi kibiashara

Misingi Bora Ya Ufugaji Wa Mbuzi Kibiashara Uhakika media · 20 minutes ago NAMNA BORA YA UFUGAJI.   1. Wafugwe kwenye banda bora.   2. Chagua kulingana na sifa zao na lengo la ufugaji (uzalishaji) nyama au maziwa.   3. Walishwe chakula sahihi kulingana na umri.   4. Kuzingatia ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti wa magonjwa.   5. Kuweka kumbukumbu za uzalishaji.   6. Kuzalisha nyama au maziwa bora yanaokidhi mahitaji ya soko.   SIFA ZA ZIZI AU BANDA BORA LA MBUZI.   1. Banda bora linatakiwa liwe ni lenye kuweza kuwakinga mbuzi au kondoo na mashambulizi ya wanyama wakali (hatari) na wezi.   2. Liwepo sehemu ambayo maji hayawezi kutuama.   3. Mabanda yatenganishwe kulingana na umri.   4. Liwe na ukubwa ambao linaweza kufanyiwa usafi.   Kama utafuga mbuzi kwa kuwafungia (shadidi) muda wote zingatia yafuatayo:-   1. Banda imara lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya,upepo/mvua.   2. Lenye hewa ya kutosha.   3. Liwe na sakafu ya kichanja na sehemu ya kuwekea chakul

Misingi bora ya ufugaji wa mbuzi kibiashara

Misingi Bora Ya Ufugaji Wa Mbuzi Kibiashara Uhakika media · 20 minutes ago NAMNA BORA YA UFUGAJI.   1. Wafugwe kwenye banda bora.   2. Chagua kulingana na sifa zao na lengo la ufugaji (uzalishaji) nyama au maziwa.   3. Walishwe chakula sahihi kulingana na umri.   4. Kuzingatia ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti wa magonjwa.   5. Kuweka kumbukumbu za uzalishaji.   6. Kuzalisha nyama au maziwa bora yanaokidhi mahitaji ya soko.   SIFA ZA ZIZI AU BANDA BORA LA MBUZI.   1. Banda bora linatakiwa liwe ni lenye kuweza kuwakinga mbuzi au kondoo na mashambulizi ya wanyama wakali (hatari) na wezi.   2. Liwepo sehemu ambayo maji hayawezi kutuama.   3. Mabanda yatenganishwe kulingana na umri.   4. Liwe na ukubwa ambao linaweza kufanyiwa usafi.   Kama utafuga mbuzi kwa kuwafungia (shadidi) muda wote zingatia yafuatayo:-   1. Banda imara lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya,upepo/mvua.   2. Lenye hewa ya kutosha.   3. Liwe na sakafu ya kichanja na sehemu ya kuwekea chakul