Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 19, 2018

Magufuli amewajibu wanao sema dangote amefunga wawekezaji mtwara

Rais John Magufuli leo  March 19, 2018  amevishukia vyombo vya habari vya kimataifa zinavyoandika kuwa Mfanyabiashara mkubwa Afrika  Aliko Dangote  amefunga uwekezaji wake kwenye kiwanda chake cha Cement kilichopo  Mtwara  nchini  Tanzania . Rais Magufuli  ameeleza kuwa taarifa hizo ni za uongo, na ukweli ni kwamba kuna mashine yake imeharibika na alikuwa na matatizo na management yake hivyo ameanza kufanya mabadiliko madogo ya watendaji wake hao wa kiwanda hicho. “Katika biashara yoyote, kuna vita, panaweza kuwa hata na vita kati ya taifa na taifa kuhusiana na biashara lakini niwaambie tu kuwa Tanzania ni sehemu bora ya kufanya uwekezaji.” – Rais Magufuli

Bocco atetewa na mashabiki wa Al masry

Bocco atetewa na Mashabiki wa Al Masry Uhakika media 5  · 23 minutes ago PAMOJA na mwamuzi kutoka Eritrea kumlamba kadi ya njano nahodha wa Simba, John Bocco akimtuhumu kumkanyaga mtoto, mashabiki wa Al Masry wamepinga hilo na kusema mwamuzi hakutumia busara. Bocco aliteleza na kuanguka wakati akiufuata mpira uliotoka. Alipoanguka alijikuta anamkanyanga mtoto muokota mipira ambaye alilazimika kupata matibabu. Baada ya mechi mashabiki wa Al Masry walionekana wakimpa pole Bocco kutokana na kilichotokea. Wengine waliliambia Championi Jumatatu kuwa mwamuzi hakuonyesha busara kumuadhibu Bocco ambaye wanadhani hakukosea. Simba ilitoka suluhu katika mchezo huo na kutolewa kwa jumla ya mabao 2-2, baada ya kuruhusu mabao mawili ya ugenini katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam

Wanafunzi 7 wa shule ya sekondari ya lyamungo wafukuzwa

Wanafunzi 7 wa shule ya sekondari wafukuzwa Uhakika media 5  · 51 minutes ago Shule ya sekondari ya Lyamungo iliyopo Hai mkoani Kilimanjaro inafunguliwa leo baada ya kufungwa kwa wiki mbili kufuatia fujo zilizopelekea kuvunjwa kwa nyumba moja ya Mwalimu hali iliyopelekea wanafunzi 7 wa kidato cha tano kufukuzwa. Wakati shule hiyo ikifunguliwa Kamati maalum iliyoundwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai na kubaini chanzo cha matukio ya mara kwa mara na utovu wa nidhani katika shule hiyo imewasilisha ripoti yake na hatua za kuchukua. Wanafunzi 890 walilazimika kuja na wazazi wao katika ofisi ya Mkuu wa shule huku wakiwa na barua katika maeneo wanayotoka. Uongozi wa shule hiyo umechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwafukuza wanafunzi 7 wa kidato cha Tano lakini pia kuwasimamisha kwa muda wanafunzi wa kidato cha sita ambao watalazimika kufika shuleni siku ya mitihani ya Kitaifa ya kitado cha sita. Jengo ambalo liliharibiwa liliharibiwa vibaya na wanafunzi hao limeanza ku

Amuua mama mkwe, amjeruhi mkewe kisa unyumba

Amuuwa mama mkwe, amjeruhi mkewe kisa unyumba Uhakika media  5  · 47 minutes ago Kijana aliyefahamika kwa majina ya Joseph Medardi (32) mkazi wa Nyakahanga Wilaya ya Ngara mkoani Kagera amemuuwa mama mkwe wake Elizabeth Simon (70) kwa kumkata kata mapanga na kumjeruhi mkewe Elice Joseph (28) kisha na yeye kujimwagia petroleum.  Kijana huyo amefanya tukio hilo kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa na matatizo na mkewe kuhusu suala la unyumba jambo ambalo lilimpelekea kumrudisha mkewe huyo nyumbani kwa mama yake, ambapo amekaa huko takribani wiki tatu, siku moja kabla ya kikao cha kuwasuluhisha wanandoa hao ndipo kijana huyo ametekeleza mauaji hayo.  Mtoto wa marehemu Elizabeth Simon (70) ambaye ni Mchungaji Ezekia Simon amesimulia jambo hilo kwa undani zaidi na kusema kuwa chanzo cha yote hayo kuwa ni matatizo ya unyumba na kudai kuwa kijana huyo ambaye yeye ni shemeji yake alionekana amekuja na kusudio la kuwauwa wote yaani mama yake pamoja na mdogo wake huyo ambaye amejeruhiwa tu

Haji Manara: haitowezekana kamwe nikaonesha uzalendo kwa klabu za tanzania

Haji Manara: Haitowezekana kamwe nikaonesha uzalendo kwa klabu za Tanzania. Uhakika media  5  · 39 minutes ago Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema hatoweza kuonesha uzalendo wa soka kwa ngazi ya klabu labda mambo mengine yasiyohusiana na soka. Akizungumza na kipindi cha Sports Hedikota kinachorushwa na Radio EFM, Manara amesema hawezi kujitolea kuishabikia Yanga hata siku moja pale inaposhiriki mashindano ya kimataifa. Manara ameeleza kuwa aliwahi kuhamasisha timu za Tanzania kuonesha uzalendo haswa pale klabu zinaposhiriki mashindano ya kimataifa, lakini akapuuzwa na viongozi wa Yanga. Kutokana na kuupuzwa, Haji ameweka wazi kutothubutu tena kusapoti suala hili kutokana kutoungwa mkono na baadhi ya watu. "Haitowezekana kamwe nikaonesha uzalendo kwa klabu za Tanzania, juzi hapa niliwaomba watu tuungane tuwe kitu kimoja lakini kuna mtu mmoja kutoka upande wa pili akanijibu kwa kebehi" alisema Manara

Ronaldo: Hakuna hata mmoja duniani wa kumlinganisha na kipaji changu

Ronaldo;Hakuna hata mmoja duniani wa kumlinganisha na kipaji changu Uhakika media 5  · 31 minutes ago MWANASOKA Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo amesema kwamba hakuna mtu hata mmoja duniani wa kumlinganisha naye kwa kipaji chake, kujituma na uadilifu wake kisoka.  Nyota huyo wa Real Madrid na mshindi wa tuzo tano Ballon d'Or hata kama mjadala wa nani zaidi kati yake Lionel Messi utaendelea, Ronaldo anaamini yeye ni namba moja katika soka.  Akizungumza katika tangazo jipya la Nike, Ronaldo alisema; “Mwanzoni nilikuwa ninaota kuwa mchezaji bora duniani.  “Rafiki zangu, walikuwa wakiniangalia kama, "unasemaje?" Nilikuwa nacheza kwa kujifurahisha, kwa utani, lakini kichwani kwangu mawazo hayo yalianza nilipokuwa Manchester, hapo ndipo nilipoanza kuamini,”.  “Siwaoni watu wangu wenye kipaji kama changu cha kujaaliwa, kujituma na maadili yangu ya soka. Hakuna mmoja wa kumlinganisha nami, hakuna mmoja atakuwa Cristiano Ronaldo. Utakuwa wewe, nitakuwa mimi,”amesema.  Ronal

Utamkuta mtu hana hata kiwanda cha pipi alafu anazungumzia viwanda 'Rais magufuli'

Leo March 19, 2018  Moja ya shughuli inayoendelea ikulu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli  Ambae ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara anaongoza Mkutano wa 11 wa baraza hilo. Akifungua mkutano huo Rais Magufuli amewataka wanaohusika na masuala ya Viwanda ndio wazungumzie Viwanda  “Unamkuta mtu hana kiwanda lakini kila siku anazungumzia Kiwanda, hana kiwanda hata cha Pipi, nimeamua nyinyi wenye viwanda ambao mnazipata hizo changamoto tujue tatizo ni nini?”

Asilimia 76.6 warusi wampa tena Putin urais

Usiku wa March 19, 2018 Rais wa Urusi Vladimir Putin ameibuka mshindi mkubwa katika uchaguzi mkuu nchini humo na ataliongoza taifa hilo kwa miaka sita. Ushindi huo ulitarajiwa katika upigaji kura uliomalizik jumapili. Hata kabla ya kura zote kuhesabiwa tayari alikuwa amejizolea asilimia 76 ya kura kwa mjibu wa tume ya uchaguzi. Akizungumza katika mkutano wa kutangazwa mshindi amesema ushindi wake ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika uongozi wake. “Sina mpango wowote wa kufanya marekebisho yoyote ya katiba, kuhusiana na uenyekiti na serikali kwa ujumla. Nilishasema awali kwamba nafikiria suala hilo. Lakini kuanzia leo naanza kufikiria kwa undani, kwa sababu nilipaswa kusubiria matokeo ya uchaguzi kwanza.Mabadiliko yote yatatangazwa yakifuatiwa na uzinduzi..”  -Putin BREAKING: Alichozungumza Zitto Kabwe mbele ya waandishi wa habari

Rais Magufuli aongoza mkutano wa biashara wa baraza kuu la taifa

Leo March 19, 2018  Moja ya shughuli inayoendelea ikulu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli  Ambae ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara anaongoza Mkutano wa 11 wa baraza hilo. Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ikulu,  Gerson Msigwa  kupitia ukurasa wa Twitter amesema kauli mbiu katika mkutano huo ni  “Tanzania ya viwanda – ushiriki wa sekta binafsi”. Ujumbe aliopewa Dr Tulia kwenda kwa Rais Magufuli

Ris mwanamke wa kwanza Afrika ajiuzulu

Jana March 18, 2018  Rais wa Mauritius Ameenah Gurib-Fakim  ametangaza kujiuzulu huku kashfa ya matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kashfa ya matumizi mabaya fedha ikiwa inaendelea kumuandama. Gurib-Fakim  alikuwa ni rais pekee mwanamke Barani Afrika ametuhumiwa kwa kununua vitu binafsi vya kifahari vyenye thamani kubwa kwa kutumia kadi ya benki ya Taasisi ya Dunia yenye makao yake nchini Uingereza. Gurib-Fakim  alisema mapema wiki hii kwamba aliitumia kadi bila kujua, lakini alikuwa amewarudishia fedha hizo. Hata hivyo, Rais huyo alichaguliwa kuwa rais mwaka 2015 na hapo awali alikuwa Profesa wa kemia katika kitivo cha sayansi cha Chuo Kikuu cha Mauritius. Tanzania inashika nafasi Pili katika kuwashirikisha Wanawake katika Uongozi

Putin aibuka kidedea wa urais Urusi agoma agoma kubadili katiba

Putin aibuka kidedea urais Urusi, agoma kubadili katiba Uhakika media 1  · 2 hours ago Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameibuka mshindi kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine ujao wa miaka sita baada ya kujipatia ushindi mkubwa wa zaidi ya asilimia 76 katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika jana Jumapili, Machi 18 nchini humo.  Akizungumza katika mkutano wa kutangazwa mshindi, Putin alisema ushindi wake ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika uongozi wake huku akieleza kuwa huo ni uthibitisho wa kukubalika kwa sera zake na kwamba hana mpango wowote wa kufanya marekebisho ya katiba na kusisitiza umoja na mshikamano.  “Hadi hapa sina mpango wowote wa kufanya marekebisho yoyote ya katiba, kuhusiana na unyekiti na serikali kwa ujumla. Nilikwisha sema awali kwamba nafikiria suala hilo. Lakini kuanzia leo naanza kufikiria kwa undani, kwa sababu nilipaswa kusubiria matokeo ya uchaguzi kwanza,” alisema Putin.  Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari Putin alikwepa s

Mama Samia azuru ksburi la dk Omary Ally Juma

Mama Samia azuru kaburi la Dk Omari Ali Juma Uhakika media 1  · 2 hours ago Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jana ameanza ziara ya siku tatu Pemba ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli za maendeleo. Makamu wa Rais ambaye amewasili Pemba jana na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama ambapo alipokea taarifa za mikoa miwili ya Pemba. Pia Makamu wa Rais alizuru kaburi la Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi, Pemba na kuweka shada la maua. Aidha Makamu wa Rais aliwataka Wananchi wa Chumbageni kukumbuka historia na kurudi nyumbani, Makamu wa Rais aliyasema hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Chumbageni Wambaa. Leo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatazamiwa kuendelea na ziara yake ambapo ataweka jiwe la msingi katika Kituo cha Huduma za Mama na Mtoto Shumba Vyamboni .

Odinga aweka hadharani mazungumzo yake na Rais uhuru

Odinga aweka hadharani mazungumzo yake na Rais Uhuru Uhakika media 1  · 2 hours ago Kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchini Kenya Nasa, Raila Odinga ameweka wazi walichoongea na Rais Uhuru Kenyatta, walipokutana mapema mwezi huu na kwamba waathirika wa ghasia za uchaguzi za mwaka 2017 watalipwa fidia na serikali.  Odinga amesema kuwa pamoja na fidia kulipwa jambo jingine walilokubaliana na Rais Kenyatta ni kufuta kesi za watu walioshiriki kuapishwa kwake, Januari 30 mwaka huu.  Walipokutana viongozi hao wawili walikubaliana kuzika tofauti zao za kisiasa kwa maslahi ya taifa la Kenya ingawa kumekuwa na shauku kubwa miongoni mwa wanasiasa na wananchi kuhusu masuala zaidi waliyokubaliana.  Rais Uhuru Kenyatta pamoja na Odinga walikutana Ikulu Machi 9  ambapo baada ya mazungumzo yao wote walisema kuwa wamekubaliana kuiganisha Kenya kwani nchi hiyo ni kubwa kuliko wao.

Droo ya FA CUP ipo tayari manchester united kuivaa spars

Droo ya FA Cup ipo tayari, Manchester United kuivaa Spurs Uhakika media 1  · 2 hours ago Manchester United imepangwa kucheza na Tottenham Hotspurs kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA.  United ilishinda mchezo wake wa mwisho baada ya kuiondoa Brighton FC, wakati Tottenham yenyewe ilipata matokeo dhidi ya Swansea City, Jumamosi ya wiki hii.  Mbali na United kukutana na Tottenham, Chelsea nayo imepangwa kukipiga dhidi ya Southampton iliyoitoa Wigan Athletic kwenye mashindano hayo.  Chelsea imefika hatua hii baada ya kutoshana nguvu mpaka muda wa dakika za ziada 'Extra Time' leo dhidi ya Leicester City na kupata matokeo ya mabao 2-1.  Timu hizi zimepangwa kukutana kufuatia droo iliochezshwa jana Machi 18 2018.

Wema aeleza mapenzi yake kwa Aunt

Wema aeleza mapenzi yake kwa Aunt Uhakika media1  · 2 hours ago Supastaa wa Bongo Movie, Wema Sepetu amelifunguka kuwa, hakuna mtu wa kumgombanisha na staa mwenzake, Aunt Ezekiel kwa kuwa wanapendana.  Katika mahojiano maalum, Wema ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alitupia picha karibia kumi kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram akiwa na Aunt alisema mara kwa mara wamekuwa wakigombana, lakini siyo kwamba hawapendani.  “Hakuna wa kunigombanisha na Aunt. Kama tunagombana, mtu wa pembeni anatakiwa kukaa kimya maana tukipatana mambo yanakuwa ni moto,” alisema Wema

Waziri Ole Nasha atoa ufafanuzi wa michango mashuleni

Waziri Ole Nasha atoa ufafanuzi wa michango mashuleni Uhakika media 1  · 2 hours ago Kufuatia sintofahamu iliyoibuka hivi karibuni kuhusu suala la michango mashuleni, Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William OleNasha ametoa ufafanuzi wa kisera juu ya jambo hilo.  Ole Nasha amesema michango yote mashuleni iratibiwe na ofisi za wakurugenzi wa halmashauri husika lakini pia isitokee michango hiyo ikafungamanishwa kwa aina yoyote na mwanafuzi.  Katika kuwapunguzia wazazi mzigo wa michango mashuleni serikali ilipitisha uamuzi wa kupitiwa upya na kuratibiwa vyema utaratibu wa michango yote mashuleni, ambapo uamuzi huo unaonekana kuibua sintofahamu katika baadhi ya maeneo nchini.  Akiwa mkoani Kilimanjaro, katika halfa za kutia wakfu jina jipya la shule ya sekondari Bishop Alpha Mohamed High school kutoka jina la zamani Pasua Sekondari, Olenasha alitoa ufafanuzi huo wa Serikali.  Pamoja na kutiwa wakfu kwa jina jipya la shule hiyo ,waumini wa kanisa la Anglican,wachungaji ,m

Kessy atamba kutwaa ubingwa na yanga musimu huu

Kessy atamba kutwaa ubingwa na Yanga msimu huu Uhakika media 1  · 1 hour ago Beki wa pembeni wa Yanga Hasan Kessy amesema hajutii kuichezea Timu hiyo akitamba kuwa anajiandaa kubeba ubingwa akiwa na mabingwa hao watetezi.  Kessy alitoa kauli hiyo baada ya timu yake hiyo kuifikia Simba kwa idadi ya pointi 46, baada ya awali kuachwa kwa pointi saba.  Beki huyo, tayari amebeba taji hilo la ubingwa mara moja tangu ajiunge nayo msimu uliopita akitokea Simba baada ya mkataba wake kumalizika.  Akizungumza leo Jumatatu alisema amebeba ubingwa huo wa ligi kwa mara ya kwanza akiwa na Yanga huku akiamini kubeba kwa mara ya pili msimu huu, inawezekana.  “Simba watajutia sisi kuwafikia kwa pointi 46 walizokuwa wanaongoza katika msimamo wa ligi na malengo yetu ni kuutetea ubingwa huo tunaoushikilia katika msimamo.  “Kama tumeweza kuzifikia pointi zao, tutashindwaje kuwapita na kukaa kileleni na mwisho wa ligi tunatangazwa kuwa ni mabingwa kwa mara ya nne mfululizo?  “Na hilo linawezekana kwet

Serikali yaombwa kutunga sheria ya kuchangia mbegu nchini

Serikali yaombwa kutunga sheria ya kuchangia mbegu nchini Uhakika media 1  · 1 hour ago Wadau wa kilimo kutoka katika sekta binafsi nchini wameiomba Serikali kutunga sheria ya kutambua mfumo usio rasmi wa uzalishaji wa mbegu kwa kuwa mfumo huo unachagia zaidi ya asilimia 70 ya mbegu za kilimo nchini.  Washiriki wa mafunzo kutoka Mikoa 13 Nchini wakifuatilia mada mada zilizokuwa zikitolewa na makufunzi wa mafunzo ya mfumo wa uzalishaji mbegu kupitia mradi wa “Mbegu Zetu Haki Zetu” yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Mkoani Morogoro na kuandaliwa na Shirika la PELUM Tanzania kupitia ufadhili wa Bread for the World  Akizungumza mwishoni mwa wiki Mkoani Morogoro katika mafunzo ya mfumo wa uzalishaji mbegu kupitia mradi wa “Mbegu Zetu Haki Zetu” yaliyoandaliwa na Shirika la PELUM Tanzania kupitia ufadhili wa Bread for the World, Mratibu toka Shirika la TABIO Abdallah Mkindi alisema, uundaji wa chombo cha kisheria katika mfumo wa mbegu usio rasmi utasaidia kuleta mageuzi ya haraka katka

ujerumani imefuta ada vyuo vikuu vyote kwa wanafunzi wote ndani na nje ya nchi

Jana March 18, 2018  Nimeipata hii stori kutoka Ujerumani imepitisha sera mpya ya elimu kwa kuondoa aina zote za ada za masomo katika mfumo wa elimu ya juu, na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote wanaotoka ndani na nje ya Ujerumani. Sasa wanafunzi wote wanaosoma nchini Ujerumani watakuwa na fursa ya kupata elimu  bure, na kufanya kufanya fursa za elimu katika bara la ulaya na ulimwenguni kwa ujumla. Good News inatoka katika taifa la Ulaya Ujerumani ambapo wameamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote kutoka U.S.A na duniani kote. Wakati gharama ya elimu ya chuo kikuu ya Marekani inapoongezeka kwa masomo ya shahada ya kwanza ya kuanzia $ 14,300 kwa vyuo vikuu vya serikali kama UCLA hadi $ 37,800 kwa shule binafsi kama ada ya Chuo cha Harvard, Ujerumani sio gharama kubwa sana kuanza.

sikiliza albam mpya hapa

Msanii Lulu Diva ametuletea wimbo wake mpya unaitwa  “Homa”  na huu ametoa kama zawadi kwa mashabiki zake ikiwa ni muda mfupi tu toka achie wimbo wa  “Amezoea”  ambao unafanya vizuri mtaani, wimbo huu mpya una dakika 3:10 ukiwa umetayarishwa kwa Producer Abbar karibu kuusikiliza. “Ningealikwa harusi ya Shilole ningeenda, nimerudia dini yangu” – MZIWANDA FULL VIDEO: Uzinduzi wa Album ya Wakazi KISIMANI ulivyokuwa

video mpya

Leo March 18, 2018   Weusi  kutoka Arusha wameachia Video ya wimbo wao waliomshirikisha  Christian Bella ‘ NIJUE ‘. Ni Nahreel kutoka The Industry ndo kai-produce wakati Video ikiongozwa na Hanscana. Bonyeza  PLAY  hapa chini kuitazama pia usisahau kuacha Comment yako ili waweze ona maoni yako juu ya wimbo wao.

BREAKING NEWS

Jana March 18, 2018  Taarifa tuliyoipokea ni kuhusu Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu,  Anthony Mavunde  amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro akisumbuliwa na homa kali. Mavunde  amesema alipelekwa hospitalini hapo usiku wa kuamkia Jumapili baada ya kujisikia vibaya na saivi anaendelea kupatiwa matibabu

SOMA KWA MAKINI

JULIUS MTATIRO ANAPASWA KUKAMATWA KUSAIDI UPELELEZI WA KUJITEKA. ABDUL NONDO. . Na David Maphone. .. NI UJINGA KUSEMA KWAMBA JESHI LA POLISI LIMEMTEKA ABDUL NONDA KWA SABABU TU HALIJAMFIKISHA MAHAKAMANI. . Nimesoma maandiko ya Julius Mtatiro kuhusu sakata la KUJITEKA kwa kijana Abdul NONDA, Sasa nakubaliana na wengine kwamba Julius Mtatiro anapaswa Ima kukamatwa au kukimbizwa HOSPITAL DODOMA ili kuokoa Afya ya Akili yake, Katika andiko lake Mtatiro anasema JESHI LA POLISI kwa sababu halijampeleka Abdul NONDA Mahakamani kwa siku (12) wakiendelea na Uchunguzi ili kuwapata waliokuwa nyuma ya MPANGO wa kuchafua Taswira ya NCHI basi JESHI hilo LIMEMTEKA mtuhumiwa Abdul NONDA huu ni Upumbavu na unaweza kutamkwa na Kichaa tu.!! , Ukipitia maelezo yake aliyoyapa kicha cha habari ''WIKI MBILI ZA ABDUL NONDO KUTEKWA RASMI!'' Utadungua ni kwa namna gani kijana huyu alivyojenga CHUKI na Serikali,Jeshi la Polisi na nchi yetu Tanzania, Kila mtanzania kwa sasa anahitaji kujua

Jinsi ya kutafuta masoko

Jinsi ya kutafuta Masoko Uhakika media  · 8 hours ago UTANGULIZI Kuwafundisha washiriki kufikiri ki- masoko na kuelewa baadhi ya mbinu za masoko kitu ambacho kitawafanya waelewwe maana ya maneno “soko na masoko” pia utafiti wa soko na kuyafanyia kazi  katika biashara/miradi yao. Soko ni nini? Soko ni utaratibu au mtindo  uliowekwa kwa mujibu wa kanuni /sheria  kumwezesha mfanya biashara kuuza bidhaa zake kwa wateja/walaji. Husaidia kupanga nini uuze,nani umuuzie au jinsi gani watu wanavyoweza kujuakitu gani unauza,hivyo kukuwezesha kuzalisha kile ambacho kinahitajika  katika soko sahihi. Mafanikio katika biashara hutokana na mwonekano wa kipekee  wa bidhaa au bidhaa unayozalisha kukidhi matakwa ya walaji au wateja pia, kuweza kutambua  aina fulani ya watu ambao wangependa kununua bidhaa yako na kuweza kueleza  bayana ni kitu gani, watu wategemee kunufaika kwa kunua bidhaa zako kati ya kundi hili la walengwa. Kwa kifupi soko ni MTEJA Wa bidhaa na huduma uayozalisha Soko

Fahamu madhara ya mirungi kiafya

Fahamu Madhara Ya Mirungi Kiafya Uhakika media  · 8 hours ago HISTORIA;    Ni mmea ambao una majina mengi kulingana na eneo,mfano gomba,miraa,mirungi nk.   Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuwa zaidi ya masaa 14.6 milioni yanapotezwa kila siku kwa ulaji wa mirungi huko Yemen.   Ulaji wa mirungi ulianzia Ethiopia,ukaenea hadi nchi za Afrika Mashariki,Yemen, Zimbabwe, Zambia, Malawi na hata Afrika kusini.   Mirungi ilionekana kuwa ni moja ya madawa ya kulevya hivyo ikakatangazwa na umoja wa mataifa UN na kupigwa marufuku mwaka 1971 kwasababu ya ufanano wa kemikali iitwayo amphetamine.   Yapo madhara mengi ya kiuchumi, kidini nk. Lakini yafuatayo ni madhara ya kiafya ya mirungi kama ilivyofanywa na shirika la afya duniani kama ifuatavyo;   MADHARA YA KIAFYA;    Mtumiaji wa mirungi yupo katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo.  Kupungukiwa msukumo wa kufanya tendo la ndoa (low sex drive) na  pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mre