Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 16, 2018

Rais wa Ufaransa amtaka Trump asiondoe majeshi Siriya

Rais wa Ufaransa amtaka Trump asiondoe majeshi Syria Uhakika media1  · 51 minutes ago Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema amemshamwishi Rais wa Marekani Donald Trump, asiviondoe vikosi vya askari wa Marekani vilivyoko nchini Syria.  Mapema mwezi huu, Rais Trump alisema kwamba ataviondoa vikosi vya askari wake vipatavyo elfu mbili ambavyo vilitumwa nchini Syria hivi karibuni.  Ingawa Rais wa Macron amewaambia waandishi habari nchini kwamba amezungumza na rais Trump kabla ya shambulizi la anga lililotekelezwa mwisho mwa juma lililopita na kumtaka ashiriki kutafuta suluhu ya mgogoro huo kwa muda mrefu zaidi.  Akitolea ufafanuzi juu ya shambulio hilo la anga lililotekelezwa kwa pamoja baina ya Marekani, Ufaransa na Uingereza kwamba lilikuwa la halali.

Juluo aipa ubingwa Simba VPL

Julio aipa Simba ubingwa wa VPL Uhakika media1  · 45 minutes ago KOCHA Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amesema kama Simba itafanikiwa kushinda mechi zake mbili zijazo ikiwemo ya Yanga basi itakuwa imeshatwaa ubingwa wa msimu huu kutokana na kasi waliyonayo.  Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 55, nyuma ya Yanga inay­oshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 47. Azam kabla ya mechi ya jana ilikuwa na pointi 45 katika nafasi ya tatu.  Tayari Simba imebakiza mechi saba ambazo sawa na pointi 21 wakati Yanga ikiwa ina mechi nane sawa 24.  Akizungumza na Cham­pioni Jumatatu, Julio alisema: “Unajua kila kitu mipango, Simba sasa hivi ni wakati wao, wapo vizuri na wanastahili kuendelea kushin­da kwa sababu kikosi chao kipo vizuri, kama wakiendelea na kasi hii kwa kushinda mechi mbili zijazo ikiwemo ya Yanga basi wa­takuwa mabingwa na hilo halina mjadala.  “Nadhani Yanga kwa sasa ingeachana na suala la ubingwa na kuendelea kuijenga timu yao kwa sababu imenifurahisha falsafa yao

Mbowe atuma salamu za pongezi kwa Fatma Karume

Mbowe atuma salamu za pongezi kwa Karume Uhakika media 1  · 41 minutes ago Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amempongeza Fatma Karume baada ya kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa TLS. 

Hatuna taarifa ya Rais kushinda tuzo " Ikulu

" Hatuna taarifa ya Rais kushinda tuzo" Ikulu Uhakika media 1  · 36 minutes ago Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, nchini Bwana Gerson Msigwa, amesema haiana taarifa juu ya tuzo aliyoshinda Rais John Magufuli nchini Ghana, kama kiongozi bora barani Afrika. Akizungumza na www.eatv.tv Msigwa amesema kuwa utaratibu wa tuzo yoyote lazima mtu anayepewa apewe taarifa rasmi, lakini mpaka sasa hawajapokea taarifa yoyote kutoka kwa waandaaji wa tuzo hizo, hivyo hawajui lolote kama ni kweli ama la. “Hatuna taarifa ya tuzo hiyo, tunavyojua ni kwamba mtu yeyote anayepewa tuzo lazima apewe taarifa rasmi kutoka kwa watoaji, sasa hatujapata taarifa yoyote mpaka sasa, nasikia ndio tuzo ambazo kina Monalisa wameshinda, lakini hatujapokea taarifa rasmi kuhusu tuzo hiyo, hivyo siwezi nikaizungumzia”, amesema Msigwa. Tuzo hiyo ambayo imetajwa kuwa ameshinda Rais Magufuli, imetolewa Aprili 15, 2018 jijini Accra nchini Ghana, ambapo pia Watanzania wengine katika tasnia ya

Serikali ya yabanwa bungeni kuhusu thamani ya shilingi

Serikali yabanwa bungeni kuhusu thamani ya Shilingi Muungwana Blog 1  · 31 minutes ago Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Devotha Minja ameitaka Serikali kutoa majibu ina mpango gani kuchukua hatua ili kulinda thamani ya shilingi kama nchi nyingine zinavyolinda fedha zao.  Mbunge huyo amesema licha ya kuwepo kwa matamko mengi lakini bado maeneo mengi Watanzania wanalazimishwa kutumia dola badala ya shilingi ya Tanzania.  Akijibu swali hilo bungeni leo Jumatatu, Aprili 16, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema matumizi ya fedha za kigeni sambamba na shilingi ya Tanzania yanasimamiwa na Sheria ya Matumizi kwa Fedha za Kigeni ya 1992.  Dk Kijaji amesema Desemba 2017 waziri wa fedha alitoa tamko kwa umma kuwa ifikapo Januari Mosi, 2018, matumizi ya fedha za kigeni yazingatie mambo halisi yaliyopo na ikiwemo bei zote kutangazwa kwa shilingi ya Tanzania.  Kuhusu utitiri wa maduka ya kubadilisha fedha,  amesema hadi sasa Serikali imeshafungia jumla ya maduka 92 na ita

Mbaloni kwa kuhamasisha maandamano Aprili 26

Mbaroni kwa kuhamasisha maandamano Aprili 26 Uhakika media1  · 2 hours ago Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, linawashikilia wanafunzi tisa wa Chuo Kikuu cha Stella Maris na Daktari wa Hospitali ya Mission Nanyamba kwa tuhuma za kumkashifu Rais John Magufuli na kuhamasisha maandamano ya Aprili 26.  Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Lucas Mkondya, alisema watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp na Telegram kumkashifu Rais na kuhamasisha maandamano hayo.  Kamanda Mkondya bila kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa madai ya sababu za kiupelelezi, alisema daktari huyo ni kutoka Halmashauri ya mji wa Nanyamba.  “Ninatoa onyo watu wajiepusha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kusababisha uvunjifu wa sheria za nchi. Watuhumiwa wote tunawashikilia kwa upelelezi zaidi,” alisema.  Katika tukio lingine, Kamanda Mkondya alisema wanawashikilia wahamiaji haramu 23 waliokutwa katika nyumba ya kulala wageni eneo

CCM WAMEMTELEKEZA MZEE MAKAMBA JANUARY

" CCM wamemtelekeza mzee Makamba" January uhakika media 1  · 2 hours ago JANUARY Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira ametoa madai mazito kwa chama chake, kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtelekeza baba yake Mzee Yusuph Makamba akiwa mgonjwa. Makamba ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, akielezea hali ya baba yake kiafya na kusema pamoja na kupitia hali hiyo lakini CCM hakimpi stahiki zake kama mstaafu wa chama hicho. Mzee Makamba ameshika nafasi mbalimbali katika chama lakini kikubwa zaidi ni kuwa Katibu Mkuu cha chama hicho, pamoja na nafasi mbalimbali serikalini ikiwemo Mkuu wa mikoa mbalimbali ukiwemo Dar es Salaam. Katika taarifa hiyo ya January pia imeeleza tuhuma za wanasiasa aliowalea Mzee Makamba ambao mmoja wao kwa sasa anasema maneno mabaya dhidi ya mzee huyo. Soma andiko la January hapa chini : Majuzi nilienda kumjulia hali Mzee Makamba ambaye anaumwa. Ma

CCM imemtelekeza mzee Makama January

" CCM wamemtelekeza mzee Makamba" January Uhakika media 1  · 2 hours ago JANUARY Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira ametoa madai mazito kwa chama chake, kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtelekeza baba yake Mzee Yusuph Makamba akiwa mgonjwa.  Makamba ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, akielezea hali ya baba yake kiafya na kusema pamoja na kupitia hali hiyo lakini CCM hakimpi stahiki zake kama mstaafu wa chama hicho.  Mzee Makamba ameshika nafasi mbalimbali katika chama lakini kikubwa zaidi ni kuwa Katibu Mkuu cha chama hicho, pamoja na nafasi mbalimbali serikalini ikiwemo Mkuu wa mikoa mbalimbali ukiwemo Dar es Salaam.  Katika taarifa hiyo ya January pia imeeleza tuhuma za wanasiasa aliowalea Mzee Makamba ambao mmoja wao kwa sasa anasema maneno mabaya dhidi ya mzee huyo.  Soma andiko la January hapa chini :  Majuzi nilienda kumjulia hali Mzee Makamba ambaye anaumwa. Mazungu

Watu 7 wafariki kutokana na mvua za dar

Watu saba wafariki kutokana na Mvua Dar Uhakika media 1  · 1 hour ago Watu saba wamefariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam.  Kamanda wa polisi kanda maalum jiini Dar es salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha vifo hivyo, na kueleza kwamba mwili mmoja umekutwa ukielea kuelekea maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam.  Sambamba na hilo Kamanda Mambosasa amesema maeneo mengi jijini Dar es salaam yamejaa maji, na kuwataka watu kuwa makini wanapotumia barabara hasa sehemu zenye makorongo, na kuwaangalia zaidi watoto ambao wanapita mara kwa mara wakienda shule au wakiwa wanarudi kutoka shule.  “Watu wasijaribu maji, ukijaribu maji ujue utaondoka nayo, kwa hiyo watoto wetu wanapokwenda shuleni tuwasindikize, sehemu nyingi zenye makorongo kwa mfano kule Kinyerezi, kule Goba kule Makongo, zile shortcut zote maji yamejaa, watu wajiepushe kutumia njia hizo, watapoteza watoto wakiwa wanaenda au kutoka shule”, amesema Kamanda Mambosasa.  Jeshi la Polisi lim

Magazeti ya leo 16/4/2018

MAGAZETI YA LEO 16/4/2018 Uhakika media   · 3 hours ago