Mkuu wa Wilaya aelezea Shule kuita Waganga Uhakika media 5 · 59 minutes ago Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mohamed Mtanda ametolea ufafanuzi suala la shule ya Msingi Kabwe kuita waganga wa kienyeji kutoka Kongo, ili kutatua tatizo la kishirikina linaloikabili shule hiyo.` Akizungumza na www.eatv.tv. Mkuu wa Wilaya hiyo Said Mtanda amesema kwamba ni kweli alipokea simu kutoka kwa Mkuu wa shule hiyo kumuelezea matatizo yao hapo shuleni, na lengo walilofikia serikali ya kijiji ili kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara. Licha ya hayo mkuu wa wilaya hiyo amesema yeye kama kiongozi wa serikali ni kulichukua tatizo hilo kitaalam kwa kupeleka madaktari ambao watatafuta njia sahihi ya kutibu wanafunzi hao, na sio kuruhusu mambo ya kishirikina, ingawa hawezi kuwakataza wazee wa kijiji hicho kwani anaheshimu mila zao. “Nilipokea simu kutoka kwa mkuu wa shule hiyo akinielezea matatizo yao, akaniambia na uamuzi wa kijiji ulivyoamua, lakini mimi kama kiongozi wa ser
https://uhakika media.blogspot.com