Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo aukana Waraka wa Pasaka wa Maaskofu wa Kanisa katoliki Uhakika media 5 · 40 minutes ago Mwadhama Kadinali Polycap Pengo amesema hakuwa anajua kama kuna waraka utatolewa kuhusu kwaresma na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania huku akisema waraka huo una mazuri mengi japo umechanganya dini na siasa. Kadinali Pengo ameyasema hayo wakati akiadhimisha ibada ya Jumapili ya matawi huko Bagamoyo katika tamasha la vijana. "Katika wiki chache zilizopita watu wamekuja kwangu wakaniuliza unaionaje ile barua ya Maaskofu kuhusu Kwaresma mwaka huu? Ninazungumzia hilo na wala mtu asiende aka-quote kitu kingine ndio maana nataka kusema wazi kabisa:- "Barua ile ijapokuwa hata jina langu mnaliona limeandikwa pale kwamba na mimi ni mmoja wa waandishi au watamkaji...mimi nimeipokea, baadhi yenu mmeshaipokea. " Kwahiyo sioni namna gani mimi naweza kuwa mwandishi au mhubiri kwenu wa ile barua ambayo imetungwa labda na maaskofu...naamini na baad
https://uhakika media.blogspot.com