Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 17, 2018

Mwenyekiti wa chadema atimuliwa

Mwenyekiti wa Chadema atimuliwa uhakika media 1  · 6 hours ago Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia baraza kuu la uongozi Mkoa wa Morogoro limemvua James Mkude nafasi aliyekuwa akiishika ya Mwenyekiti wa Manispaa ya Morogoro kutokana na tuhuma za kujihusisha na matukio yaliyo kinyume na katiba ya chama hicho.  Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mlimba Suzani Kiwanga na kusema hatua hiyo imekuja baada ya kujiridhisha na tuhuma zilizo wasilishwa ndani ya chama hicho ingawa ni tuhuma binafsi zinazomkabili mwenyekiti huyo aliyesimamishwa na kwamba hazihusiani na chama.  Akitoa maadhimio ya wajumbe wa baraza la uongozi la chama hicho mkoa wa Morogoro waliokutana kujadili muenendo wa mwenyekiti huyo, Bi. Suzani amesema kuwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ya mwaka 2006 toleo la mwaka 2016 kifungu cha saba pamoja na maadili ya uongozi kinatoa mamlaka kwa baraza hilo kumsimamisha mtu yeyote atakae kiuka maadili

Waganga wa Jadi wachangia vifo na migogoro katika jamii

Waganga wa jadi huchangia ongezeko la vifo na migogoro katika jamii Uhakika media  · 6 hours ago Wananchi wa Kijiji cha Bukuba  Wilaya ya Buhigwa katika  Mkoa  Kigoma wameonywa vikali kwenda  kwa waganga wa jadi kupata matibabu kwani huchangia ongezeko la vifo katika jamii hasa kwa Mama na watoto.  Akizungumza na Wandishi wa Habari katika Uzinduzi wa Zahanati ya Ilakoze kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mratibu wa Damu Salama wilayani humo Bw. Notas Makuna amewataka wananchi kutotumia waganga wa kienyeji kutibu matatizo yao badala yake watumie vituo vya afya na zahanati zilizopo kumaliza matatizo hayo.  Joshua  Kabega ni Mkazi wa Kijiji hicho alisema walikua wanatembea  umbali mrefu kutafuta huduma ya  afya, na kutumia   gharama za matibabu pamoja na ukosefu wa madawa kwa wakati, zitapungua baada ya kuanzishwa kwa Zahanati mpya ndani ya kijiji hicho.  “Tunashukuru sana kwa kujengwa kwa zahanati hii tutafaidika sana hasa katika kijiji chetu cha Bukuba, Kibuye na Nya

Urusi yaweka vikwazo vipya

Urusi yawekewa vikwazo vipya Uhakika media 2  · 2 hours ago Muakilishi wa Marekani Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema kuwa Marekani itaiwekea vikwazo vipya Urusi na mashirika mengine ambayo yanahusika na  mpango wa sialaha za kemikali nchini Syria.  Hayo Nikki aliyazungumza Jumapili na kusema kuwa vikwazo mihvyo huenda vikachukuliwa Jumatatu.  Katika mahojiano aliofanya katika runinga ya CBS News, Nikki  amesema pia kuwa malengo ya Marekani Syria haijawahi kuwa kumuondoa madarakani Assad bali kuzuia  vita na kutuma ujumbe. Ujumbe ambao haukufafanualiwa.  Akizungumza kuhusu Marekani na Syria  uwezekano wa maazungunzo, Haley amesema kuwa serikali ya Assad haina umuhimu  kushirikishwa  katika  mazungumzo Washington.

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari mpya

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari mpya Uhakika media 2  · 2 hours ago Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali unaozidi km 40 kwa saa katika maeneo yote ya pwani kuanzia saa 24 zijazo kutoka sasa.  Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Jumatatu) na kudai kutakuwepo vipindi vya mvua kubwa katika saa 24 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam, Pwani, Tanga Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.  Mbali na hilo, TMA imesema kuna tarajiwa vipindi vifupi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Kigoma, Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Arusha na Manyara huku upepo wa pwani unatarajiwa kuvuma kutoka kusini kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote.

VIDEO:Mbowe na viongozi wengine wa chadema wakitoka mahakamani

VIDEO: Mbowe na viongozi wengine chadema wakitoka Mahakamani Uhakika media 3  · 5 hours ago Kufutia kesi inayoendelea kuhusu Mwenyekiti wa chadema na wenzake, Mh. Freeman Mbowe, leo kesi yao imesikilizwa mahakama ya kisutu na kughairishwa hadi siku ya tarehe 17/ April/ mwaka huu ndio siku kesi hiyo itaendelea kusikilizwa.  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...............USISAHAU KUSUBSCRIBE....................

VIDEO: Watu 9 wafariki nyumba kujaa maji kutokana na mvua zinazo endelea

VIDEO: Watu 9 wamefarika, nyumba kujaa maji kutokana na Mvua Zinazoendelea Uhakika media3  · 2 hours ago Watu wapatao 9 wameripotiwa kufa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa takribani siku tatu mfululizo jijini dar es salaam, ambapo wengine wameripotiwa kuangukiwa na ukuta wakiwemo mama na mtoto wakiwa wamelala na mwingine kuteleza kwenye daraja, hayo yamesemwa na kamanda kanda maalum ya Dar es salaam SACP Lazaro Mambosasa leo jijini dar es salaam.  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..............USISAHAU KUSUBSCRIBE.....................

Jengo la ghorofa 10 hatarini kuanguka wakazi wahamishwa barabara yafungwa Dar

VIDEO: Jengo la ghorofa 10 hatarini kuanguka wakazi wahamishwa,Barabara yafungwa Dar uhakika media 1  · 1 hour ago Familia zaidi ya kumi leo zimekuwa kwenye taharuki jijini Dar es salaam baada ya nondo za nguzo ya nyumba ya ghorofa 10 kupinda na kupelekea kuhatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.... USISAHAU KUSUBSCRIBE

Makonda ashuhudia mafuriko Dar awapa pole waathirika

Makonda ashuhudia mafuriko Dar awapa pole waathrika Uhakika media 2  · 15 minutes ago Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wahanga wa mafuriko na kuwataka wananchi waishio maeneo ya mabondeni kuhama ili kuokoa maisha yao.  Makonda amesema kuwa hadi sasa zaidi ya watu 7 wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo ambapo amesema njia pekee iliyobaki ni wananchi kuchukuwa tahadhari.  Kufuatia mwendelezo wa mvua hizo  Makonda ameziomba mamlaka husika kusimamisha  masomo kwa muda wa siku mbili ili kuwaepusha wanafunzi kukumbwa na Maafa.  Aidha   Makonda amesema serikali inaendelea na ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya na mvua ikiwemo madaraja, Barabara,shule pamoja na kuzibua mitaro.  Akiwa Mtaa wa Mfaume Kata ya upanga  Makonda ameshuhudia jengo la gorofa kumi likiwa limepata hitilafu ya kutitia ambapo ameagiza  mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina na kuwasihi wakazi wa jengo hilo pamoja

VIDEO: CHADEMA yakanusha kuhusika na ufisadi

VIDEO: CHADEMA Yakanusha Kuhusika na Ufisadi Uhakika media 1  · 1 hour ago Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimekanusha taarifa ya kuwahusisha na ufisadi iliyotolewa na mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde bungeni akinukuu ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali CAG. Mkurugenzi wa utawala na fedha Chadema, Rodrick Lutembeke amekanusha tuhuma hizo.  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KUSUBSCRIBE

Nyuma zaidi ya 17 zasombwa na maji Dar

VIDEO: Nyumba zaidi ya 17 zasombwa maji Dar, Makonda ashuhudia Jangwani, Vingunguti Uhakika media  5  · 35 minutes ago Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wahanga wa mafuriko na kuwataka wananchi waishio maeneo ya mabondeni kuhama ili kuokoa maisha yao.  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI ......USISAHAU KUSUBSCRIBE