Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 15, 2018

Monalisa ambwaga Lupita Nyong'o

Monalisa ambwaga Lupita Nyong'o Uhakika media 5  · 7 hours ago Mrembo na muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama 'Monalisa'  ameibuka mshindi kwenye tuzo za 'The African Prestigious Awards' nchini Ghana akimbwaga mpinzani wake Lupita Nyong'o.  Katika tuzo hizo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo huko jijini Accra nchini Ghana Monalisa ametwaa tuzo katika kipengele cha 'Best African Actress'. Kwa mujibu wa tuzo hizo Monalisa sasa ndiye muigizaji bora wa kike barani Africa.  Monalisa amethibitisha ushindi wake kupitia mtandao wa 'Instagram' ambapo amepandisha picha akiwa na tuzo yake na kuandika ujumbe huu ''Tumeshindaaaaaaa narudi home na Tuzo za kutosha.Ahsante Watanzania,Nawapenda mno''.  Kwa ujumbe huo wa Monalisa unaashilia huenda pia kuna tuzo nyingine wameshinda Watanzania ambao walikuwa wanawania vipengele mbalimbali katika tuzo hizo kubwa za filamu nchini Ghana.  Watanzania wengin

Magazeti ya leo 15/4/2018

MAGAZETI YA LEO 15/4/2018 Uhakika media · 10 hours ago

Nafasi za kazi zilizo tangazwa leo

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo uhakika medi  5  · 52 minutes ago Bonyeza Links zifuatazo:   Scholarships for Tanzanians - April 2018   Job Opportunity at TJL Company Accountants   2 Job Opportunities at Pact Tanzania   3 Job Opportunities at Save the Children Tanzania, April 2018   Nafasi zingine Ingia  www.ajirayako.co.tz    

Hii ndiyo kauli ya Lissu baada ya B. Fatma Karume kutangazwa msindi wa Urais TLS

Hii ndio kauli ya Lissu baada ya Bi. Fatma Karume kutangazwa mshindi wa urais wa TLS Uhakika media 5  · 46 minutes ago Jana Aprili 14, 2018 Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilipata Rais mpya mteule Bi. Fatma Karume, Hatimaye Mhe. Tundu Lissu ambaye ndiye aliyemuachia kiti hicho ametoa pongezi kwa wanachama wa TLS.  Mhe. Lissu ambaye yupo hospitalini nchini Ubelgiji tangu mwezi Januari mwaka huu, amesema kuwa uchaguzi huo umethibitisha kuwa TLS ni chama ambacho kinaweza kujisimamia na kujiendesha bila kuingiliwa na mtu.  “Napenda kuwapongeza wanachama wote wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kwa kumchagua Bi. Fatma Karume kuwa Rais mpya wa TLS. Uchaguzi huu umethibitisha, kwa mara nyingine tena, umuhimu wa Chama cha kitaaluma cha mawakili kujisimamia na kujiendesha bila kuingiliwa,“ameeleza Tundu Lissu na kutoa pongezi kwa Bi. Fatma .  “Namtakia Rais Mteule Fatma Karume kila kheri katika kutelekeza majukumu yake mapya na muhimu katika kipindi hiki cha historia ya nchi ye

Ronaldo na Bale waachwa nje ya kikosi

Ronaldo na Bale waachwa nje ya kikosi Uhakika media  5  · 34 minutes ago Kocha wa Mabingwa watetezi wa La Liga Zinedine Zidane, amepangua kikosi chake na kuwaacha nyota Cristiano Ronaldo na Gareth Bale kuelekea mchezo wao wa ligi leo dhidi ya Malaga.  Zidane amewapa mapumziko nyota hao baada ya kuisadia timu hiyo kushinda mchezo wa robo fainali dhidi ya Juventus na kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya jumatano iliyopita.  Kiungo Luka Modric pia ameondolewa kwenye kikosi cha wachezaji 20 hivyo kufanya timu hiyo kusafiri kwenda La Rosaleda na wachezaji 19 pekee. Inaaminika nyota hao watatu wameachwa ili kuwapa nafasi ya kuwa vizuri kwenye mechi dhidi ya Bayern Munich.  Real Madrid ambayo inashika nafasi ya 4 leo inaweza kurejea katika nafasi ya 3 endapo itaibuka na ushindi huku Malaga inapigania kukwepa kushuka daraja ikiwa inaburuza mkia.

Israel yaiunga mkono Marekani

Israel yaiunga mkono Marekani Uhakika media 5  · 29 minutes ago Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake inaunga mkono mia kwa mia uamuzi wa Marekani kuishambulia serikali ya Assad.  Waziri Netanyahu amesema Israel inaunga mkono uamuzi huo wa Marekani ulioungwa mkono na Ufaransa pamoja na Uingereza.  "Tumekuwa tukiunga mkono uamuzi wa Trump dhidi ya silaha za kemikali toka mwaka mmoja uliopita",alisema Netanyahu.  Israel inaamini serikali ya Assad inapashwa kudhibitiwa vilivyo ili kuhakikisha kuwa haitumii silaha za kemikali dhidi ya halaiki.  Marekani,Uingereza na Ufaransa zimefanya shambulizi la anga dhidi ya serikali ya Assad nchini Syria.  Hii ni baada ya shambulizi baya la kemikali kutokea Douma na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70 wengi wao wakiwa ni watoto wadogo.

Uturuki yazichunia Urusi na Marekani

Uturuki yazichunia Marekani na Urusi Uhakika media 5  · 26 minutes ago Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt ÇavuÅŸoÄŸlu amesema kuwa nchi yake haichagui Marekani wala Urusi.  Waziri huyo amesema kuwa Uturuki haitofanya chaguo kati ya Marekani na Urusi,Marekani na serikali ya Assad,Ufaransa na Uingereza.  "Lengo letu kuu ni kuleta amani nchini Syria.Hilo ni jambo ambalo Uturuki imelitilia manani",alisema ÇavuÅŸoÄŸlu.  Hayo waziri huyo ameyazungumza wakati akitoa hotuba katika mkutano wa chama cha AK mjini Antalya.  Hapo awali waziri ÇavuÅŸoÄŸlu alisema kuwa mashambulizi ya Marekani ni dhidi ya serikali ya Assad inayotumia silaha za kemikali.  "Tunapashwa kuikoa Syria kutoka katika serikali hiyo",aliongeza ÇavuÅŸoÄŸlu.  Ufaransa,Marekani na Uingereza kwa pamoja zimefanya shambulizi dhidi ya silaha za kemikali za serikali ya Assad nchini Syria.  Hio ni kufuatia shambulizi baya la kemikali lililofanyika Douma na kusababisha vifo vya watu 78 huku wengine wengi wakiwa

Marekani: Tutawashambulia tena

Marekani: Tutawashambulia tena Uhakika media 5  · 20 minutes ago Rais wa Marekani Donald Trump ameiambia serikali ya Syria akisema Marekani iko tayari kuishambulia tena ikiwa itafanya shambulizi lingine la kemikali.  Onyo hilo lilikuja bada ya Marekani, Uingereza ba Ufaransa kushambulia vituo vitatu kujibu shambulizi linaloshukiwa kuwa la kememikali kwenye mji wa Douma wiki moja iliyopita.  Syria inakana kufanya shaambulizi lolote la kemikali na badala yake inasema kuwa lilifanywa na waasi.  Kura iliyoletwa na Urusi kwa Baraza la usalama la Umoja wa Mataiafa, kulaani mashambulizi yaliyoongoznwa na Matekani ilikataliwa.  Mashambulizi hayo ndiyo makubwa zaidi dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad, yaliyofanywa na nchi za magharibi katika kipindi cha miaka saba nchi hiyo imekuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.  Marekani, Uingereza na Ufaransa wamewapa azimio jipya wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, wakitaka kufanya uchunguzi huru kuhusu matumaini ya silaha

BREAKING NEWS: mkurugenzi afariki kwa ajari

BREAKING NEWS: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa afariki kwa ajali Uhakika media 5  · 3 minutes ago Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Ngusa Izengo, amefariki dunia katika ajali ya gari  iliyotokea usiku wa kuamkia leo huko Chalinze-Nyama nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Serikali yatoa boti kusaidia doria

Serikali yatoa boti kusaidia doriadoria Uhakika media 5  · 1 hour ago Picha ya Mtandao   Serikali imetoa boti yenye thamani ya zaidi ya shilingi billion nne ili kusaidia doria katika mwambao wa bahari mkoani Tanga lengo likiwa ni kukabiliana na uingizwaji wa bidhaa zinazopitishwa kwa njia ya magendo ili kukwepa kodi.  Akizungumza mara baada ya kuzindua boti hilo mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa boti hilo linafanya kazi kwa saa 24.  Mhe. Martine Shigela amesema kuwa kwa sasa wafanyabiashara wa magendo wasifikiri tena kuna njia katika pwani ya bahari Hindi hivyo ameagiza meli hiyo ifanye kazi ipasavyo.  Kwa upande wake meneja wa bandari mkoa wa Tanga Percival Salama amesema uboreshaji wa Bandari hiyo unaoendelea ambapo mpaka sasa ujenzi wa gati namba mbili unaoendelea bandarini hapo umefikia karibu asilimia 70 wa wanatarajia ifikapo mwezi wa sita itakua imekalika.

ACT Wazalendo watoa mapendekezo haya kwa CAG

ACT Wazalendo Watoa mapendekezo yao, wabaini maeneo nane hatari katika ripoti ya CAG Uhakika media  5  · 8 minutes ago Leo Jumapili Aprili 15, 2018 Chama cha ACT Wazalendo kimetoa tathmini na uchambuzi wake juu ya ripoti  mpya ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17.  Soma taarifa hiyo iliyotolewa leo Aprili 15, 2018 na Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe.  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, Prof. Mussa Assad ametoa taarifa yake ya ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwa mwaka 2016/17. Kwa sasa taarifa hiyo iko wazi kwa umma, baada ya kuwa imekabidhiwa rasmi bungeni. Sisi ACT Wazalendo, tumeisoma, kuipitia na kuichambua taarifa husika, kwa lengo la kuitumia ili itusaidie kutimiza wajibu wetu wa kuisimamia Serikali, kama chama cha Upinzani bungeni.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu Magufuli tayari amechukua hatua za kiuwajibikaji dhidi ya baadhi ya Watendaji wa Mamlaka za Serikali z

ACT Wazalendo watoa mapendekezo haya kwa CAG

ACT Wazalendo Watoa mapendekezo yao, wabaini maeneo nane hatari katika ripoti ya CAG Uhakika media 5  · 8 minutes ago Leo Jumapili Aprili 15, 2018 Chama cha ACT Wazalendo kimetoa tathmini na uchambuzi wake juu ya ripoti  mpya ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17.  Soma taarifa hiyo iliyotolewa leo Aprili 15, 2018 na Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe.  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, Prof. Mussa Assad ametoa taarifa yake ya ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwa mwaka 2016/17. Kwa sasa taarifa hiyo iko wazi kwa umma, baada ya kuwa imekabidhiwa rasmi bungeni. Sisi ACT Wazalendo, tumeisoma, kuipitia na kuichambua taarifa husika, kwa lengo la kuitumia ili itusaidie kutimiza wajibu wetu wa kuisimamia Serikali, kama chama cha Upinzani bungeni.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu Magufuli tayari amechukua hatua za kiuwajibikaji dhidi ya baadhi ya Watendaji wa Mamlaka za Serikali za

ACT Wazalendo watoa mapendekezo haya kwa CAG

ACT Wazalendo Watoa mapendekezo yao, wabaini maeneo nane hatari katika ripoti ya CAG Uhakika media 5  · 8 minutes ago Leo Jumapili Aprili 15, 2018 Chama cha ACT Wazalendo kimetoa tathmini na uchambuzi wake juu ya ripoti  mpya ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17.  Soma taarifa hiyo iliyotolewa leo Aprili 15, 2018 na Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe.  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, Prof. Mussa Assad ametoa taarifa yake ya ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwa mwaka 2016/17. Kwa sasa taarifa hiyo iko wazi kwa umma, baada ya kuwa imekabidhiwa rasmi bungeni. Sisi ACT Wazalendo, tumeisoma, kuipitia na kuichambua taarifa husika, kwa lengo la kuitumia ili itusaidie kutimiza wajibu wetu wa kuisimamia Serikali, kama chama cha Upinzani bungeni.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu Magufuli tayari amechukua hatua za kiuwajibikaji dhidi ya baadhi ya Watendaji wa Mamlaka za Serikali za