Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 21, 2018

MBINU 10 ZA KUONGEZA MBEGU ZA KIUME

Mbinu 10 za kuoongeza mbegu za kiume (sperm count) Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua milioni 20, chochote chini ya hapa kinaweza kuwa sababu ya kutokutungisha ujauzito. Ikitokea umegundulika kuwa na mbegu chache, ni nyepesi sana na hazina nguvu za kukimbia vya kutosha basi makala hii itakupa maelezo juu ya mbinu 10 zinazoweza kukusaidia kuongeza uwingi wa mbegu zako bila gharama yoyote. Visababishi vya mbegu kuwa chache: Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, kwa bahati nzuri vingi ya vitu hivyo tunao uwezo wa kuvidhibiti kwa kupunguza matumizi yake. Vitu hivyo ni pamoja na: • Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume. Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta. Unashauriwa kutokuweka

MBINU 11 ZA KUPUNGUZA UZITO NA UNENE BILA KUFANYA MAZOEZI WALA KUFUNGA KULA

MBINU 11 ZA KUPUNGUZA UZITO NA UNENE BILA MAZOEZI WALA KUFUNGA KULA Kuendelea kutegemea mazoezi au kufunga kula au kupunguza kula kunaweza kusiwe msaada kwa baadhi ya wengine wanaotaka kupunguza uzito na unene wa miili yao. Hata hivyo zipo mbinu chache unazoweza kuzitumia na ukaweza kudhibiti uzito wako. Bila kukupigisha stori nyingi hapa chini nakuelezea mbinu hizo bila kuchelewa kama ifuatavyo: Mbinu 11 za kupunguza uzito na unene bila mazoezi wala kufunga kula 1. Kula chakula pole pole Ubongo wako unahitaji muda wa kutosha kushughulika na hilo tendo la kutafuna na kumeza chakula. Kula pole pole kunahusiana moja kwa moja na kuweza kula chakula kichache na kujisikia kushiba. Ni muda gani unatumia kumaliza chakula chako unaweza kuathiri pia uzito wako. Utafiti unaonyesha watu wanaokula kwa haraka haraka hutokewa kuwa na uzito mkubwa pia ukilinganisha na wale wanaokula pole pole. Jaribu hii haitakugharimu kitu. 2. Tumia sahani ndogo kwa vyakula visivyo na afya Kama itakutoke

Faida ya mboga ya mchicha ni dawa ya kutibu maradhi mengi

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA. Uhakika media   /   2 years ago MBOGA YA MCHICHA HUTIBU MARADHI YAFUATAYO Kuumwa mgongo Kusafisha njia ya mkojo Kusafisha damu Unatibu tigo Unatibu minyoo Unatibu damu Baridi yabisi Tezi la shingo Homa Kuongeza damu Unatibu maumivu Tonic ya nywele Unasaidia kupata haja ndogo kwa wingi MATAYARISHO Chukua mchicha kilo 1 chemsha maji lita 2 na nusu. Yakichemka loweka mchicha kwa dakika 15. Tumia kikombe. Ni bora utumie yote kwa siku . Dozi ni siku 5 KUTIBU MGONGO Chukua mchicha ponda. Chua mara 3 kwa siku. Usiku unapasha moto mchicha kisha unufunga mahali panapouma. Lala nao wakati vuguvugu la joto lake lenye maji ndani (dawa) ikiingia ndani fanyahivyo kwa siku 5, ukibadilisha kila siku (fresh) TIBA YA TEZI LA SHINGO Chukua mchicha kiasi kidogo, ponda, fungia shingoni pale penye uvimbe wakati unapolala kwa kitambaa, kwa muda wa si

Uteuzi alioufanya Rais Magufuli leo

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu asubuhi ya leo March 21, 2018 ni kwamba Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation – NHC) Blandina Nyoni kuanzia leo Pia Rais Magufuli ameivunja Bodi ya shirika hilo la NHC kuanzia leo. Taarifa hiyo inaeleza kiwa uteuzi wa Mwenyekiti na bodi nyingine utafanyika baadaye.

Ronaldo baada ya ushindi wa tuzo ya pili Ureno

Staa wa soka wa  Ureno  club ya  Real Madrid  ya  Hispania Cristiano Ronaldo  usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kushinda tuzo ya pili mfululizo ya mchezaji bora wa taifa la Ureno 2017 . Tuzo hiyo  Ronaldo  anashinda ikiwa ni miaka mitatu imepita toka shirikisho la soka  Ureno  litangaze kumpa tuzo ya heshima ya mchezaji bora wa Ureno  wa muda wote. Ronaldo aliambatana na mpenzi wake Georgina Rodriguez Ronaldo  ameshinda kwa asilimia 65 huku  Patricio  akipata asilimia 18 na Bernardo Silva  wa  Man City  akipata asilimia 17, baada ya ushindi huo Ronaldo aliulezea mwaka 2017 kuwa ni moja kati ya miaka yake mizuri kisoka. “Binafsi mwaka 2017 ni mwaka ambao hauwezi kusahaulika kwangu baada ya kuiwezesha Ureno kufuzu kucheza Kombe la dunia na kushinda mataji matano nikiwa na Real Madrid”>>>   Ronaldo

Pogba ni kweli hana raha kuchezea man united

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa  Didier Deschamps amenukuliwa na vyombo vya habari mbalimbali duniani akimzungungumzia kiungo wake wa kimataifa  Paul Pogb a anayeichezea Man United  ya  England  na atamsaidia kumfanyia counselling kipindi hiki cha mapumziko mafupi. Pogba  imeripotiwa hana raha baada ya kocha wa  Man United  Jose Mourinho  kumuweka benchi katika game mbili zilizopita baada ya kuikosa game ya  Liverpool  kwa majeruhi hivyo  Didier Deschamps amemwambia  Pogba  aweke pembeni mawazo hayo kabla ya game za Ufaransa  za kirafiki dhidi ya  Colombia na  Urusi . “Nimekuwa na utamaduni wa kufanya majadiliano ya kina na wachezaji kila ninapowaita timu ya taifa kwa sababu huwa sina taarifa zao zote, nimewaambia mchana huu kuwa ni mapumziko ya mechi za kimataifa na kila kitu kinachohusu ishu za vilabu vyao havipo, hali iliyopo kwa sasa Pogba hana furaha nayo”>>>  

Bakari Malima atoa neno kuhusu yanga kucheza kombe la shiirikisho Afrika

Bakari Malima atoa neno Yanga kucheza Kombe la Shirikisho Afrika Uhakika media 2  · 10 hours ago Mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakali Malima 'Jembe Ulaya', amesema haipi nafasi Yanga ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.  Yanga imeangukia kwenye michuano hiyo baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers kwa mabao 2-1.  Akizungumza na kipindi cha michezo kupitia Radio One, Malima amesema haoni nafasi ya Yanga kusonga mbele kutokana na vigogo waliopo kwenye mashindano hayo.  Baadhi ya timu kongwe na kubwa zilizopo ni Enyimba FC, Raja Cassablanca na USM Algier na Al Masry SC iliyowatoa Simba.  Droo ya upangaji wa timu zitakazokutana kwenye mashindano hayo inataraji kufanyika kesho Jumatano mjini Cairo Misri.

Serikali yatoa neno kushambuliwa kwa afisa wa sirya

Serikali yatoa neno kushambuliwa afisa wa Syria Uhakika media 2  · 10 hours ago Baada ya kuwepo kwa taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kushambuliwa kwa afisa wa ubalozi wa Syria nchini Tanzania na watu watatu wasiojulikana na kupigwa ikiwa pamoja na kuporwa pesa, simu na gari aliyokuwa akiitumia kwa shughuli za ubalozi.  Kufuatia taarifa hizo Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abasi amefunguka na kukiri kupata taarifa hizo na kudai kuwa serikali inafuatilia suala hilo na itatoa taarifa kamili kuhusu jambo hilo. "Umma unaarifiwa kuwa vyombo vya dola vinafuatilia taarifa za Afisa Ubalozi wa Syria nchini kushambuliwa, kuporwa. Taarifa kamili itatolewa" alisema Abasi  Aidha katika taarifa za awali zinadai kuwa afisa huyo amelazwa katika hospitali ya Agha Khan akipatiwa matibabu kufuatia shambulio hilo

Yanga TV kuzinduliwa rasmi

VIDEO: Yanga TV kuzinduliwa rasmi Uhakika media 2  · 10 hours ago Klabu soka ya Yanga imezindua programu maalum ikijiunga kidigitali katika kutoa taarifa za timu hiyo kwa mashabiki wake na kuiingizia kipato timu yao, hata hivyo kufuatia uzinduzi huo pia na jitihada za viongozi ya kuletea maendeleo ambapo iliambatana na minong'ono ya mda mrefu sasa imefikia mwisho ambapo Aprili Mosi mwaka huu klabu hiyo kongwe zaidi nchini inatarajia kuzindua TV ambapo mashabiki na watanzania kiujumla wataijua Yanga kupitia Yanga TV.  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......... USISAHAU KUSUBSCRIBE

Jinsi ya kuwa mzungumzaji bora

Jinsi ya kuwa mzungumzaji bora Uhakika media 2  · 5 hours ago Wapo baadhi ya wasomaji wangu walikuwa wakiniuliza "eti nifanye nini ili kuwa mzungumzaji mzuri mbele ya watu wengine?  Swali hili kiukweli limekuwa likiwatatiza watu wengi sana kwa namna moja ama nyingine.  Na kutokana na hali hiyo kumewafanya watu hao hao kuwa katika hali unyonge,  kwani huisi watachekwa na sababu nyingine kama hizo.   Lakini ukweli ni kwamba endapo utazijua siri hizi kuwa mzungumzaji bora zitakwenda kukusaidia kutoka katika hali uliyonayo hatimaye kuwa mzungumzaji mzuri.   Zifuatazo ndizo mbinu kuwa mzungumaj bora:   1.kuwa na taarifa za uhakika na kutosha.   Moja ya  njia bora ya kuwa mzungumzaji mzuri ni kuwa na utajiri wa vitu vingi katika kibubu cha ubongo wako . Watu wengi wanajiona hawawezi kuchangia maada yeyote ile mbele ya wengine hii ni kwa sababu wamekuwa hawana taarifa sahihi na za uhakika za kuweza kuzungumza. Hivyo Kama endapo nia yako ni kutaka kuzungumza mambo mbalimbali katika

Magazeti ya leo 21/3/2018

MAGAZETI YA LEO 21/3/2018 Uhakika media  · 51 minutes ago

Kilimo cha nanasi

MCHANGANUAO WA KILIMO BORA CHA NANASI NA FAIDA UTAZOZIPATA Uhakika media  /  31 minutes ago Leo naomba niweke mkusanyiko wa mada za kilimo.. nimeamua kufanya hivi ili kusaidia wale ambao ni wanachama wapya na wanachama wengine ambao wanataka kujikumbusha mada hizo na kuchukua hatua: Tukumbuke!! TUKIWEKA JITIHADA.. KILIMO KINALIPA!!.nawapeni mfano: unaenda Kiwangwa bagamoyo unanunua ekari moja ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha nanasi. gharama zitakuwa hivi: ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- (ekari ni hatua 70x70) utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/= gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji), Mbolea 100,000. matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni). jumla 1,500,000/- Mapato nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumpt

homa ya mapafu kwa watoto

HOMA YA MAPAFU KWA WATOTO PNEUMONIA FOR KIDS Uhakika med  /  2 weeks ago Homa ya mapafu ni aina ya maambukizi yanayoathiri mapafu. Ni ugonjwa ambao unaua watoto wengi hasa katika nchi zinazoendelea duniani. Inakadiriwa kwamba watoto karibu milioni 1.6 walio chini ya miaka 5 wanakufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu. Kutokana na vifo vingi vinavyotokana na homa ya mapafu tarehe 12 ya mwezi wa Novemba kila mwaka imefanywa kuwa siku rasmi ya homa ya mapafu duniani, ambapo nembo ya siku hiyo ni nguo za rangi ya bluu. Muundo wa Mapafu Mapafu yanajumuisha mirija mikubwa ya hewa ( bronchi ) ambayo hugawanyika kufanya mirija midogo zaidi ya hewa ( bronchioles ), ambayo nayo hutengeneza vifuko vidogo vidogo ya hewa ( alveoli ). Vifuko hivi vidogo vya hewa ( alveoli ) vina mishipa ya kupitisha damu ( capillaries ) ambayo husaidia kuchuja na kusafirisha hewa safi ya oksijeni tunayovuta kuingia kwenye damu na hewa chafu ya ukaa (kaboni dioksidi) kuondolewa kwenye damu na kuin