Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 27, 2018

Makamu wa Rais awapa somo mashirka ya umma

Makamu wa Rais awapa somo viongozi wa mashirika ya umma Uhakika media 5  · 34 minutes ago Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi kuwaruhusu wafanyakazi kushiriki michezo katika maeneo yao ya kazi lakini pia kuwaruhusu wafanyakazi hao kushiriki Michezo ya SHIMMUTA.  Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) mjini Dodoma.  Makamu wa Rais amesema michezo ni muhimu sana kwenye Tanzania ya Viwanda kwani michezo husaidia mwili kuwa wenye afya bora na utendaji wao wa kazi unakuwa mzuri zaidi.  Makamu wa Rais amesema yeye alikuwa mwanamichezo mzuri wa mpira wa pete (Netball) lakini kwa sasa anafanya mazoezi kidogo kidogo asubuhi na jioni.  “Najua Umuhimu wa kufanya mazoezi kwa sababu nikiacha kufanya mazoezi nadorora na katika nafasi hii ukidorora unadorora mpaka akili na

VIDEO: SERIKALI YA JPM YAJIPANGA

VIDEO: Serikali ya JPM kujiimarisha Katika sekta ya Viwanda kwa Vijana Kupitia TICE Uhakika media 3  · 14 minutes ago Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji ikishirikiana na taasisi ya TICE wamesema watafanya maonyesho ya ubunifu na uvumbuzi, yatakayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja, jijini Dar es salaam. siku ya tarehe ishirini na saba hadi tarehe ishirini na tisa mwezi wa nne mwaka huu, ambapo maonyesho hayo yatazunguka katika mikoa mitano ambayo ni Mwanza, Arusha, Dar es salaam, Mbeya pamoja na Dodoma.  Maonyesho hayo yatahudhuriwa na viongozi wa kiserikali pamoja na balozi mbali mbali, ambapo waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Mh. Charles Mwijage ndie atakae yafungua maonyesho hayo ambayo yatasaidia kuinua vipaji na kuonyesha uvumbuzi mbali mbali kutokwa kwa vijana wa kitanzania kujionyesha mambo makubwa wanayoweza kuyafanya.  Hayo yamesemwa na afisa mawasiliano wa wizara hiyo Bw. Edward Nkomola wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Taxif

Nafasi za ajira

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo Uhakika media 5  · 20 minutes ago Bonyeza Links zifuatazo:   13 Job Opportunities at CVPeople Africa, Project Oficers   Job Opportunity at Kazini Kwetu Tanzania   3 Job Opportunities at Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT)   Nafasi zingine Ingia  www.ajirayako.co.tz  

Nafasi za ajira

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo Uhakika media 5  · 20 minutes ago Bonyeza Links zifuatazo:   13 Job Opportunities at CVPeople Africa, Project Oficers   Job Opportunity at Kazini Kwetu Tanzania   3 Job Opportunities at Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT)   Nafasi zingine Ingia  www.ajirayako.co.tz  

BREAKING NEWS

BREAKING NEWS: Rais Magufuli awatumbua Wakurugenzi Uhakika media 5  · 4 hours ago Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr,John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo kuwasimamisha kazi Wakurugenzi wawili wa Kigoma Ujiji na Pangani kwa sababu ya kupata hati chafu katika ripoti ya CAG iliyowasilishwa leo.  “Kuna Wilaya mbili, Halmashauri Mbili zina hati chafu, Mimi nafikiri Kigoma Ujiji na Pangani, Mimi nafikiri saa nyingine tuchukue hatua kwa vile Waziri wa TAMISEMI upo hapa WAKURUGENZI wa Wilaya hizo WASIMAMISHWE kazi leo” -Rais Magufuli

VIDEO: EXCLUSIVE LIPUMBA ACHALUKIA MAANDAMANO YA APR 26

VIDEO: EXCLUSIVE: LIPUMBA Ayacharukia Maandamano ya April 26 Uhakika media 1  · 4 hours ago Kufuatia kuzidi kusambaa kwa taarifa za kuwepo kwa maandamano Aprili 26 mwaka huu, mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama, Profesa Ibrahim Lipumba amejitokeza na kuwashukia wale wanaohamasisha maandamano hayo akisema yanapaswa kuongozwa na taasisi au chama tawala na siyo mtu ambaye hata Tanzania hayupo. Lipumba amewataka wananchi kuwa makini ili wasije wakapata madhara siku hiyo.  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..USISAHAU KUSUBSCRIBE

Huu ndio undani wa aliye muua mkewe na kumficha mbuyuni

Huu ndio undani wa aliyemuua Mkewe na kumficha Mbuyuni Uhakika media 5  · 2 hours ago UNDANI wa mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina Bernard Shumba mkazi wa Singida kugundulika na jeshi la polisi mkoani humo kuwa amemuua mke wake miaka minane iliyopita kisha kuufi cha mwili wa marehemu kwenye mbuyu, umeanikwa.  Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema Shumba alikuwa mara kwa mara akiwa kwenye vilabu alikuwa akigombana na mtu anasema kwamba anaweza kumfanyizia kama alivyomfanya mkewe.  Kutokana na tambo zake hizo raia wema waliamua kuliarifu jeshi la polisi ambalo kwa weledi mkubwa walithibitisha kile alichokuwa akisema Shumba kwani alikwenda kuwaonesha polisi alikomfi cha  mkewe miaka minane iliyopita baada ya kumuua.  “Tuwapongeze polisi kwa kazi nzuri kwa sababu tambo za huyu bwana zimezaa matunda na kuonesha yalipo mabaki ya mkewe,” alisema mtoa taarifa wetu ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.“Nitoe wito kwa wananchi kwamba, watu wabaya wasifi chiwe siri kama bwana,” al

VIDEO: Makonda apambana na viongozi wa serikal dar.

VIDEO: Makonda kupambambana na Wabunge, viongozi wa serikali Dar Uhakika media 1  · 58 minutes ago "Mpaka sasahivi kwa taarifa nilizonazo tunao baadhi ya viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, Wabunge na vingozi wa dini wengi waliowapa kinamama mimba na wakawatelekeza na mtawashuhudia, nafahamu zoezi hili ni gumu na linahitaji watu wa mungu ili kufanikisha" RC Makonda  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHU KUSUBSCRIBE

BEAKING NEWS:

BREAKING NEWS: Viongozi wa Chadema wafikishwa Mahakamani Uhakika media 5  · 1 hour ago Leo March 27, 2018 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.  Viongozi wa CHADEMA wengine waliofikishwa Mahakamani ni Katibu Mkuu Dr. Vincent Mashinji, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalim, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa na Ester Matiko Mbunge. 

mbinu za kutengeneza shape

MBINU ZA KUTENGENEZA SHAPE YAKO UNEKANE WA KISASA Published by: uhakika media PENDEZA NA KESSY PRODUCT: Weka muonekano wako vizuri sasa, wauzaji wa products za asili na mafuta yasio na madhara yeyote wala kemikali kwa matumizi na matokeo ni kwa araka kuanzia wiki mbili hadi nne. 1) Kutoa mvi sugu pia za kuzaliwa nazo  Tsh. 100,000/= 2) Kurefusha nywele kuzijaza na kuzuia kukatika Tsh. 100,000/= 3) Kutengeneza shepu kuwa na umbo zuri (hips & batks), wana dawa ya aina tatu(@)Kupaka Tsh. 100,000/=, (b) Kunywa (c) Vidonge Tsh. 130,000/= 4)Kuondoa nyama uzembe mikononi, kiunoni. Dawa ya kupaka Tsh. 100,000/= 5) Kuondoa kitambi kabisa (@) Kupak Tsh. 10o,000/=, (b)Vidonge/sliming majan Tsh. 130,000/=. 6) Kupunguza mwili mzima kuanzia kilo unazoitaji wewe @) Dawa ya maji na vidonge Tsh. 30,000/= 7)Kupunguza matiti na yasimame kama mwanzo Tsh. 90,000/= 8) Kuongeza maziwa saizi unayohitaji wewe Tsh. 90,000/= 9)Kuongeza unene wa mwili mzima  Tsh. 100,000/= 10) Kuondo

Breking news

MBOWE, MASHINJI, MNYIKA NA WENGINE WAWEKWA MAHABUSU SENTRO March 27, 2018 by Global uhakika media MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa chama hicho akiwepo Katibu Mkuu Dkt Vincent Mashinji, John Mnyika, Salum Mwalimu na Ester Matiko wamewekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha polisi Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha hilo na kusema kuwa viongozi hao wamewekwa mahabusu leo Machi 27, 2018 baada ya kuripoti Kituo Kikuu Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao. “Viongozi Wakuu wa Chama pamoja na wabunge waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao, wamewekwa mahabusu. Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Mawakili wetu wanashughulikia. Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi,” alisema Makene.

Breaking news

JPM AWASIMAISHA KAZI WAKURUGENZI HALMASHAURI KIGOMA UJIJI, HANDENI March 27, 2018 by uhakika media IKULU: Rais Magufuli amewasimamisha kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Kigoma Ujiji na Pangani baada ya kuandikiwa hati chafu kwenye Vitabu vya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyowasilishwa leo.
Breaking news: ABDUL NONDO ASIMAMISHWA MASOMO CHUO KIKUU March 27, 2018 by Global Publishers Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye, amemsimamisha masomo Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo hadi kesi yake ya kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kutekwa itakapomalizika. Nondo alipewa dhamana na mahakama ya Iringa, jana Jumatatu,Machi 2018 baada ya kusota rumande kwa wiki kadhaa. TAARIFA YA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM

Ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi

UGONJWA WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI NA NAMNA YA KUJIKINGA March 27,02018 by uhakika media SARATANI ya shingo ya kizazi ni aina ya saratani ambayo hushambulia sehemu ya viungo vya uzazi vya mwanamke inayounganisha kati ya uke na mfuko wa mimba (uterus). Ugonjwa huo husababishwa na virusi vya HPV(human papilloma virus). Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (W.H.O), saratani ya shingo ya kizazi ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi duniani. Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya vifo hivi hutokea katika nchi zinazoendelea. Mwanamke anapopata maambukizi ya HPV(Human Papilloma Virus), kwa mara ya kwanza kinga yake hujaribu kupambana na virusi hawa ili wasilete madhara,virusi hawa wasipodhibitiwa mapema huanza kushambulia seli za shingo ya kizazi na kusababisha ukuaji wa seli za saratani katika eneo hili. VIHATARISHI VYA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha mtu akapata ugonjwa wa saratani ya shingo ya k

Chango la uzazi

UGONJWA WA CHANGO LA UZAZI KWA WANAWAKE! March 27, 2018 by uhakika media CHANGO la uzazi ni miongoni mwa magonjwa yanayoshambulia viungo vya uzazi vya mwanamke ambapo humsababishia maumivu makali ya tumbo na kushindwa kupata ujauzito, au mimba kuharibika kila zinapoingia. Zipo aina nyingi za chango ambazo zinaweza kujitokeza kila moja peke yake au zikajikusanya na kujitokeza kwa pamoja, mkusanyiko huu ndiyo unaitwa Ovulation Disorder (O.D). CHANZO CHA TATIZO Matatizo ya chango la uzazi, inatokana na vifuko vya mayai ya uzazi (ovaries) kutokuwa na uwezo wa kuzalisha mayai na kufanya yakue kwa wakati muafaka. Mwanamke mwenye matatizo haya hushindwa kuwa na siku za hatari za kunasa ujauzito na kama zipo basi huwa hazina mpangilio unaoeleweka. Yawezekana mwanamke mwenye tatizo hili akawa na uwezo wa kuzalisha mayai lakini yakashindwa kukomaa au hata yakikomaa yakashindwa kusafiri kwenye mirija ya uzazi kwenda kukutana na mbegu za uzazi za kiume kwa ajili ya kurutubishwa. Tati

TETESI ZA SOKA ULAYA

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 27.03.2018: Marouane Fellaini kuondoka United, Shaw atakwenda Barca? Saa 2 zilizopita Sambaza habari hii Facebook  Sambaza habari hii Twitter  Mshirikishe mwenzako Haki GETTY IMAGES Image Luke Shaw akiwa na Jose Mourinho Barcelona wanapanga kuwasilisha ombi la kutaka kumchukua beki wa Manchester United Luke Shaw mwisho wa msimu. Beki huyo wa kushoro wa miaka 22 kutoka England amekosolewa sana na meneja wa United Jose Mourinho wiki za karibuni. (Mirror) Mabingwa wa Ufaransa Monaco ndiyo klabu ya karibuni zaidi kuonesha nia ya kumtaka kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini. Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 30 kutoka Ubelgiji unamalizika mwisho wa msimu na anatarajiwa kuondoka Old Trafford. (Mail) Dani Ceballos ambaye amekuwa akitafutwa na Liverpool ameambia anaweza kutoka Real Madrid mwisho wa msimu. Kiungo huyo wa kati Mhispania wa miaka 21 amekuwa pia anatafutwa na AC Milan na Juventus. (Mundo Deportivo kupitia Talksport)

Mechi ya Brazil Vs ujerumani

Brazil v Ujerumani: Watalipiza kisasi kichapo cha 7-1 au wataaibishwa tena? Saa 3 zilizopita Sambaza habari hii Facebook  Sambaza habari hii Twitter  Mshirikishe mwenzako Haki GETTY IMAGES Mkufunzi wa Brazil Tite amesema timu yake bado inatatizwa na "mizimu" ya kipigo cha 7-1 ambacho walipokezwa na Ujerumani katika nusu fainali ya Kombe la Dunia miaka minne iliyopita. Mataifa hayo mawili yatakutana tena wka mara ya kwanza Jumanne mjini Berlin tangu Brazil walipoaibishwa kwao nyumbani wakati wa michuano hiyo ya Kombe la Dunia. "Hii ina maana kubwa sana kisaikolojia - hakuna anayehitaji kujidanganya kuhusu hilo," Titea aliambia jarida la Kicker. "Matokeo hayo ya 7-1 ni kama mizimu, watu bado huyazungumzia. Kadiri unavyoyazungumzia zaidi, ndivyo mizimu hii inavyochukua muda mrefu kutoweka

Michezo

Ureno 0-3 Uholanzi: Cristiano Ronaldo apigwa breki mjini Geneva Saa 4 zilizopita Sambaza habari hii Facebook  Sambaza habari hii Twitter  Mshirikishe mwenzako Haki EPA Mabingwa wa Ulaya Ureno walipokezwa kichapo cha kushangaza na Uholanzi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezewa mjini Geneva, Uswizi. Winga wa zamani wa Manchester United Memphis Depay na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Ryan Babel waliwaweka Waholanzi 2-0 mbele

Rais kim Jong-un Afanya ziara ya kushitukiza

Kim Jong-un amefanya ziara ya kushtukiza China? Dakika 13 zilizopita Sambaza habari hii Facebook  Sambaza habari hii Twitter  Mshirikishe mwenzako Haki AFP/GETTY IMAGES Image Babake Kim Jong-Un, Kim Jong-il, hakupenda kutumia ndege kusafiri Kuna tetesi ambazo zinaendelea kushika kasi kwamba afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Korea Kaskazini ambaye amefanya ziara ya ghafla nchini China ni kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. Vyombo vya habari Japan vilikuwa vya kwanza kuibuka na taarifa kwamba afisa wa ngazi ya juu mno kutoka Korea Kaskazinia alikuwa amewasili Beijing kwa kutumia treni maalum ya kidiplomasia. Treni hiyo ilipokelewa kwa ulinzi mkali. Korea Kusini imesema haifahamu ni nani huyo aliyefanya ziara hiyo lakini inafuatilia tukio hilo kwa makini sana.

Mambo mawili ya kuzingatia kabla hujaanza kikimo cha biashara

FAHAMU MAMBO MAWILI KABLA HUJAANZA KILIMO BIASHARA Uhakika media  /  3 weeks ago Habari za leo ndugu msomaji wangu na pole kwa shughuri mbalimbali za ujenzi wa Taifa. Jumatatu iliyopita nilikuandikia nilikuandikia makala inayokufahamisha Kilimo bora cha zao la muhogo lakini leo nimekuletea kitu cha tofauti kidogo. Unapoanzisha mradi unatarajia mwisho wa siku uumalize kwa kupata faida, sasa basi leo nataka nikufahamishe mambo makubwa mawili unayotakiwa kuyajua kabla hujaanza mradi wako wowote wa kilimo.   Jambo la kwanza: Farming master-plan Hili ni jambo la kwanza na muhimu sana kulifahamu. Farming master-plan ni muongozo wa shughuri zote unazotakiwa kuzifanya katika kilimo chako tangu kuandaa shamba mpaka kuvuna. Hii ijumuishe shughuri kama kupanda, kudhibiti magugu, uwekaji wa mbolea na kupulizia madawa ya wadudu na magonjwa. Unatakiwa kujua shughuri hizi zote, muda wa kuzifanya, namna ya kuzifanya na mahitaji yake ili uzifanye.   Kwa mfano uwekaji wa mbolea: waka

UFUGAJI BORA WA MBWA

JIFUNZE MATUNZO MAZURI KWA MBWA WA KUFUNGWA Uhakika media/   2 weeks ago Mnyama huyu huaminika ndiye mwaminifu zaidi kati ya wanyama wote wanaofugwa nyumbani Kuna wale wanaomfuga pia kwa sababu humchukulia kama 'kipenzi' chao (pet). Je, wajua mbwa ni kitega uchumi kwa baadhi ya wanaomfuga? Mnyama huyu ametajirisha baadhi ya wafugaji wanaomthamini. Mbwa hawa hufugwa na kutunzwa kwa msingi wa malengo matatu, wale wa kunusa (sneaver dogs), wa kulinda/kuhifadhi usalama (guard dogs) na wa kuongoza (guide dogs) maafisa wa usalama. Mbwa huzaa mara mbili kwa mwaka ambapo hubeba ujauzito kwa kipindi cha siku 63 (miezi 2). Kwa kawaida mbwa mmoja huzaa kati ya vilebu 8 - 12. Lishe Anachohitaji mbwa ni lishe bora pekee huku magonjwa yanayomwathiri yakiwa finyu kinyume na wanyama wengine. "Lishe ni kiungo muhimu kwa mbwa, hulishwa kwa chakula anachokula binadamu japo kuna vyakula vingine vinavyonunuliwa kwenye maduka,". Vilebu hulis

kilimo cha alizeti

WAFAHAMU WADUDU NA NDEGE WAHARIBIFU WA UKUAJI WA ALIZETI NA JINSI YA KUZUIA Uhakika media  /  2 days ago Alizeti ni mazao muhimu sana ambayo kiukweli yana faida lukuki sana pale ambapo mtu ataamua kuwekeza nguvu katika kulima.zai hili. Kwani alizeti hutumika kutengeneza mafuta ya kupikia pamoja. Pia baada ya kukamuliwa kwa mafuta, makapi yake hutumika kutengeneza chakula cha mifugo ambacho kwa neno moja huitwa (mashudu). Wanyama na wadudu wanaoathiri ukuaji wa alizeti. 1..NDEGE Alizeti hushambuliwa sana na ndege ambao huweza kuteketeza hadi asilimia 50 ya mazao shambani. Kuzuia - Usipande alizeti karibu na msitu/pori - Vuna mapema mazao yako mara baada ya kukomaa. - Panda alizeti kwa wingi katika shamba moja. - watishe  ndege kwa mutumia sanamu, makopo. Weka nyuzi zinazopatikana katika kanda za muziki, ambazo utazifunga katika miti miwili.ambayo wakati upepo unavuma hupiga kelele hivyo ndege huogopa. 2..Funza wa vitumba. Funza huyu hutoboa