Mwanasiasa wa Kenya aliyezuiliwa na kusafirishwa kilazima atua Canada Uhakika media 2 · 40 minutes ago Mwanasiasa wa upinzani aliyezuiwa kuingia Kenya wiki iliyopita na kusafirishwa kwa lazima hadi Dubai ameelekea nchini Canada, vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti. Bw Miguna Miguna, ambaye ni wakili, amesafiri kwa ndege iliyokuwa ikielekea Toronto, Canada, baada ya kukaa katika uwanja wa kimataifa wa Dubai kwa siku nne. Gazeti la Nation, limesema afisa mmoja wa serikali amewafahamisha kwamba Bw Miguna aliondoka Dubai akitumia ndege ya Air Canada 57 (ACA57) baada ya kuwasilisha pasipoti yake ya Canada. Wakili huyo alikuwa amesema hakuwa na pasipoti hiyo alipowasili uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi Jumatatu wiki iliyopita. Wakili wake Cliff Ombeta hata hivyo ameambia BBC kwamba mteja wake hakuwa na pasipoti hiyo. Aidha, amesema kwa sasa hawezi kuthibitisha iwapo Bw Miguna yumo safarini kuelekea Canada. Safari ya ndege kutoka Dubai kwenda Toronto huchukua takr
https://uhakika media.blogspot.com