Wamiliki Viwanda Mikocheni wapewa mwezi mmoja Uhakika media 5 · 2 hours ago WAMILIKI wa viwanda eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam wamepewa mwezi mmoja kutatua kero ya uchafuzi wa mazingira kwa kudhibiti utiririshaji wa majitaka unaohatarisha afya za wakazi wanaoishi kabla ya kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria. Agizo hili lilitolewa jana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola, baada ya kutembelea viwanda vya Iron and Steel Ltd na MMI Integrated Mills Ltd vilivyopo maeneo ya Mikocheni ‘B’ kujionea uchafuzi wa mazingira. Akizungumza mara baada ya ziara yake ya ghafla, Lugola alisema hakuridhishwa na namna viwanda hivyo vinavyolinda mazingira na afya ya wananchi, hivyo kutoa mwezi mmoja kurekebisha hali hiyo. “Nawaagiza wamiliki wa viwanda hivi wakutane na watendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara moja kujadili namna ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira, utirirshaji wa maji machafu, moshi n
https://uhakika media.blogspot.com