RIWAYA NA HADITHI ZA KUSISIMUA Mtuhumiwa 07 Posted by uhakika media Mara alihisi akimwagiwa petroli mwili mzima. Hah! Nachomwa moto hivi hivi sasa! Alijikurupusha na kusimama kutoka pale chini, lakini akapigwa ngwara iliyorudisha tena ardhini kwa kishindo huku akisikia lile kundi la watu likiendelea kumpigia mayowe ya jazba. Akajua kuwa sasa mwisho wake ulikuwa umedhihiri. Hakuwa tayari kulikubali hilo. Kwa nguvu zake zilizosalia alijitahidi kujiinua kutoka pale chini ili aukwepe umauti ule uliokuwa ukimkabili. Hapo ikawa kama ndio amechokoza nyuki, kwani aliangushiwa mapigo makali kutoka kila upande. Alipigwa rungu la nguvu kichwani na akahisi fahamu zikimpotea taratibu. “Lete kibiriti upesi tumuwashilie mbali kimburu huyu!” Sauti yenye jazba iliamuru. Na mara hiyo lilitokea gari na kumulika lile eneo kwa taa zake kali. Jaka alihisi kuwa aliweza kuusikia mvumo wa gari hilo ila fahamu zilikuwa zinamhama kwa kasi. Taa za gari lile ziliwamulika wale watu waliokuwa tayari wamesha
https://uhakika media.blogspot.com