Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 28, 2018

NAFASI ZA KAZI

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo Uhakika media 5  · 1 hour ago Bonyeza links zifuatazo:   2 Employment Opportunities at Under The Same Sun (UTSS)   Job Opportunity, Women’s Empowerment Project Coordinator at TATU Project   Job Opportunity at Good Neighbors - Senior Credit Program Officer   24 Job Opportunities at Zanzibar University   Job Opportunity, Community Health Specialist   2 Job Opportunities at REPOA Tanzania, Deadline 29th March   Nafasi zingine za Ajira ingia  www.ajirayako.co.tz    

Lulu Diva kumleta Cardi B bongo

Lulu Diva kumleta Cardi B bongo Uhakika media 5  · 1 hour ago Lulu Abbas ‘Lulu Diva’  MWANAMUZIKI wa kike anayefanya poa na ngoma yake ya Homa, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa kwa sasa muziki umerudi kwenye mfumo wa albamu kama zamani hivyo yupo kwenye mata-yarisho ya albamu yake mpya ambayo atawa-shirikisha wanamuziki mbalimbali akiwemo Cardi B, kutoka Marekani.  Akichonga na Risasi Vibes, Lulu Diva alisema muziki umehamia kwenye albamu na ni heshima pia kufanya kazi nzuri ambayo hata baadaye inabaki kwenye historia hivyo kumshirikisha Cardi B ni chachu ya kutangaza muziki wake kimataifa zaidi.  Cardi B.   “Najiandaa kufanya albamu kama ambavyo wanamuziki wakubwa wamekuwa wakifanya hivi karibuni na albamu yangu itakuwa imesheheni wanamuziki wakali ndani na nje ya Afrika na ndani yake nitamshirikisha Cardi B, kutoka Marekani, nafurahi sana maana naona nikitoka kimataifa zaidi kwa kweli,” alisema Lulu Diva. 

Mganda awagaragaza Diamond na Davido

Mganda awagaragaza Diamond na Davido kwenye tuzo za Nickelodeon Uhakika media 5  · 49 minutes ago Jana usiku nchini Marekani kulikuwa na ugawaji wa tuzo za kimataifa za Nickelodeon ambapo mastaa nguli kutoka Afrika walikuwa wanachuana kuwania tuzo hizo.  Mastaa hao ni Diamond Platnumz, Cassper Nyovest, Davido, Emannuella na Eddy Kenzo ambao wote walikuwa wanachuana kwenye kipengele cha Favourite African Star 2018 ambapo Eddy Kenzo ameibuka kidedea kwa kunyanyua tuzo hiyo.  Tuzo hiyo ambayo watu wengi walibashiri kuwa mtoto mwenye kipaji cha kipee barani Afrika, Emmanuella angeibuka kidedea, imezua gumzo nchini Nigeria kwa watu wengi kuhoji ushindi wa Eddy Kenzo. 

Nisha na Brown mapenzi wazi wazi

Nisha na Brown mapenzi wazi wazi Muungwana Blog 5  · 43 minutes ago Couple mpya kwa sasa mjini ambayo imeanza kuchukua headlines zake ni Muigizaji Nisha na Brown ambaye hapo awali alikuwa akitoka kimapenzi na Jacqueline Wolper.  Wawili hao wamezidi kuachia video mtandaoni wakiwa pamoja na safari hii wanaonekana wakipeana mabusu mazito wazi wazi.  Katika video hiyo aliyoweka Nisha Instagram ameandika; kitu pekee tunachohitaji ni furaha ila mara nyingi tunaangukia kwenye vilio vya kujitakia. Washauri wa mapenzi ni wengi ila unahisi unaweza kunishauri wa kuwa naye wakati tayari moyo wangu upo sehemu fulani.  Hata hivyo kuna taarifa ambazo zinadai wawili hao kuna project wanayofanya pamoja inayokwenda kwa jina la Bachela ingawa hakuna yeyote kati yao aliyethibitisha hilo hadi sasa. 

Mwakyembe awahakikishia wananchi kuwa serikali haina ugomvi na wasanii

Mwakyembe awahakikishia wananchi kuwa serikali haina ugomvi na Wasanii Uhakika media 5  · 34 minutes ago Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewahakikishia wananchi kuwa serikali haina ugomvi wowote na wasanii nchini bali wanachofanya ni kusimamia maadili katika kazi zao wanazozifanya.  Dkt. Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo (Machi 28, 2018) baada ya kupita siku kadhaa tokea Naibu Waziri wa wizara yake Juliana Shonza kutoa tamko la kuzifungia baadhi ya kazi za wasanii zilizokosa maadili katika jamii na kupelekea kuleta utata mkubwa kutoka na wengi wao kutokujua dhamira ya serikali ni ipi.  "Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo yanafanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa kiongozi wa Wizara, hivyo basi ieleweke kwamba hatua zilizochukuliwa na Naibu Waziri Shonza hivi karibuni zilikuwa za Wizara kwa mujibu wa sheria za nchi", amesema Dkt. Mwakyembe.  Pamoja na hayo, Dkt. Mwakyembe ameendelea kwa kusema "serikali hai

VAR yawakwamisha Waingereza

VAR yawakwamisha Waingereza Uhakika media 5  · 31 minutes ago Ikiwa Uingereza ndio nchi iliyokuwa kinara kwenye kudai matumizi ya teknolojia kwenye mchezo wa soka na kufanikisha kuanzishwa kwa Video assistant referee (VAR) hatimaye teknolojia hiyo imewasaidia wapinzani wao.  VAR imeisaida timu ya taifa ya Italia kusawazisha bao dhidi ya England kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la Wembley jijini London usiku wa kuamkia leo ambapo England ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.  Dakika ya 87 mwamuzi Deniz Aytekin alilazimika kusimamisha mechi na kwenda kutazama marudio ya tukio la mlinzi wa England anayechezea Burnley James Tarkowski aliyemwangusha Federico Chiesa wa italy ndani ya eneo la 18.  Baada ya kupata uhakika wa tukio kupitia picha za marudio, mwamuzi aliamuru mkwaju wa penalti ndipo mchezaji Lorenzo Insigne akapiga na kuisawazishia Italia na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.  Teknolojia hiyo inatarajiwa kutumika kuamua matukio mbalimbali yenye uta

Kocha wa standi united atoa neno kwa wapinzani

Kocha wa Stand United atoa angalizo kwa Wapinzani Uhakika media 5  · 25 minutes ago Kuelekea mchezo wa robo fainali wa Kombe la Shirikisho nchini dhidi ya Njombe Mji, kocha mkuu wa Stand United, Mrundi Niyongabo Almasi ametoa angalizo kwa wapinzani wao hao kwani wamefanya maandalizi kwaajili ya ushindi tu.  “Tumejiandaa kuhakikisha tunafanya vyema katika mchezo ili tushinde tuingie katika nusu fainali na lengo letu ni kucheza fainali kisha tupate nafasi ya kuwakilkisha nchini mwakani hivyo Njombe Mji waje wakijua tumejipanga'', amesema.  Aidha Niyongabo ameongeza kuwa hata timu nyingine kwenye michuano hiyo zijipange kwakuwa timu hiyo imejipanga kuhakikisha inafanya maajabu ya kuchukua ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza.  Stand watakuwa wenyeji wa Njombe Mji FC Machi 30, mwaka huu  kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga kwenye mchezo huo ambao utaamua nani anakwenda nusu fainali ya (ASFC).

Thiago: Brazil inahitaji kuheshimika duniani

Thiago: Brazil inahitaji heshima zaidi duniani Uhakika media 5  · 17 minutes ago Mlinzi wa timu ya taifa ya Brazil, Thiago Silva, amesema Brazil inahitaji heshima zaidi duniani na sio kubezwa kwasababu ilipoteza kwa mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani kwenye fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.  Thiago ambaye ni nahodha wa PSG ya Ufaransa ameyasema hayo baada ya kikosi chao kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya FIFA uliopigwa mjini Berlin.  "Tunaiheshimu sana Ujerumani lakini hii jezi ya Brazil inastahili heshima zaidi, tunafurahi kuwa tumeanza kuirudisha heshima ambayo dunia nzima ilikuwa imeanza kuipoteza na kuidharau timu hii yenye kila historia katika mchezo wa soka'', amesema.  Naye mashambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus ambaye ndiye mfungaji wa bao la jana usiku amesema, "Ninafurahi sio tu kwa sababu nimefunga bao, lakini pia kwa namna ambavyo hamu yangu ya kusaidia timu imetimia na nitaendelea

Thiago: Brazil inahitaji kuheshimika duniani

Thiago: Brazil inahitaji heshima zaidi duniani Uhakika media 5  · 17 minutes ago Mlinzi wa timu ya taifa ya Brazil, Thiago Silva, amesema Brazil inahitaji heshima zaidi duniani na sio kubezwa kwasababu ilipoteza kwa mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani kwenye fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.  Thiago ambaye ni nahodha wa PSG ya Ufaransa ameyasema hayo baada ya kikosi chao kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya FIFA uliopigwa mjini Berlin.  "Tunaiheshimu sana Ujerumani lakini hii jezi ya Brazil inastahili heshima zaidi, tunafurahi kuwa tumeanza kuirudisha heshima ambayo dunia nzima ilikuwa imeanza kuipoteza na kuidharau timu hii yenye kila historia katika mchezo wa soka'', amesema.  Naye mashambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus ambaye ndiye mfungaji wa bao la jana usiku amesema, "Ninafurahi sio tu kwa sababu nimefunga bao, lakini pia kwa namna ambavyo hamu yangu ya kusaidia timu imetimia na nitaendelea

Mahakama yaamuru mmiliki wa IPTL akatibiwe muhimbili

Mahakama Yaamuru mmiliki wa IPTL Akatibiwe Muhimbili Uhakika media 5  · 11 minutes ago Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa IPTL, Harbinder  Sethi akatibiwe katika Hospital ya Taifa Muhimbili baada ya mshtakiwa huyo kulalamika afya yake imearibika sana.  Mbali ya Sethi, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Bilioni 309.  Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo March 28, 2018 kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na pia wanafatilia vielelezo vya upelelezi nje ya nchi.  Baada ya kueleza hayo, Seth alisimama na kumueleza Hakimu Shaidi kuwa; 'Afya yangu imearibika sana, nahitaji kupelekwa hospitali.'  Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi amesema ni dhahiri afya ya mshtakiwa ikiangaliwa hata kwa macho inaonekana ni dhahifu.  “Naamuru mshtakiwa akatib

Mchungaji adakwa akijaribu kumfufua marehemu

Mchungaji adakwa na Polisi akijaribu kumfufua Marehemu Uhakika media 5  · 7 minutes ago Mchungaji mmoja  nchini  Msumbiji amejikuta akiishia  mikononi mwa polisi baada ya kujaribu kumfufua mwanamume mmoja eneo la kati la Msumbiji bila mafanikio.  Mchungaji huyo alidai kuwa roho mtakatifu alimwambia asafiri hadi katika hospitali inayofahamika kwa jina Chimoio iliyopo katika jimbo la Manica, ili akafanye muujiza ambao alidai ana uwezo wa kufanya na alipowashawishi Maafisa wa hospitali walimruhusu aingie ndani ya chumba cha kuhifadhi maiti ili atekeleze muujiza huo.  Hata hivyo baada ya siku mbili za maombi, hakuweza kurejesha uhai wa marehemu na familia hiyo haikushangazwa na kushindwa kwake. Dada wa marehemu  ambaye hakutaka jina lake litajwe aliwaambia waandishi wa habari kuwa “Kasisi aliomba, akaomba na kuomba hadi akanena kwa lugha. Alizungusha kichwa cha marehemu huku na kule huku akiomba.  “Lakini hakuna hata sehemu ya marehemu kaka yangu iliyoweza kutikisika. Wakati mmoja k

Tetesi za soka Ulaya leo 28/3/208

Tetesi za soka ulaya Uhakika media Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 28.03.2018: Gabriel Jesus amekataa mshahara mpya, City wanamtaka Isco Saa 4 zilizopita Sambaza habari hii Facebook  Sambaza habari hii Twitter  Mshirikishe mwenzako Image Gabriel Jesus amewaambia maafisa wa Ligi ya Primia na wale wa Brazil mkataba mpya ni mpaka msimu wa majira ya joto Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus, mwenye umri wa miaka 20, amekataa malipo ya £90,000- kutoka kwa viongozi wa Ligi ya Primia na wale wa Brazil na hivyo watalazimika kusubiri hadi msimu wa majira ya joto kujadili mkataba mpya . (Mail) Manchester City wanammezea mate mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Uhispania ya Real Madrid Isco, mwenye umri wa miaka 25 ambaye wanataka kumnunua £75m msimu wa majira ya joto . (Sun)

Timbulo afunguka kutohofia kufungiwa muziki

Timbulo afunguka kutohofia kufungiwa Muzuki Uhakika media 5  · 2 hours ago Ally Timbulo   LICHA ya baadhi ya wanamuziki kufungiwa nyimbo zao na serikali kutokana na kuwa kinyume na maadili, msanii wa Bongo Fleva, Ally Timbulo ameeleza kwamba hana hofu na hilo kwani muziki wake ni wa Kiafrika zaidi. Akistorisha na Risasi Vibes, Timbulo alisema muziki wake una asili ya Kiafrika na siyo asili ya Ulaya kama wanamuziki wengi wanavyofanya ambao wanaacha maungo nyeti wazi au kucheza kihasara hivyo hana hofu kabisa kwamba serikali itamfungia.  “Sina muziki wenye asili ya Ulaya, muziki wangu ni wa Kiafrika, kwa hiyo sina shaka na kufungiwa maana hata video zangu nafanya zenye maadili yanayotakiwa ambapo zinaangaliwa na wakubwa kwa wadogo,” alisema Timbulo.  Hata hivyo aliwataka wasanii wenzake kufuata utaratibu kwani kila mahali kuna utaratibu na sheria zake hivyo inawapasa kuzingatia hilo ili kuweza kusonga mbele zaidi. 

Dullah Makabila amuweka katika hali tete Tiko

Dullah Makabila amuweka katika hali tete Tiko Uhakika media 5  · 2 hours ago Msanii wa muziki wa Singeli, Dullah Makabila   BAADA ya habari na picha za msanii wa muziki wa Singeli, Dullah Makabila na msanii wa filamu Bongo, Tiko Hassan kuzagaa wakiwa kimahaba, habari mpya ni kwamba ishu hiyo imemsababishia mwanadada huyo tafrani ya aina yake.  Rafiki wa karibu na Tiko aliieleza Za Motomoto News kuwa, mrembo huyo, baada ya picha na habari kuvuja kwamba anatoka kimapenzi na Dullah Makabila, hali ilikuwa tete kwani mpenzi wake anayemweka mjini alimjia juu na penzi lao kuwa shakani.  Tiko Hassan   “Kiukweli Tiko ameumizwa sana na Makabila ambaye alivujisha picha kwani ana mpenzi wake ambaye ndiye anayemweka mjini hivyo baada ya kuona habari hizo kuliibuka gogoro zito na kushindwa kuelewana kabisa yaani mpaka sasa Tiko anaendelea kuomba msamaha kwa bwana’ke maana huyo Dullah anasema ni rafiki yake wa kawaida tu,” alisema mtoa habari huyo.  Alipoulizwa Tiko kuhusiana na hilo alisema

Linex afunguka haya

Linex azungumzia ishu ya kupotezwa na Ulevi Uhakika media 5  · 2 hours ago Sunday Mangu ‘Linex’   MSANII wa Bongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’, ameibuka na kufungukia tetesi zinazozagaa dhidi yake kuwa ulevi ndiyo umempoteza kimuziki na kusema siyo kweli bali wanaozungumza hivyo ni wabaya wake ambao hawana nia nzuri kwake.  Akipiga stori na Risasi Vibes, Linex alisema kuwa muziki ni kama biashara nyingine na mtu anaweza kushuka na kupanda hivyo kilichompoteza ni changamoto za maisha kuwa nyingi na kushindwa kuzimudu ila anaamini atarejea tena na kuwa kama alivyokuwa zamani.  “Wanaosema kwamba nimepotea kimuziki kisa ulevi hawana nia njema na mimi, mwanamuziki yeyote anaweza kupotea bila kujali umaarufu alionao, ndiyo maana hata Bill Gates leo anaweza kuwa namba moja kwenye listi ya matajiri duniani na baada ya muda hata kwenye kumi bora akawa hayumo tena,” alisema Linex. 

BANCABC yatangaza kupunguza riba za mikopo

BANCABC yatangaza kupunguza riba za mikopo Uhakika media 5  · 1 hour ago BANCABC ambayo ni sehemu ya Atlas Mara iliyosajiliwa katika soko la Hisa London imepiga hatua kwa mara nyingine katika soko nchini kwa kutangaza punguzo katika tozo za mikopo ili kutoa uhueni kwa wateja wake wakati wa ulipaji wa mikopo na kuwawezesha wateja wapya kukopa kuanzia Aprili Mosi Mwaka huu. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC, Dana Botha alisema watapunguza riba kwenye mikopo ya masharti, huduma ya ‘over draft’ na mikopo ya nyumba kwa wateja wao. “Mwaka jana benki nyingi zilipita katika wakati mgumu wa ukwasi,hivyo kufanya uwezo wa kukopesha kuwa mdogo.Kwa miezi kadhaa sasa serikali kupitia benki kuu ya Tanzania-BOT imekuwa ikisisitiza kuhusu punguzo la riba hili kwa kusaidia kupunguza masharti kama vile kiwango cha chini cha fedha kwa mabenki,viwango vya punguzo hati fungani za hazina na kukopesha mabenki kwa viwango vya chini. “Hili limewezesha ukopeshaji

Shamsa:huwa naishi maisha ninayo weza siku zote

Shamsa: Huwa naishi maisha ninayoyaweza siku zote, sitamani vya watu Uhakika media 5  · 1 hour ago Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kudai hata adharauliwe kwa kiasi gani hawezi kuthubutu kutamani au kujilinganisha maisha yake na mtu mwingine kwa kuwa anaimani kila mmoja Mungu amempangia fungu lake.  Shamsa ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii ikiwa kama somo au fundisho kwa baadhi ya watu wenye tabia ya kupenda kutamani na kujilinganisha maisha na watu fulani waliowazidi uwezo na matokeo yake huwa wanaishia kuaibika kutokana na wanachokifanya hakipo katika uwezo wao.  "Huwa naishi maisha ninayoyaweza siku zote, sitamani vya watu wala kulinganisha maisha yangu na mtu yeyote kwasababu huwa naamini Mwenyezi Mungu amempa kila mtu kwa wakati wake na kila mtu ana kalma yake", amesema Shamsa.  Pamoja na hayo, Shamsa Ford ameendelea kwa kusema "hata unidharau mpaka kunitemea mate kwa kuhisi una vikubwa kuliko nilivyo navyo mimi, huwa siumii k

Mama Samia asema kufanya upandikizaji wa figo ni hatua kubwa sana katika maendeleo ya nchi

Mama Samia asema kufanya upandikizaji figo ni hatua kubwa katika maendeleo ya nchi. Uhakika media 5  · 1 hour ago MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kitendo cha Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), kufanya upandikizaji figo ni hatua kubwa katika maendeleo ya nchi.  Akizungumza jana mjini hapa, Mama Samia alisema serikali inajivunia hatua hiyo na kwamba inafuatilia kwa karibu afya ya mgonjwa aliyepandikizwa figo wiki iliyopita.  Alibainisha kuwa gharama za upandikizaji figo katika hospitali hiyo, ambazo ni Sh. milioni 22 zinaweza kukusanywa katika ngazi za familia na kuokoa maisha ya mgonjwa.  Alipongeza hatua hiyo na kusema itakomboa wananchi wasiokuwa na uwezo, ambao wanaugua ugonjwa huo na kushindwa kwenda India kupata matibabu.  “Tunajivunia hatua hii na serikali inafuatilia kwa karibu afya ya mgonjwa aliyepandikizwa figo," alisema makamu wa rais. "Gharama katika Hospitali ya Benjamini Mkapa sio kubwa sana, ndugu wanaweza kujich

Wafanyakazi wa ngorongoro na mashitaka ya mamilioni

Wafanyakazi Ngorongoro na mashitaka ya mamilioniuha  5  · uhakika media 5 . 1hour ago WAFANYAKAZI watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) jana walifikishwa mahakamani kwa kosa la kuisababishia hasara serikali ya dola za Kimarekani 35,500 (sawa na Sh. milioni 79).  Watuhumiwa waliofikishwa kizimbani na kusomewa mashtaka ni Joseph Mtwala (36), John Mlambo (42), Mwahu Yunus (38), Mery Njau (38) na Catherine Edward (33).  Watuhumiwa kwa pamoja walisomewa shtaka moja na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), Adamu Kilongozi akisaidiwa na Hamidu Simbano na Richard Jacopiyo alidai kuwa walitenda kosa hilo kati ya Desemba 25, mwaka 2013 na Juni 6, mwaka 2014.  Kilongozi alidai kuwa watuhumiwa hao wakiwa katika lango la Nabi mkoani Mara na lango kuu la Loduare mkoani Arusha walisababishia serikali kiasi hicho cha hasara wakiwa watumishi wa NCAA.  Mwendesha mashtaka huyo alisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru mk

JK kuwa mgeni rasmi katika harambee

'JK' kuwa mgeni rasmi katika harambee Uhakika media 5  · 1 hour ago RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee ya kukusanya fedha kiasi cha Sh. bilioni moja, kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Sekondari Lindi iliyoungua Julai 2016.  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema harambee hiyo itafanyika kesho jijini Dar es Salaam.  Zambi alisema maandalizi yote kwa ajili ya harambee hiyo yamekamilika na inatarajia kuhudhuriwa na wadau wa sekta ya elimu nchini.  Alisema harambee hiyo imepanga kukusanya Sh. bilioni moja ikiwa ni karibu nusu ya mahitaji ya Sh. bilioni mbili zinazotakiwa kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo kongwe.  “Kutokana na fedha tutakazokusanya, tumepanga ujenzi uanze wakati wowote. Zoezi hili litakwenda sambamba na mpango wa mkoa kuboresha mfumo mzima wa masuala ya elimu toka ngazi ya awali,” alisema Zambi.  Mkuu wa mkoa huyo alikiri kuwa mkoa wake ni mmoja kati