Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 1, 2018

Pope Francis baptises Italy's migrant' hero' at Easter service

Uhakika media Video Pope Francis baptises Italy's 'migrant hero' at Easter service A Nigerian man dubbed Italy's "migrant hero" has been baptised by Pope Francis during an Easter service at St. Peter's Basilica. John Ogah, 31, was begging outside a supermarket in Rome last year when a masked thief armed with a cleaver tried to rob it. He held the man down until police arrived - and was ultimately rewarded with a residency permit. As the Pope baptised him, an Italian police captain stood by his side as his godfather. 01 Apr 2018

Mali Jihadist faces war crimescharges at International Criminal Court

Mali jihadist faces war crimes charges at International Criminal Court Uhakika media 1 April 2018 Share Image REUTERS Image Tombs at the Djingareyber mosque in Timbuktu were smashed by Islamist militants in 2012 The International Criminal Court in the Hague has taken into custody a man wanted for war crimes in Mali, after the authorities there handed him over. Al Hassan Ag Abdoul Aziz Ag Mohamed Ag Mahmoud headed the Islamic police in Timbuktu when it was under the control of jihadist militants five years ago. He is accused of victimising women and girls by approving their forced marriages to Islamist fighters. He is also alleged to have helped destroy ancient mausoleums in Timbuktu. The arrest warrant for Mr Al Hassan listed crimes against humanity including "torture, rape and sexual slavery; persecution of the inhabitants of Timbuktu on religious and gender grounds; and other inhumane acts". The only other man tried by the ICC over Mali

Joh Makini afunguka haya

Joh Makini afunguka hawezi kupangiwa aina ya mashairi ya kuimba Uhakika media 5  · 30 minutes ago Rapa kutoka Weusi anayetamba kwa sasa na 'hit song' ya 'Mipaka', Joh Makini amefunguka na kudai hawezi kupangiwa aina ya mashairi ya kuimba katika muziki wake kwa kuwa hicho ndio kitu pekee kinachoweza kumtofautisha yeye na wasanii wengine nchini.  Joh Makini ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kupita upepo wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kufungia baadhi ya kazi za wasanii zilizokuwa hazina maadili huku wengine wakitakiwa kubadilisha baadhi ya mashairi yaliyokuwepo katika nyimbo zao ili mradi zilete maana nzuri katika jamii ya kitanzania ambao ndio wasikilizaji wao.  "Tunavyoandika mashairi wakati mwingine unakuwa tofauti na watu wanavyopokea kitaani kwa hiyo ikawa sisi tunatoa nyimbo yeye maana fulani halafu wao BASATA wakasikiliza huo wimbo wakasema wanaufungia huo wimbo kwasababu unamaana mbaya wakati wewe hukumaanisha hivyo",

Miguna Amlaumu Odinga

Miguna amlaumu Odinga Uhakika media 5  · 27 minutes ago Mwanasheria Miguna Miguna ambaye hivi karibuni amekuwa akipitia mambo mbali mbali kuhusu uraia wake na kulazimika kuondolewa nchini Kenya, amemlaumu kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga kwa yote anayoyapitia.  Kwenye ujumbe alioutuma kutoka nchini Dubai ambako bado yupo, Miguna amesema Odinga hakupaswa  kula bata na watu waliompokonya urais wake, na yeye alkiyemuapisha kuendelea kupata misuko suko huku akiachwa bila msaada.  "Raila Odinga hawezi na hakupaswa kufurahia Pasaka na kula pamoja na waliomdhulumu, huku mtu aliyemuapisha kuwa Rais wa watu 'akiuawa' na watu hao ambao wamemuibia uchaguzi, kuua na kupoteza wafuasi wake", ameandika Miguna kwenye ujumbe huo alioutuma.  Sambamba na hayo, Miguna ametoa ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter akimsema Gavana Joho wa Mombasa ambaye naye alikuwa mstari wa mbele wakati wa harakati za kuapishwa kwa Odinga, hajawahi kumpigia simu wala kumjulia hali, hat

Tiangong-1: Chombo cha anga cha China kuanguka duniani kesho jumatatu

Tiangong-1: Chombo cha anga cha China kuanguka duniani kesho Jumatatu Uhakika media 5  · 20 minutes ago Kifusi kutoka kwa kituo cha maabara cha safari za anga cha China, kinaweza kupasuka na kuanguka duniani Ijumaa,wanasayansi wanaokifanyia uchunguzi wanasema.  Kituo hicho cha Tiangong-1 ni sehemu ya mpango wa safari za anga za mbali wa Uchina, na wa sampuli ya kituo cha safari za anga za mbali cha binadamu wa mwaka 2022.  Kiliwekwa kwenye uzio mwaka 2011 na miaka mitano baadae kikamilisha shughuli yake, na baadae kilitarajiwa kuanguka duniani.  Muda na mahala kitakapoangukia ni vigumu kutabiri kwasababu sasa hakidhibitiwi, Makadirio ya hivi karibuni ya kurejea kwa chombo hicho ni tarehe 2 Aprili.  Sehemu kubwa ya kituo hicho kina uwezekano mkubwa wa kuungua hewani, lakini kifusi kinaweza kunusurika na hivyo kuanguka kwenye uso wa dunia.  Mwaka 2016 China ilipoteza mawasiliano na chombo cha Tiangong-1 na haikuweza tena kudhibiti mienendo yake , kwa hiyo haijulikani kabisa kitais

Marekani na Korea kusini yaanza mazoezi ya kivita

Marekani na Korea Kusini yaanza Mazoezi ya kijeshi Uhakika media5  · 16 minutes ago Marekani na Korea Kusini kwa pamoja yameanza mazoezi yao ya kijeshi ya kila mwaka, baada ya zoezi hilo kucheleweshwa kwa karibu mwezi mzima.  Mazoezi hayo yalisitishwa ili kutoa fursa kulegezwa kwa masharti ya mazungumzo kati ya Korea zote mbili, wakati wa mashindano yaliyomalizika ya Olimpiki majira ya baridi.  Katika siku za nyuma, Korea Kaskazini, ilielezea mazoezi hayo ya kijeshi, kama maandalizi ya kuivamia.  Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa, mara hii Pyongyang, imekimya kuhusiana na mazoezi hayo.  Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, anasemekana kuwaambia maafisa wakuu wa nchi jirani ya Korea Kusini, ambao walizuru taifa lake kuwa, anaelewa kuwa hali inafaa kusonga mbele.  Mwisho wa mwezi huu, mkutano mkuu umeandaliwa kati ya mataifa hayo mawili, ambayo zamani yalikuwa mahasimu, na utakuwa mkutano wa kwanza kabisa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Dalali afunguka kuhusu Simba kutwaa ubingwa msimu huu

Dalali afunguka Simba kutwaa ubingwa msimu huu Uhakika media 5  · 1 hour ago Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali, anaimani timu yake itatwaa ubingwa wa ligi msimu huu baada ya kuukosa kwa muda wa takribani miaka mitano.  Dalali ambaye aliwahi kufanya vizuri wakati akiwa Mwenyekiti wa Simba, amesema kikosi walichonacho hivi sasa kina morali ya juu na si kama kadhaa nyuma.  "Simba hii iko vizuri, hauwezi ukailinganisha na timu zingine katika ligi, uwezekano wa kubeba kombe upo kwa asilimia 100" alisema Dalali wakati akizungumza na kipindi cha Michezo, kupitia Radio One jana.  Aidha Dalali ametamba kwa kusema Simba ni lazima ishinde mchezo wa Jumanne dhidi ya Njombe Mji ili kuendelea kujitengenezea mazingira ya kuwa kileleni. Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.  Dalali ameeleza mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuwa na uhitaji wa alama tatu, hivyo watambana ili kupata matokeo.

Mpiga picha wa Diamond ajibu kuhusu kufukuzwa WCB

Mpiga picha wa Diamond ajibu kuhusu kufukuzwa WCB Uhakika media 5  · 1 hour ago Baada ya Mpiga Picha wa Diamond Platnumz ‘Kifesi’ kutangaza kuacha kazi hiyo, kumeibuka stori kuwa Kifesi amefukuzwa kazi kitu ambacho amekikanusha vikali.  Kifesi amesema taarifa zinazodai kuwa amefukuzwa kazi hazina ukweli wowote na kilichotokea ni maamuzi yake binafsi.  “Hapana sijawahi kuachishwa kazi, kama niliachishwa basi niliachishwa pasipo kupewa taarifa, ninachofahamu nimechukua maamuzi haya na ni kitu ambacho nilikuwa nimepanga kufanya kutoka siku nyingi, so jana nikasema i think it right time to do this,” Amesema Kifesi  Pia amejibu kuhusu kuingilia masuala ya Diamond na Zari ndiko kumepelekea hayo, Kifesi amejibu; “Kumtetea zari sijaanza leo, ukiangalia Instagram kuna posti za zamani nilikuwa nafanya hivyo lakini ni suala gumu kulielezea”.  Dada wa Diamond, Ema Platnumz baada ya kusikia taarifa za Kifesi kuacha kazi, kwenye moja ya post Instagram ali-comment; “Acha uongo Kifesi umefuku

Hii ndio barua ya prof: Kitila Mkumbo kwenda kwa mkuu wa kanisa la KKKT

Hii ndio Barua ya Profesa Kitila Mkumbo Kwenda kwa Mkuu wa Kanisa la KKKT Uhakika media 5  · 1 hour ago Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) S. L. P. 3033 ARUSHA. Mheshimiwa Baba Askofu, Shalom!  YAH: MAMBO MATANO AMBAYO HAYAPONYI KATIKA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT   Jina langu ni Kitila Mkumbo, muumini katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambalo wewe ndiye mkuu wake. Kikazi, mimi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Dodoma. Kitaaluma, mimi ni mhadhiri mwandamizi katika Saikolojia na Elimu nikiwa na cheo cha Profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.  Mheshimiwa Baba Askofu, kwa unyenyekevu mkubwa nimeamua kukuandika barua hii ili kutoa maoni yangu binafsi kwa kanisa unaloliongoza kupitia kwako kuhusu maudhui ya waraka uliotolewa na waheshimiwa maaskofu wa KKKT siku ya Jumamosi tarehe 24 Machi 2018. Waraka huo ulitarajiwa kusomwa katika makanisa siku ya Jumapili tarehe 25 Machi 20

Idadi ya watoto walio zaliwa leo yatolewa Muhimbili

Idadi ya Watoto waliozaliwa leo yatolewa Muhimbili Uhakika media 5  · 1 hour ago Jumla ya watoto 7 wamezaliwa siku ya leo Aprili Mosi, 2018, ambayo ni sikukuu ya pasaka, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.  Taarifa hiyo imetolewa na ofisi ya mahusiano ya hospitali ya Muhimbili, ambapo imeeleza kwamba watoto hao waliozaliwa wanne ni kike, huku wakiume wakiwa watatu, na wazazi sita wakiwa wamejifungua kawaida na mmoja kwa upasuaji.  Mama na watoto hao wote wapo salama na wanaendelea vizuri hospitalini hapo.

Rais Magufuli awatakia watanzania wote kheri ya pasaka

Rais Magufuli awatakia Watanzania wote heri ya Pasaka Uhakika media 5  · 1 hour ago Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Aprili 01, 2018 ameungana na wakristo wote katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.  Akizungumza baada ya kukaribishwa na Padre Tegete kutoa salamu, Rais Magufuli amewatakia watanzania wote heri ya Pasaka na ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuishi kwa amani na upendo huku wakishiriki ipasavyo katika ujenzi wa Taifa.  "Kifo na ufufuko wa bwana wetu Yesu Kristo ukafufue matendo yetu, tuendelee kuijenga amani yetu, upendo wetu na tujenge maendeleo ya watanzania wote, kwani Kristo alifundisha upendo miongoni mwetu. Kwa hiyo Baba nakushukuru sana kwa kuongoza Misa hii, naomba ufikishe shukrani zangu kwa Kardinali Pengo, Maaskofu wote na watanzania wote tuendelee kusimama pamoja ili kulijenga Taifa letu", amesema  Rais Magufuli.