Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 10, 2018

VIDEO: Mbwembwe za Joti aingia uwanjani kisa Samatta nusra akamatwe na polisi' refa amtoa

VIDEO: Mbwembe za Joti aingia uwanjani kisa Samatta nusra abebwe na polisi, refa amtoa Uhakika media 1  · 12 hours ago Joti ambae ni msemaji wa team Samatta leo ameonyesha vituko vya aina yake ambapo imepelekea baadhi ya mashabiki kuachwa midomo wazi kwa kitendo cha kuingia uwanjani wakati mpira uneendelea baada ya Mbwana Samatta kufanyiwa madhambia kwenye eneo la hatari  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

VIDEO: Highlight TEAM KIBA Vs SAMATTA Ali Kiba akosa penati

VIDEO: Highlight Mechi TEAM KIBA Vs SAMATTA, Ali Kiba akosa penati Uhakika media 1  · 10 hours ago Baadhi ya matukio yaliyojitokeza kweny mchezo wa leo kati ya Team Samatta Vs Kiba ni pamoja na mchekeshaji Joti kuonesha mbwembwe mbalimbali na kuwa kivutio kikubwa huku Ali Kiba akikosa panati katika mchezo huo kujua zaidi  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI ........USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Yafahamu matatizo ya ngozi yatokanayo na kunyoa ndevu na nywele na jinsi ya kujitibu

Yafahamu matatizo ya ngozi yanayotokana na kunyoa ndevu na nywele na jinsi ya kujitibu Uhakika media·  9 hours ago Wakati unaponyoa ndevu na nywele, baada ya kunyoa, wakati wa kuota nywele hizo zipo baadhi ya sehemu nywele hushindwa kutoka nje ya ngozi na kuota ndani ya ngozi hali inayopelekea kusababisha uvimbe na vipele.   Zipo aina mbili za mapele yanayotokana na Kunyoa nywele na ndevu.   Magonjwa haya ni kama ifatavyo   1. Acne Keloidalis Nuchae   Acne keloidalis nuchae (AKN) Ni tatizo linalotakana na maambukizi ya bacteria P.Acnes kwenye ngozi baada ya kunyoa,hali inayopeleka vijitundu vya vinyweleo kuziba na kufanya nywele kushindwa kutoka nje ya ngozi na kukulia ndani ya ngozi hivo kusababisha mapele makubwa na makovu. Acne keloidalis nuchae (AKN) mara nyingi hutokea sehemu ya kisogo.   Mbali na kunyoa tatizo hili pia huweza kusababishwa na uvaaji wa kofia.   2.Pseudofolliculitis barbae (PFB)   Tatizo hili huwapata watu wengi, hili hutokea sehemu za kidevu na mashavu. Hi

Ugonjwa wa chango la uzazi (mke/mume)

Ugonjwa Wa Chango La Uzazi - (Mke / Mume) Uhakika media 9 hours ago Tunapozungumzia mgonjwa wa chango tuna maana kuwa ni matatizo yaliyopo katika viungo vya uzazi kwa mke au mume. Huu ni ugonjwa ambao humpata mtu katika umri mdogo utotoni. Kwa mfano :- mume, hupata maumivu ya tumbo mara kueneza anapokuwa mdogo. Kwa upande wa mwanamke hupata maumivu ya tumbo anapoanza kuvunja ungo. Maumivu hayo hupelekea mtu (mume/mwanamke) kupata madhara katika viungo vyake vya uzazi.   DALILI ZAKE   Kwa mwanaume atakuwa akishiriki tendo la ndoa, anawahi sana kufika kileleni na kurudia mara nyingine ni vigumu sana. Pia mwanaume hatakuwa na uwezo wa kusimamisha. Ni vigumu kumpa mimba mwanamke. Mwanamke mwenye chango la uzazi ana dalili zifuatazo:-   Kupata maumivu makali wakati anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa Siku zake za hedhi hazitakuwa na ratiba, zitakuwa zinabadilika badilika Hujisikia homa kali anapokaribia s

Media zinaua muziki wa bongo: TID

"Media zinaua mziki wa bongo" TID Uhakika media · 16 hours ago Msanii wa kizazi kipya nchini Khalid Mohamed maarufu TID amefunguka na kusema kuwa utaratibu wa media kushusha wasanii pale wanapodai maslai yao na kuwapandisha wengine ndio kitu kinaathiri muziki wa Bongo Flava TID  ametoa kauli hiyo wakati akiongea na Wasafi TV  Muimbaji huyo ameeleza kuwa kitu hicho ndicho kilitokea kwenye muziki wake na kwa sasa kimemtokea Diamond.  “Na kweli anaweza because he has a media, yaani yeye ndio kama Mungu anajiona but mimi hapana. Nilifanya kosa hilo lakini kosa hilo ndilo limewasanua wasanii wengine, unaona msanii kama Diamond naye amekataa,” amesema na  kuongeza; “So Diamond was me lakini wakasema wewe siunajifanya mjanja sasa tunamleta Diamond tukushushe wewe. At the end Diamond naye wanataka kumuua, sijui wanataka kumuweka nani,”  TID amesema kuwa hajaona kitu kama hicho nchini Kenya kwani bado anamuona Jaguar ni msanii mkubwa, Nonini ni msanii mkubwa anapewa heshima yak

Magazeti ya leo 10/6/2018

MAGAZETI YA LEO 10/6/2018 Uhakika media  · 1 hour ago

Polisi, TRA wakamata kiwanda bubu kilimanjaro

Polisi, TRA wakamata kiwanda bubu Uhakika media 1  · 8 hours ago Polisi Mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani humo, wamekamata kiwanda bubu kinachotengeneza vinywaji vikali ambavyo vimepigwa marufuku hapa nchini.  Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Bwana HAMISI ISSA amethibitisha kukamatwa kwa vifaa mbalimbali vya kutengenezea pombe hizo katika nyumba  moja ya kuishi maeneo ya Msaranga Manispaa ya Moshi.  Amesema vifaa mbalimbali vya kutengeneza pombe hizo vimekamatwa zikiwemo chupa 1,600 na stika 800 zenye nembo feki za Mamlaka ya Mapato nchini pamoja na watu wawili waliokuwa wanatengeneza pombe hizo.  Naye Afisa Mwandamizi wa Kodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Kilimanjaro, Bwana TILSONI KABUJE amesema bidha hizo hazina ubora kutokana na kutengenezwa katika mazingura ambayo siyo salama pamoja na kuziingiza sokoni bila kulipa kodi.