Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mbinu

Faida ya unacho kitafuta/ lengo katika maisha

Faida za kujua unachokitaka (lengo lako) katika maisha Uhakika media  · 5 hours ago Kimsingi kila  mwanadamu anapenda kuwa na maisha mazuri siku zote,  hakuna hata mmoja ambaye anapenda kuiishi katika maisha ambayo  sio mazuri hata siku moja. Baadhi wa watu hasa ambao hawajafanikiwa  ukiwauliza kile ambacho wanakihitaji, wengi wao hutoa majibu ya ujumla kwamba nataka kuwa mfanyabiashara, nataka kusoma , nataka kujenga nyumba na vitu vingine vingi ambavyo mwanadamu huyu anataka kuwa  au kuvifanya kwa hapo baadae.  Lakini ukweli ni kwamba kusema hayo huwa tunakosea kwa sababu huwa tunayoongelea kwa mapana sana, hapa namaanisha ya kwamba lengo lako la kesho lazima liwe maalaumu na liwe limeandaliwa na siku yako ya leo. Kwa mfano usiseme unataka kuwa mbanyabishara na kuishia hapo tu, bali ni lazima uainishe ni aina gani ya biahara unayotaka kuja kuifanya na utie nia ya kweli juu ya biashara hiyo. Kwa mfano unaweza kupanga malengo yako ya hapo baa...