Waziri - Huduma usafishaji figo ni bure Uhakika media 1 · 1 hour ago WAZIRI wa Afya Hamad Rashid Mohammed amesema huduma za kitengo cha usafishaji figo kwa wagonjwa wenye matatizo hayo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja zinaendelea kufanyika bila ya malipo yeyote . Hayo aliyasema huko katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wakati alipokuwa akifanya ziara ya kukagua kitengo hicho na kuona jinsi kinavyoendelea na huduma zake zinazofanyika katika sehemu hiyo kwa kuhudumia wagonjwa kama kawaida. Alisema lengo la ziara hiyo ni kuona jinsi wananchi wanavyofaidika na huduma hiyo kwani Serikali inataka wananchi wake wasihangaike kutafuta huduma hiyo kwa kuifuata nje ya nchi au masafa marefu. Aidha alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuwajali wananchi wake imekuwa iko imara katika kuhakikisha inakipa kipaumbele kwa kukipatia vifaa vyote pamoja na dawa za kusafishia mafigo. “Wananchi mnapofikwa na matatizo haraka fikeni Hospitalini ili muweze kupata huduma dawa zipo za kut
https://uhakika media.blogspot.com