Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2018

VIDEO: Mbwembwe za Joti aingia uwanjani kisa Samatta nusra akamatwe na polisi' refa amtoa

VIDEO: Mbwembe za Joti aingia uwanjani kisa Samatta nusra abebwe na polisi, refa amtoa Uhakika media 1  · 12 hours ago Joti ambae ni msemaji wa team Samatta leo ameonyesha vituko vya aina yake ambapo imepelekea baadhi ya mashabiki kuachwa midomo wazi kwa kitendo cha kuingia uwanjani wakati mpira uneendelea baada ya Mbwana Samatta kufanyiwa madhambia kwenye eneo la hatari  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

VIDEO: Highlight TEAM KIBA Vs SAMATTA Ali Kiba akosa penati

VIDEO: Highlight Mechi TEAM KIBA Vs SAMATTA, Ali Kiba akosa penati Uhakika media 1  · 10 hours ago Baadhi ya matukio yaliyojitokeza kweny mchezo wa leo kati ya Team Samatta Vs Kiba ni pamoja na mchekeshaji Joti kuonesha mbwembwe mbalimbali na kuwa kivutio kikubwa huku Ali Kiba akikosa panati katika mchezo huo kujua zaidi  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI ........USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Yafahamu matatizo ya ngozi yatokanayo na kunyoa ndevu na nywele na jinsi ya kujitibu

Yafahamu matatizo ya ngozi yanayotokana na kunyoa ndevu na nywele na jinsi ya kujitibu Uhakika media·  9 hours ago Wakati unaponyoa ndevu na nywele, baada ya kunyoa, wakati wa kuota nywele hizo zipo baadhi ya sehemu nywele hushindwa kutoka nje ya ngozi na kuota ndani ya ngozi hali inayopelekea kusababisha uvimbe na vipele.   Zipo aina mbili za mapele yanayotokana na Kunyoa nywele na ndevu.   Magonjwa haya ni kama ifatavyo   1. Acne Keloidalis Nuchae   Acne keloidalis nuchae (AKN) Ni tatizo linalotakana na maambukizi ya bacteria P.Acnes kwenye ngozi baada ya kunyoa,hali inayopeleka vijitundu vya vinyweleo kuziba na kufanya nywele kushindwa kutoka nje ya ngozi na kukulia ndani ya ngozi hivo kusababisha mapele makubwa na makovu. Acne keloidalis nuchae (AKN) mara nyingi hutokea sehemu ya kisogo.   Mbali na kunyoa tatizo hili pia huweza kusababishwa na uvaaji wa kofia.   2.Pseudofolliculitis barbae (PFB)   Tatizo hili huwapata watu wengi, hili hutokea sehemu za kidevu na mashavu. Hi

Ugonjwa wa chango la uzazi (mke/mume)

Ugonjwa Wa Chango La Uzazi - (Mke / Mume) Uhakika media 9 hours ago Tunapozungumzia mgonjwa wa chango tuna maana kuwa ni matatizo yaliyopo katika viungo vya uzazi kwa mke au mume. Huu ni ugonjwa ambao humpata mtu katika umri mdogo utotoni. Kwa mfano :- mume, hupata maumivu ya tumbo mara kueneza anapokuwa mdogo. Kwa upande wa mwanamke hupata maumivu ya tumbo anapoanza kuvunja ungo. Maumivu hayo hupelekea mtu (mume/mwanamke) kupata madhara katika viungo vyake vya uzazi.   DALILI ZAKE   Kwa mwanaume atakuwa akishiriki tendo la ndoa, anawahi sana kufika kileleni na kurudia mara nyingine ni vigumu sana. Pia mwanaume hatakuwa na uwezo wa kusimamisha. Ni vigumu kumpa mimba mwanamke. Mwanamke mwenye chango la uzazi ana dalili zifuatazo:-   Kupata maumivu makali wakati anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa Siku zake za hedhi hazitakuwa na ratiba, zitakuwa zinabadilika badilika Hujisikia homa kali anapokaribia s

Media zinaua muziki wa bongo: TID

"Media zinaua mziki wa bongo" TID Uhakika media · 16 hours ago Msanii wa kizazi kipya nchini Khalid Mohamed maarufu TID amefunguka na kusema kuwa utaratibu wa media kushusha wasanii pale wanapodai maslai yao na kuwapandisha wengine ndio kitu kinaathiri muziki wa Bongo Flava TID  ametoa kauli hiyo wakati akiongea na Wasafi TV  Muimbaji huyo ameeleza kuwa kitu hicho ndicho kilitokea kwenye muziki wake na kwa sasa kimemtokea Diamond.  “Na kweli anaweza because he has a media, yaani yeye ndio kama Mungu anajiona but mimi hapana. Nilifanya kosa hilo lakini kosa hilo ndilo limewasanua wasanii wengine, unaona msanii kama Diamond naye amekataa,” amesema na  kuongeza; “So Diamond was me lakini wakasema wewe siunajifanya mjanja sasa tunamleta Diamond tukushushe wewe. At the end Diamond naye wanataka kumuua, sijui wanataka kumuweka nani,”  TID amesema kuwa hajaona kitu kama hicho nchini Kenya kwani bado anamuona Jaguar ni msanii mkubwa, Nonini ni msanii mkubwa anapewa heshima yak

Magazeti ya leo 10/6/2018

MAGAZETI YA LEO 10/6/2018 Uhakika media  · 1 hour ago

Polisi, TRA wakamata kiwanda bubu kilimanjaro

Polisi, TRA wakamata kiwanda bubu Uhakika media 1  · 8 hours ago Polisi Mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani humo, wamekamata kiwanda bubu kinachotengeneza vinywaji vikali ambavyo vimepigwa marufuku hapa nchini.  Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Bwana HAMISI ISSA amethibitisha kukamatwa kwa vifaa mbalimbali vya kutengenezea pombe hizo katika nyumba  moja ya kuishi maeneo ya Msaranga Manispaa ya Moshi.  Amesema vifaa mbalimbali vya kutengeneza pombe hizo vimekamatwa zikiwemo chupa 1,600 na stika 800 zenye nembo feki za Mamlaka ya Mapato nchini pamoja na watu wawili waliokuwa wanatengeneza pombe hizo.  Naye Afisa Mwandamizi wa Kodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Kilimanjaro, Bwana TILSONI KABUJE amesema bidha hizo hazina ubora kutokana na kutengenezwa katika mazingura ambayo siyo salama pamoja na kuziingiza sokoni bila kulipa kodi. 

Waziri- Huduma usafishaji figo ni bure

Waziri - Huduma usafishaji figo ni bure Uhakika media 1  · 1 hour ago WAZIRI wa Afya Hamad Rashid Mohammed  amesema huduma za kitengo cha usafishaji figo  kwa wagonjwa wenye matatizo hayo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja zinaendelea kufanyika  bila ya malipo yeyote .  Hayo aliyasema huko katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wakati alipokuwa akifanya ziara ya kukagua kitengo hicho  na kuona jinsi kinavyoendelea na huduma zake    zinazofanyika katika sehemu hiyo kwa kuhudumia wagonjwa  kama kawaida.  Alisema lengo la ziara hiyo ni kuona jinsi wananchi wanavyofaidika na huduma hiyo  kwani Serikali inataka wananchi wake wasihangaike kutafuta huduma hiyo  kwa kuifuata nje ya nchi au masafa marefu.  Aidha alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuwajali wananchi wake  imekuwa iko imara katika kuhakikisha inakipa kipaumbele kwa kukipatia vifaa vyote  pamoja na dawa  za kusafishia mafigo.  “Wananchi mnapofikwa na matatizo haraka fikeni Hospitalini ili muweze kupata huduma dawa zipo za kut

Waweza kabisa kuwa daktari

WAWEZA KABISA KUWA DAKTARI Soma hapa Uhakika media 1 hour ago St. David college of health kimara temboni ni chuo pekee tanzania kinacho kupa fursa ya ndoto yako ya kuwa daktari bingwa.  ANZIA HAPA:   Uwe na ufaulu wa PCB  Physics Chemistry Biology.......angalau kwa alama D tu.. Mfumo umebadilika wa kudahili wanafunzi, sasa omba chuoni moja kwa moja badala ya kwenda NACTE. Pia ufaulu wa Hesabu na kiingereza ni sifa ya ziada /nyongeza sio ya lazima.  Ada ni nafuu mno na pia waweza soma kwa uwezo wa shughuli zako, Wasiliana nasi  0654 354949 / 0716044610 / 0718229977  

VIDEO:Samatta, Joti, Julio watamba wataja kikosi Kiba kitakacho wapiga timu Kiba

VIDEO: Samatta, Joti, Julio watamba wetaja kikosi kitakachowapiga timu Kiba Uhakika media minutes ago Kuelekea Mechi itakaoyopigwa mda mchache kuanzia sasa kwenye uwanja wa taifa kati ya timu Kiba na Samatta, Joti ametaja kikosi kitakachoivaa timu Kiba huku akiahidi ushindi. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI .......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Katibu mkuu wa UWT aahidi makubwa CCM

Katibu Mkuu wa UWT aahidi makubwa CCM Uhakika media 1  · 46 minutes ago Katibu Mkuu wa Umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndugu Queen Mlozi ameahidi kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na uzalendo uliotukuka ili CCM ishinde katika uchaguzi mkuu wa dola mwaka 2020.  Hayo ameyasema wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa ngazi mbali mbali za UWT Zanzibar hapo Afisi Kuu CCM Kisiwandui katika ziara yake ya kwanza kujitambulisha kwa viongozi na watendaji hao.  Alisema atatekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa lengo la kuimarisha taasisi hiyo ili kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ndani ya Umoja huo na Chama kwa ujumla.Ameeleza kwamba wanawake wa UWT wanatakiwa kuelekeza nguvu zao katika kulinda maslahi ya CCM ili ishinde kwa ngazi zote kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar katika uchaguzi Mkuu ujao.  Katibu Mkuu huyo amewashukuru viongozi viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi waliomuamini na kumteuwa kushika nafasi hiyo ya ngazi ya juu ya kiutendaji kupi

TRA. Wananchi acheni kufanya biashara za magendo

TRA - Wananchi acheni biashara za magendo Uhakika media 1  · 41 minutes ago Wito umetolewa  wanakijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga kuacha kushiriki kwenye biashara za magendo badala yake watumie maeneo yaliyorasmi kisheria kwa ajili ya upitishaji wa bidhaa.  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo wakati akizungumza na wananchi  kwenye mkutano uliofanyika eneo la sokoni akiwa ameambatana na maafisa wa TRA Mkoani Tanga.  Alisema kitendo cha wananchi kuacha kutumia bandari ya Pangani ambayo ipo kisheria wanafanya makosa makubwa na kuwataka kuitumia kupitisha bidhaa badala ya kutumia zile ambazo hazitambuliki ambazo watakapokamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria.  “Tumefika hapa kigombe kutoa elimu kwa kuzungumza na wananchi kutokana na changamoto za mara kwa mara biashara za magendo ambazo zimekuwa zikipitishwa eneo hilo na kuona kutumia muda huo kuzungumza na wan