KWA AMBAO HAWAJUI RATIBA YA WEEK IJAYO KATIKA LITRUJIA YA KANISA IPO HIVI :-
Posted by uhakika media
KESHO J3: Ni siku ambayo Yuda anajitoa maalum kabisa kwenye Jumuiya Ya mitume na anaanza mpango wake Kabambe wa kumuuza Yesu.
J4:- Ndio siku ambayo Yuda atatimiza mpango wake na atakabidhiwa vipande 30 vya Fedha.
J5:- Yesu anawatangazia Mitume wake mpango wa Yuda Japo kwa mafumbo na anaeleza waziwazi yale yatakayompata.
Alhamisi :- Usiku, Yesu anaweka Sakramenti 3.
1. Kitubio.
2. Upadre.
3. Ekaristi Takatifu.
Ijumaa :- Alfajiri Yuda anapokea kikosi chá Askari tayari kumsaliti Bwana wake, Mwalimu na Muumba wake. Hapa naomba niseme kidogo, kwa tamaduni za Waisraeli kulikuwa na Salamu za Mabusu za aina 3.
i. Salamu ya Bwana na mtumwa ambapo mtumwa alitakiwa kulala kifudifudi na kubusu miguu ya Bwana wake.
ii. Salamu ya Mwalimu na Mwanafunzi wake, ambapo Mwanafunzi alipaswa kupiga goti moja na kubusu mkono au mikono ya Mwalimu wake. Na hii ndio salamu ambayo Yuda alipaswa kumsalimia Bwana Yesu siku zote hata pale katika Bustani Ya Gethsemane. Hata ministranti hufanya hili pale wanapokutana na mapadre au wakati wa kutoa amani.
iii. Salamu ya Mwalimu kwa Mwalimu, Bwana kwa Bwana, Wakuu kwa Wakuu. Hawa husalimiana kwa kubusiana mashavu.
Mpaka hapa mtaelewa usaliti wa Yuda jinsi ulivyomkubwa na nini maana ya Swali la Yesu kwa Yuda, "Yuda unamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu? ".
Yesu saa 03:00 Asubuhi anahukumiwa Kufa, Saa 06:00 Mchana anasulubiwa, saa 09:00 Alasiri anakufa na saa 12:00 jioni anazikwa.
Jumamosi :- Inaitwa Black Saturday, au Jumamosi nyesui, Bwana wa Sábato, Bwana wa Kanisa Yupo Kaburini. Wanateologia wanasema Yesu alikwenda Toharani kuwatia moyo watakatifu majeruhi na kisha Limbo kuwatia moyo watakatifu.
Kanisa linakuwa katika kimya hakuna Ibada inayoruhusiwa kufanyika.
Usiku wa Black Saturday tunaanza vijilia au Mwanzo wa kesha la Yesu Mfufuka.
Jumapili :- Kristu Mfufuka anafufuka na kushinda mauti, anaweka misingi mpya ya Kanisa.
NAWATAKIA TAFAKARI NJEMA YA WEEK HII.

Maoni
Chapisha Maoni