Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Mgodi wafungwa baada ya raia wa kichina kufariki

Mgodi wafungwa baada ya raia wa kichina kufariki dunia Uhakika media 5  · 35 minutes ago MGODI wa dhahabu katika Kijiji cha Nyamitondo wilaya na mkoani Geita umefungwa baada ya raia wawili wa China kufariki ndani ya shimo lenye urefu wa zaidi ya mita 100 kwa kulipukiwa na baruti wakati wakivunja miamba.  Wachina hao, imeelezwa, walikuwa wakivunja miamba ya dhahabu katika mgodi huo bila ya kuwa na vyeti vya kulipiua baruti.  Mgodi huo unamilikiwa kwa ubia baina ya Mayala Ngweso na kampuni ya Kichina ya Taichangain Tanzania Group.Akitoa tamko la kufunga mgodi jana, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Geita, Alli Maganga alisema hatuahiyo inalenga kupisha uchunguzi wa kina.  Pia, alisema Maganga, hatua hiyo itashinikiza   mgodi huo kutekeleza masharti na maelekezo uliopewa na serikali ili kuhakikisha sheria na kanuni za madini zinazingatiwa na kufuatwa.  Maganga alisema raia wawili wa China waliotambuliwa kwa majina ya Li Shaobin (44) na Qian Zhaorang (49)w...

DCI:Awataka walio potelewa na ndugu wawasilishe DNA

DCI awaita waliopotelewa na ndugu wawasilishe DNA Uhakika media 5  · 28 minutes ago MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, amewaita wananchi waliopotelewa na ndugu zao kufika kwa ajili ya utambuzi wa miili ya watu waliookotwa kwenye viroba pembezoni mwa bahari.  Boaz amesema tangu Jeshi la Polisi litangaze kwa wananchi kwa kuwataka waliopotelewa na ndugu kufika kutambua ndugu zao, hakuna mtu yeyote aliyejitokeza.  Oktoba 5, mwaka jana Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, alitoa wito kuwa kama kuna mtu ambaye ndugu yake amepotea afike makao makuu ya jeshi hilo kitengo cha DCI, ili kufanya uchunguzi kuona kama ni ndugu yake au la.  Pia aliwataka wananchi waliopotelewa na ndugu zao wafike kwa ajili ya kuchukua vinasaba (DNA), baada ya miili 15 kuokotwa ikiwa imefungwa kamba katika fukwe za Bahari ya Hindi.  Akizungumza na Nipashe, Boaz alisema tangu kutolewa kwa tangazo hilo hadi sasa hakuna mwananchi yeyote aliyejitokeza....

Afungwa kifungo cha maisha jera kwa kumbaka mtoto wa miaka 9

Afungwa maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 9 Uhakika media 5  · 21 minutes ago Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Shadrack Majimbo mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa Nakuru nchini Kenya, amehukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 9 na kumuambukiza magonjwa ya zinaa.  Hakimu Judicaster Nthuku amesema kuwa ushahidi unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyo alifanya vitendo hivyo vya ubakaji, na ripoti ya daktari kuthibitisha hilo huku akimuambukiza ugonjwa wa zinaa aina ya ngono.  Mahakama imeelezea kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya binti huyo, ambapo siku ya tukio alimuita na kumtaka kumsaidia kazi za nyumbani, na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili na udhalilishaji.  Sambamba na hilo mwanaume mwengine mwenye umri wa miaka 74 aliyetambulika kwa jina la Kipngeno arap Bor katika eneo la Subukia nchini Kenya huko huko Nakuru, amehukumiwa miaka 10 jela kwa kosa la kumbaka mjukuu wake, ambaye ...

Mwanaume aliye tembea na suruali yake miguuni auawa na polisi Marekan

Houston:Mwanaume aliyetembea na suruali yake miguuni auawa na polisi Marekani Uhakika media Kulingana na ndugu zake mkewe Bw. Thomas aliwauwa watoto wake wawili mwaka 2016 Afisa wa polisi nchini Marekani amempiga risasi na kumuua mtu ambaye hakuwa na silaha aliyekuwa akitembea barabarani huku suruali yake ikiwa miguuni. Familia yake inasema mauaji hayo yanaonekana yaliyokuwa ''yamepangwa'' Kamera za video ya polisi inaonyesha kuwa Danny Ray Thomas, mwenye umri wa miaka 34, akitembea mkabala na afisa wa polisi kwenye barabara mjini Houston, Texas, Alhamisi iliyopita kabla ya kumpiga risasi. Afisa huyo wa polisi Cameron Brewer alirudia mara kadhaa akipaza sauti "lala chini ardhini" kabla ya kufyatua risasi. Polisi na mwathiriwa wote ni Wamarekani weusi.

HATARI KUU ZINAZO JIFICHA NDANI YA BAFU

Hatari kuu zinazo jificha ndani ya bafu lako: Uhakika media Maji yakitiririka kutoka kwenye kifaa bafu ya kutumia manyunyu Watafiti katika nchini Uingereza wanasema kuwa usafi wa bafuni ni jambo linalofaa kuzingatiwa kuliko wengi wanavyodhania. Profesa John Oxford, katika chuo Kikuu cha Queen Mary University cha London,ameiambia BBC kuwa: "Bafu ni mahali ambapo usafi wake huwa ni mgumu'' "Watu hutumia muda wao katika kusafisha vyoo vyao lakini ingelikuwa vyema kama kila mtu angezingatia zaidi usafi wa bafu kwa kutumia madawa ya kuuwa bakteria." 1.Kuoga kwa kutumia kifaa cha kukumwagia maji mwilini kwenye bafu za manyunyu Wataalamu wanasema unapotumia kifaa hiki kwenye bafu za manyunyu hunabudi kuwa makini sana, kwani kinapotumika baada ya kuzimwa kwa muda mrefu na kutumiwa tena hugeuka kuwa makao ya vimelea vya bakteria. Hatari nyingine kwa watu wazima na watoto itokanayo na kifaa hicho (shower) ni uwezekano wa kuunguzwa na maji yanayotoka kwenye ...

TWAWEZA WAFUNGUKA HAYA KUHUSU SERIKALI

Twaweza: RaiaTanzania wanasema hawako huru kukosoa kauli za utawala. Wananchi wangependa kuwa huru kukosoa watawala iwapo hawataridhika na maamuzi ya Serikali Idadi kubwa ya wananchi (60%), nchini Tanzania wanasema hawako huru kukosoa kauli zinazotolewa na Rais wakati asilimia 54 wanasema hivyo kuhusu kauli zinazotolewa na Makamu wa Rais na asilimia 51 Waziri Mkuu. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la utafiti lisilo la serikali, Twaweza. Wananchi wanajisikia huru zaidi kuwakosoa wabunge wao kuliko wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Kwa mujibu wa shirika la Twaweza, hali hii inaweza kuwa ni kwa sababu wananchi wanawachagua wabunge kuwa wawakilishi wao na hivyo wanaona kuwa mbunge anajukumu la kusikiliza mahitaji na vipaumbele vyao na kuvifanyia kazi ipasavyo. Wananchi wanaunga mkono kwa kiasi kikubwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari. Wananchi nane kati ya kumi (81%) wanaona ukosoaji wa viongozi wa taifa kama jambo muhimu kwani itawasaidia kujire...

Urusi yatimua wanadiplomasia 60 Marekani

Urusi yatimua wanadiplomasia 60 Marekan. Uhakika media  Lavrov anasema Urusi itachukua hatua kwa nchi zote zilizowafukuza wanadiplomasia wake Urusi imewafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani, na kufunga ubalozi uliopo St Petersburg ikiwa ni majibu kwa kitendo cha Marekani kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi juu ya shutuma ya Uingereza kuhusu kuhusika kwa Urusi katika shambulio la jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Kripal na binti yake huko Uingereza. Hatua hiyo ilitangazwa na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov. Zaidi ya nchi ishirini zimewafukuza wanadiplomasia wa urusi nchini mwao katika kuunga mkono Uingereza. Miongoni mwa nchi hizo ni Marekani ambapo mapema wiki hii iliwatimua wanadiplomasia 60 wa urusi kuondoka Marekani. Boris Johnson anasema hatua hiyo ya Urusi ni sawa na kutaka kuwasha moto zaidi Katika kujibu hilo Urusi imewatimua wanadiplomasia 58 kutoka Moscow na wawili kutoka mji wa Yekaterinburg, chombo cha habari cha Interfax kiliripoti. Lavrov a...