Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Mwanasiasa wa Kenya aliye jiuzuru na kusafirishwa kilazima atua Canada

Mwanasiasa wa Kenya aliyezuiliwa na kusafirishwa kilazima atua Canada Uhakika media 2  · 40 minutes ago Mwanasiasa wa upinzani aliyezuiwa kuingia Kenya wiki iliyopita na kusafirishwa kwa lazima hadi Dubai ameelekea nchini Canada, vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti.  Bw Miguna Miguna, ambaye ni wakili, amesafiri kwa ndege iliyokuwa ikielekea Toronto, Canada, baada ya kukaa katika uwanja wa kimataifa wa Dubai kwa siku nne.  Gazeti la Nation, limesema afisa mmoja wa serikali amewafahamisha kwamba Bw Miguna aliondoka Dubai akitumia ndege ya Air Canada 57 (ACA57) baada ya kuwasilisha pasipoti yake ya Canada.  Wakili huyo alikuwa amesema hakuwa na pasipoti hiyo alipowasili uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi Jumatatu wiki iliyopita.  Wakili wake Cliff Ombeta hata hivyo ameambia BBC kwamba mteja wake hakuwa na pasipoti hiyo.  Aidha, amesema kwa sasa hawezi kuthibitisha iwapo Bw Miguna yumo safarini kuelekea Canada.  Safari ya ndege kutoka ...

Serikali ya kijiji yapiga marufuku kuoa bila taarifa

Serikali ya Kijiji yapiga Marufuku kuoa bila taarifa Uhakika media 2  · 27 minutes ago SERIKALI ya Kijiji na Kata ya Nsalala Tarafa ya Itwangi Shinyanga Vijijini, imetunga sheria ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni, kwa kumtaka mwananchi anayetaka kuoa ama kuozesha kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji. Lengo la marufuku hiyo ni ili kijiridhisha kama anayeolewa siyo mwanafunzi au msishana chini ya umri wa  miaka  18. Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nsalala, Sandeko Machungo, kwenye mdahalo wa kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia ndani ya jamii kupitia mitandao ya kijamii, ulioandaliwa na Shirika la Kivulini linalotetea haki za watoto na wanawake kwa ufadhiri wa shirika la OXFAM la Uingereza. Alisema viongozi wa Serikali ya kijiji mara baada ya kupata elimu ya ukatili wa kijinsia kupitia mashirika mbalimbali, wameona ni vyema wakatunga sheria ndogo kijijini ya kuzuia wananchi kuoa amakuozesha bila ya kutoa taarifa kwe...

Kamati kuamua rufaa ya Wambura

Kamati kuamua rufaa ya Wambura Uhakika media 5  · 21 minutes ago RUFAA ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura, sasa imefikia patamu baada ya juzi Jumamosi kusikilizwa katika makao makuu ya shirikisho hilo, Karume jijini Dar es Salaam na hivi sasa watu wengi wanataka kujua nini kinachofuatia.  Hivi karibuni, Wambura alikata rufaa Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF kupinga maamuzi ya Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo ya kumfungia maisha kujihusisha na soka kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine.  Wakili wa Wambura, Emmanuel Muga, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, kamati hiyo iliziita pande mbili zote zinazochuana katika sakata hilo na kuzisikiliza kwa umakini mkubwa.  Alisema katika kikao hicho, mambo yalienda vizuri, kwa hiyo kinachosubiriwa tu hivi sasa ni maamuzi ya hiyo kamati.  “Kamati imesikiliza kwa umakini utetezi wa Wambura, vilevile TFF nao wakizun...

Watanzania acheni kulalamika, Askofu Cheyo

"Watanzania acheni kulalamika" Askofu Cheyo Uhakika media 2  · 11 minutes ago Askofu Kiongozi wa  Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi Alinikisa Cheyo, amewaasa Watanzania kuacha kulalamika na badala yake wajikite katika kufanya kazi njema inayompendeza Mungu.  Askofu Cheyo ametoa kauli hiyo katika ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi ushirika wa Mbeya Mjini.  Askofu amesema ili  Watanzania waweze  kujiletea maendeleo yenye tija kufikia uchumi wa kati wanapaswa kuachana na mambo ya kisiasaili waweze  kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato.  Askofu Cheyo pia ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wake wengine wa dini nchini kutofautisha dini na siasa ili kujenga upendo miongoni mwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kudumisha amani ya nchi.

Mtulia, Mollel kuapishwa mkutano wa 11 wa Bunge unao anza kesho

Mtulia, Mollel kuapishwa mkutano wa 11 wa Bunge unaoanza Kesho Uhakika media 2  · 6 minutes ago Wakati kesho Aprili 3, 2018 ukitarajiwa kuanza kwa mkutano wa 11 wa Bunge utakao malizika Juni 29, 2018 Mjini Dodoma.  Wabunge wateule wawili kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni, Maulid Mtulia (Kinondoni) na Dk. Godwin Mollel (Siha), wanatarajia kuapishwa hiyo kesho.  Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Bunge Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, wabunge hao wateule wataapishwa katika Mkutano wa 11 wa Bunge utakaoanza kesho Jumanne Aprili 3, Mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya mijadala na kupitisha Bajeti ya Serikali na kujadili hotuba ya hali ya uchumi wa taifa itakayowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango.  Aidha, Bunge litajadili utekelezaji wa bajeti za wizara zote kwa mwaka wa fedha 2017/18 na makadirio ya matumizi ya Serikali kwa mwak...

Conte hana nafasi ya kuendelea Chelsea musimu ujao

Conte hana nafasi ya kuendelea Chelsea msimu ujao Uhakika media 5  · 2 hours ago Kocha wa Chelsea, Antonio Conte, hapewi nafasi ya kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kwa msimu ujao kutokana na kiwango cha timu kutoridhisha.  Mwandishi na Mchambuzi wa soka katika kituo cha Sky Sports, Garry Neville, amesema hampi nafasi ya kuendelea na Chelsea kufuatia kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Tottenham Hostpurs Jumapili ya jana katika mchezo wa Ligi Kuu England.  Neville ameeleza kuwa itakuwa ngumu Conte kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo mpaka sasa ipo nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi, "Sidhani kama ataendelea kuwepo Chelsea msimu ujao'' alisema Neville.  Conte alitwaa ubingwa wa EPL msimu wa kwanza alipojiunga na Chelsea 2016/17 lakini mambo yamekuwa magumu zaidi msimu huu kwa kikosi chake kutokuwa na makali kama ya msimu uliopita.

Baada ya kutolewa kwenye michuano yanga kurejea Dar

Baada ya kutolewa kwenye michuano Yanga kurejea Dar Uhakika media 5  · 2 hours ago Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho jana dhidi ya Singida United, kikosi cha Yanga kinatarajia kuwasili leo Dar es Salaam.  Yanga ilishindwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kichapo cha matuta (4-2) kutoka kwa walima alizeti hao, hiyo ilikuwa ni mara baada ya dakika 90 kwenda sare ya 1-1.  Yanga inarejea Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha FC ya Ethiopia utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii Uwanja wa Taifa. Endapo Yanga itafanikiwa kuingia hatua ya makundi katika michuano ya Shirikisho Afrika, itajitwalia kiasi cha milioni 600 kutokana na taratibu za CAF zilivyo ambapo kila anayeingia hatua hiyo hupewa kitita hicho cha pesa.