Uhakika media 5 · 2 hours ago
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte, hapewi nafasi ya kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kwa msimu ujao kutokana na kiwango cha timu kutoridhisha.
Mwandishi na Mchambuzi wa soka katika kituo cha Sky Sports, Garry Neville, amesema hampi nafasi ya kuendelea na Chelsea kufuatia kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Tottenham Hostpurs Jumapili ya jana katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Neville ameeleza kuwa itakuwa ngumu Conte kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo mpaka sasa ipo nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi, "Sidhani kama ataendelea kuwepo Chelsea msimu ujao'' alisema Neville.
Conte alitwaa ubingwa wa EPL msimu wa kwanza alipojiunga na Chelsea 2016/17 lakini mambo yamekuwa magumu zaidi msimu huu kwa kikosi chake kutokuwa na makali kama ya msimu uliopita.
Maoni
Chapisha Maoni