Uhakika media 5 · 2 hours ago
Kocha wa vinara wa ligi kuu soka ya England EPL Manchester City Pep Guardiola, amesema safu ya mbele ya klabu ya Liverpool inayoongozwa na Mohamed Salah haizuiliki kirahisi.
Guardiola ameyasema hayo kuelekea mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Man City watakuwa wageni wa Liverpool Jumatano April 4 kabla ya kurudiana wiki mbili zijazo.
"Sio Salah tu ni wote watatu Mane na Firmino, wameshindaka kutoka na kiwango chao cha kufunga, kwasasa ni safu kali na yakuogopa sana'', amesema Pep Guardiola ambaye timu yake inaongoza ligi ikiwa na alama 84.
Msimu huu tayari Mohamed Salah ana mabao 37 huku Roberto Firmino na Sadio Mane kwa pamoja wana mabao 38. Nyota hao wote walihusika kwenye ushindi wa mabao 4-3 iliopata Liverpool dhidi ya Man City Januari 14.
Aidha Guardiola ameongeza kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwani Liverpool kwa ujumla ipo kwenye kiwango kizuri msimu huu na michuano ya Ligi ya Mabingwa ikifikia hatua ya robo fainali kila mechi huwa ni ngumu.
Maoni
Chapisha Maoni