Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Magazeti ya leo 9/6/2018

MAGAZETI YA LEO 9/6/2018 Uhakika media  3 hours ago

Serikali yaingilia kati tukio la mwanamke kujifungulia nje ya kituo cha polisi

Serikali yaingilia kati suala la Mwanamke kujifungulia nje ya Kituo cha Polisi Uhakika media 5  · 4 hours ago Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya askari polisi waliosababisha mwanamama Amina Rafael kujifungua nje ya kituo cha Polisi cha Mang’ula huko mkoani Morogoro.  Kauli hiyo ya Masauni imekuja baada ya kutakiwa kutoa maelezo na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuhusiana na madai hayo yaliyotolewa na Mbunge wa Arumeru Mashariki , Joshua Nassari aliyetaka suala hilo lijadiliwe ndani ya Bunge na kwamba ni matukio yanayoendelea kujitokeza ikiwamo Dar es Salaam, Tarime na Mwanza.  Naibu Waziri Masauni amesema, serikali imesikitishwa na suala hilo na tayari jalada la uchunguzi limeshafunguliwa.  Akielezea tukio hilo Masauni amesema "kulikuwa na tukio la wizi, lililomhusisha mume wa huyu mama, (Abdallah Mohamed), anayedaiwa kununua vitu vya wizi ambavyo vilikutwa katika nyumba yake, Polisi walimtaarifu ...

Kigoma kujenga vizuizi kuzuia ajali

Kigoma kujenga vizuizi kuzuia Ajali Uhakika media 5  · 4 hours ago Serikali imesema itahakikisha inajenga Vizuizi katika maeneo ambayo Barabara imepishana na reli ili kudhibiti Ajali katika maeneo hayo na Magari yawe yanasimama wakati Treni ikipita.   Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga ikiwa zimepita Siku mbili tangu kutokea kwa Ajali ya basi dogo lililogonga treni eneo la Gungu mkoani Kigoma na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine 35 kujeruhiwa.  “Haiwezekani watu wapoteze maisha kwa sababu ya uzembe wa baadhi ya madereva. Tumechoka kuona hali hii ikiendelea na lazima tuchukue hatua kuokoa maisha ya binadamu wenzetu," amesema.   Amesema ujenzi wa vivuko utahusisha wakala wa barabara (Tanroads) na Shirika la Reli Tanzania(TRC) ambao wataratibu na kujenga vizuizi hivyo.  Maeneo ambayo reli imepishana na barabara mkoani Kigoma ni Kibirizi, Gungu, Nyamoli, Kazuramimba, Uvinza, Tubira na Malagalasi. 

CHADEMA Wanena mazito kwa wanachama wake

Chadema: Nataka kuwahakikishia watanzania kwamba CHADEMA iko imara kuliko jana Uhakika media 5  · 4 hours ago Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefunguka na kudai hakijawahi kushindwa uchaguzi wowote ule ambao umefanyika katika ardhi ya Tanzania bali kinachowapata ni kupokwa matokeo yao na kurundikwa katika chama kingine cha siasa. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA),  Patrick Ole Sosopi wakati alipokuwa anazungumza kwenye media tour yake leo Juni 08, 2018 Jijini Dar es Salaam na kusema ushahidi wa jambo hilo ni mmoja wapo ni uchaguzi wa mdogo wa marudio katika Jimbo la Kinondoni ambapo sanduku la kuwekea kura liliibwa mbele ya askari polisi na likarudishwa huku kukiwa hakuna mtu yoyote aliyekamatwa. "Nataka kuwahakikishia watanzania kwamba CHADEMA iko imara kuliko jana, kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa ndio inaathari kwa sababu kazi yetu ni siasa,upande wa pili anatuimarisha zaidi sababu nyuma ya pazia kila mtanzani...

Chuo cha Royal Collage na vingine 20 vyafungiwa NACTE

Chuo cha Royal College na vingine 20 vyafungiwa na Nacte Uhakika media 5  · 4 hours ago Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) limefuta usajili wa vyuo 20 baada ya kushindwa kufuata sheria zinazoendana na matakwa ya usajili wa vyuo hivyo.  Akizungumza leo Juni 8, Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo Dk Adolf Rutayuga amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa vyuo 458 na 32 vilikutwa na mapungufu.  Sanjari na 20 vilivyofungiwa vyuo tisa vimezuiliwa kudahili wanafunzi wapya huku vyuo vitatu vikitakiwa kusitisha baadhi ya kozi walizokuwa wakitoa bila idhini ya baraza.  Dk Rutayuga amesema tayari baraza hilo limeshaviandikia barua vyuo 20 vilivyofungiwa kuvitaka vihakikishe kuwa wanafunzi wanahamia kwenye vyuo vingine.  Vyuo vilivyofutiwa usajili ni Royal College, Covenant College of Business Studies,  Mugerezi Spatial Technology College, Techno Brain, Lisbon Business College, PCTL Training Institute na Mlimani School of Professi...

Yanga yaikwepa simba Kagame

Yanga waikwepa Simba, Kagame Uhakika media · 3 hours ago Tetesi zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Yanga imeiandikia barua Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), kuwaomba kujitoa katika mashindano ya Kagame CUP yanayotarajiwa kuanza June 28 mpaka Julai 13 2018 jijini Dar es Salaam.  Sababu za msingi ziliifanya Yanga kuandika barua hiyo ni kufanya maandalizi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18 jijini Nairobi.  Kutokana na muingiliano wa ratiba ya KAGAME na CAF, Yanga wameona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM Alger pia Rayon Sports ya Rwanda.  Eatv.tv imemtafuta Katibu wa klabu hiyo Boniphace Mkwassa ambaye amethibitisha kuwa Kamati ya Utendaji wa klabu, wameazimia kufanya maamuzi hayo ili kuepuka kubanwa na muingiliano wa ratiba hiyo ambayo imekuwa si rafiki kwao.  Kufuatia kuandika baru...

Serikali yajibu mwanamke kujifungulia polisi

Serikali yajibu tukio la mwanamke kujifungulia Polisi Uhakika media 5  · 54 minutes ago Kufuatia tukio la mwanamke mjamzito kujifungua kwenye Kituo cha Polisi Mang’ula mkoani Morogoro, serikali imebanwa bungeni na kutakiwa kutoa ufafanuzi.  Hoja hiyo iliibuliwa na Mbunge wa Meru, Joshua Nassari ambapo alitaka kujua kwa nini mwanamke huyo mjamzito aliyekuwa akikaribia kujifungua alikamatwa na kuwekwa mahabusu na baadaye uchungu kumbana akiwa nyuma ya nondo kabla ya baadaye kutolewa na kujifungua nje ya kituo hicho.  Akitoa ufafanuzi, Naibu Waziri wa Ndani, Hamad Masauni, amekiri kwamba busara haikutumika katika sakata hilo kwani chanzo cha kukamatwa kwake ni mali za wizi zilizonunuliwa na mumewe kukutwa ndani ya nyumba yake. Waziri Masauni ameeleza kwamba serikali inafuatilia kwa kina na wote waliohusika watachukuliwa hatua zinazostahili.