Uhakika media 5 · 4 hours ago
Serikali imesema itahakikisha inajenga Vizuizi katika maeneo ambayo Barabara imepishana na reli ili kudhibiti Ajali katika maeneo hayo na Magari yawe yanasimama wakati Treni ikipita.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga ikiwa zimepita Siku mbili tangu kutokea kwa Ajali ya basi dogo lililogonga treni eneo la Gungu mkoani Kigoma na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine 35 kujeruhiwa.
“Haiwezekani watu wapoteze maisha kwa sababu ya uzembe wa baadhi ya madereva. Tumechoka kuona hali hii ikiendelea na lazima tuchukue hatua kuokoa maisha ya binadamu wenzetu," amesema.
Amesema ujenzi wa vivuko utahusisha wakala wa barabara (Tanroads) na Shirika la Reli Tanzania(TRC) ambao wataratibu na kujenga vizuizi hivyo.
Maeneo ambayo reli imepishana na barabara mkoani Kigoma ni Kibirizi, Gungu, Nyamoli, Kazuramimba, Uvinza, Tubira na Malagalasi.
Maoni
Chapisha Maoni