Uhakika media · 3 hours ago
Tetesi zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Yanga imeiandikia barua Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), kuwaomba kujitoa katika mashindano ya Kagame CUP yanayotarajiwa kuanza June 28 mpaka Julai 13 2018 jijini Dar es Salaam.
Sababu za msingi ziliifanya Yanga kuandika barua hiyo ni kufanya maandalizi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18 jijini Nairobi.
Kutokana na muingiliano wa ratiba ya KAGAME na CAF, Yanga wameona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM Alger pia Rayon Sports ya Rwanda.
Eatv.tv imemtafuta Katibu wa klabu hiyo Boniphace Mkwassa ambaye amethibitisha kuwa Kamati ya Utendaji wa klabu, wameazimia kufanya maamuzi hayo ili kuepuka kubanwa na muingiliano wa ratiba hiyo ambayo imekuwa si rafiki kwao.
Kufuatia kuandika barua hiyo ya kuomba kujiondoa, Yanga wanakuwa wameikwepa Simba kwenye mashindano ambapo walikuwa wamepangwa pamoja na mabingwa hao wa Ligi Kuu.
Simba na Yanga zilipangwa pamoja kwenye kundi C ambapo kuna timu zingine ambazo ni Dakadaha ya Somalia pamoja na St. George kutoka Ethiopia.
Maoni
Chapisha Maoni