RC Morogoro apiga marufuku stendi bubu
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Steven ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, kupiga marufuku uwepo wa stendi bubu katika manispaa hiyo kwa madai zimekuwa zikichangia upotevu wa mapato.
KEBWE ametoa agizo hilo wakati akifungua baraza maalumu la halmashauri ya Manispaa ya Morogoro cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu serikali kwa mwaka 2016-17.
Kwaupande wake Mkaguzi Mkuu wa nje wa hesabu za Serikali Mkoa wa Morogoro Bw. MWAMBANGA PETER amesema madiwani wanawajibu mkubwa wa kusimamia halmashauri ili kuhakikisha masaula yote ya mapatao ya halimashauri yanakwenda vizuri.
Marufuku hiyo iliyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa inalenga kuondosha stendi zote zisizo rasimi ndani ya Mkoa wa Morogoro lengo ikiwa ni kuhakikisha kunakuwa na uratibu mzuri wa mapato yatokanayo na tozo katika stendi.
Uhakika media · 22 minutes ago

Maoni
Chapisha Maoni