Uhakika media 5 · 29 minutes ago
Waziri Netanyahu amesema Israel inaunga mkono uamuzi huo wa Marekani ulioungwa mkono na Ufaransa pamoja na Uingereza.
"Tumekuwa tukiunga mkono uamuzi wa Trump dhidi ya silaha za kemikali toka mwaka mmoja uliopita",alisema Netanyahu.
Israel inaamini serikali ya Assad inapashwa kudhibitiwa vilivyo ili kuhakikisha kuwa haitumii silaha za kemikali dhidi ya halaiki.
Marekani,Uingereza na Ufaransa zimefanya shambulizi la anga dhidi ya serikali ya Assad nchini Syria.
Hii ni baada ya shambulizi baya la kemikali kutokea Douma na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70 wengi wao wakiwa ni watoto wadogo.
Maoni
Chapisha Maoni