Uhakika media 5 · 7 hours ago
Mrembo na muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama 'Monalisa' ameibuka mshindi kwenye tuzo za 'The African Prestigious Awards' nchini Ghana akimbwaga mpinzani wake Lupita Nyong'o.
Katika tuzo hizo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo huko jijini Accra nchini Ghana Monalisa ametwaa tuzo katika kipengele cha 'Best African Actress'. Kwa mujibu wa tuzo hizo Monalisa sasa ndiye muigizaji bora wa kike barani Africa.
Monalisa amethibitisha ushindi wake kupitia mtandao wa 'Instagram' ambapo amepandisha picha akiwa na tuzo yake na kuandika ujumbe huu ''Tumeshindaaaaaaa narudi home na Tuzo za kutosha.Ahsante Watanzania,Nawapenda mno''.
Kwa ujumbe huo wa Monalisa unaashilia huenda pia kuna tuzo nyingine wameshinda Watanzania ambao walikuwa wanawania vipengele mbalimbali katika tuzo hizo kubwa za filamu nchini Ghana.
Watanzania wengine waliokuwa wanawania ni King Majuto kipengele cha Mchekeshaji Bora Afrika, Vicent Kigosi kipengele cha msanii Bora wa Kiume Afrika na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein katika kipengele cha Mpiga Picha Bora Afrika.
Maoni
Chapisha Maoni