Uhakika media 5 · 34 minutes ago
Kocha wa Mabingwa watetezi wa La Liga Zinedine Zidane, amepangua kikosi chake na kuwaacha nyota Cristiano Ronaldo na Gareth Bale kuelekea mchezo wao wa ligi leo dhidi ya Malaga.
Zidane amewapa mapumziko nyota hao baada ya kuisadia timu hiyo kushinda mchezo wa robo fainali dhidi ya Juventus na kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya jumatano iliyopita.
Kiungo Luka Modric pia ameondolewa kwenye kikosi cha wachezaji 20 hivyo kufanya timu hiyo kusafiri kwenda La Rosaleda na wachezaji 19 pekee. Inaaminika nyota hao watatu wameachwa ili kuwapa nafasi ya kuwa vizuri kwenye mechi dhidi ya Bayern Munich.
Real Madrid ambayo inashika nafasi ya 4 leo inaweza kurejea katika nafasi ya 3 endapo itaibuka na ushindi huku Malaga inapigania kukwepa kushuka daraja ikiwa inaburuza mkia.

Maoni
Chapisha Maoni