Hii ndio Barua ya Profesa Kitila Mkumbo Kwenda kwa Mkuu wa Kanisa la KKKT Uhakika media 5 · 1 hour ago Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) S. L. P. 3033 ARUSHA. Mheshimiwa Baba Askofu, Shalom! YAH: MAMBO MATANO AMBAYO HAYAPONYI KATIKA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT Jina langu ni Kitila Mkumbo, muumini katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambalo wewe ndiye mkuu wake. Kikazi, mimi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Dodoma. Kitaaluma, mimi ni mhadhiri mwandamizi katika Saikolojia na Elimu nikiwa na cheo cha Profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mheshimiwa Baba Askofu, kwa unyenyekevu mkubwa nimeamua kukuandika barua hii ili kutoa maoni yangu binafsi kwa kanisa unaloliongoza kupitia kwako kuhusu maudhui ya waraka uliotolewa na waheshimiwa maaskofu wa KKKT siku ya Jumamosi tarehe 24 Machi 2018. Waraka huo ulitarajiwa kusomwa katika makanisa siku ya Jumapili...
Maoni
Chapisha Maoni