Uhakika media 5 · 1 hour ago
Ikiwa zimepita takribani siku mbili tokea mrembo Nandy kuomba radhi kutokana na video yake ya faragha kusambaa mitandaoni, msanii Dogo Janja ameibuka na kudai wasanii hawana umoja na wanafiki huwa wanafurahi sana kuona mwenzao amepatwa na majanga ili mradi apotee katika tasnia.
Dogo Janja ametoa kauli hiyo usiku wa kuamkia leo Aprili 15, 2018 kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii na kusema anahisi anaweza kuchukiwa leo hii na wasanii wenzake ila ni lazima yeye aongee ukweli ili mradi donda ndugu liliopo katika muziki limepone.
"Wasanii sisi ni ma-snichi sana aise, baada ya hii ishu ya Nandy ndio nimepata uhakika. Wakati wa ishu ya Roma nilianza kuliona jinsi kwenye makundi pembeni watu kibao walikuwa wanafurahi tena maneno kibao kama atakoma, amezoea huyo. Jana na juzi nimekaa na watu wasanii wakubwa tu na wote walikuwa wanasema bora limemtokea Nandy hili angalau spidi za 'show' zitapungua", amesema Dogo Janja.
Pamoja na hayo, Dogo Janja ameendelea kwa kusema "bora BASATA ingemfungia miezi 6 apotee kidogo, walikuwa wanapiga stori kama utani ila moyoni nimefikiria sana. Wasanii tuache roho mbaya, wote sisi masikini tunahangaikia ugali. Tukipata ajali kazini, tusiombeane mabaya tutafute amani".
Kwa upande mwingine, Dogo Janja amewashauri wasanii wenzake wawe na moyo wa upendo kwa wenzao na waache tabia ya kufurahia matatizo wanayowapata wakiwa kazini.
Maoni
Chapisha Maoni