MBINU BORA ZA KULEA VIFARANGA VYA KUKU
Uhakika media / 3 weeks ago
Kuna vitu vya msingi katika uleaji wa vifaranga vya kuku. Uleaji huu hutofautiana kati ya vifaranga wa kuku wa mayai, kienyeji na kuku wa nyama katika chakula na chanjo kwa ujumla
MATAYARISHO
· Banda liwe imara kuepuka wizi na wanyama wasumbufu kama ngoja, paka, mbwa, mwewe, na kecheche.
· Banda liwe linaweza kuingiza hewa ya kutosha na kavu isiyo na unyevunyevu.
· kabla ya kuingiza safisha banda nje na ndani kwa kutumia dawa ya kuua vijidudu vya magonjwa. Paka chokaa kuta za ndani na hakikisha banda haliwi na joto Kali, baridi kuingiza, mbua na upepo mkali.
· Tayarisha chakula bora.
· vifaa vya kulishia na kunyweshea maji.
· Tandiko safi, kama vile maranda, pumba za mchele.
· Dawa
KABLA YA KUFIKA VIFARANGA
Banda liwe tupiu kwa wiki moja baada ya kusafisha kwa dawa. Vifaranga utakaopewa watoke kwenye mzalisha mwenye historian nzuri.
· Usichanganye vifaranga wa sehemu tofauti.
· Vifaranga huweza kuathirika haraka na mazingira hivyo yafaa kuwa na uangalifu wa hewa, mwanga na joto.
· Vifaa vya mwanga na joto ni muhimu na lazima katika kulea vifaranga.
· Tangazi za msuara kwa kutumia hard board yenye urefu wa sentimita 60 na katikati weka balbu au Niko la mkaa na taa ya mafuta; Kwisha mwanga wa kutosha ili vifaranga waone chakula na maji.
· weka chokaa halafu maranda na tandiko chilk paper au magazeti juu. ya maranda.
· Masaa matano kabla ya kufika vifaranga washa taa za joto au jiko la mkaa kwa ajili ya joto kwa vifaranga, joto liwe na nyuzi joto 32-35.
· Hakikisha joto loinakuwa la wastani.
Wiki ya kwanza - 35°c
Wiki ya pili - 32°c
Wiki ya tatu - 29°c
Wiki ya nne - 26°c
Wiki ya kwanza - 35°c
Wiki ya pili - 32°c
Wiki ya tatu - 29°c
Wiki ya nne - 26°c
MUHIMU
Iwapo vifaranga wanatoka mbali na wamechoka wape glucose au sukaei kidogo kwenye maji ( kijiko cha chakula kwa kila Lita tank za maji).
KUPOKEA VIFARANGA
Watoe vifaranga kwenye maboksi kwa haraka na kuwaingiza kwenye mduara au hard board uliyoiandaa na hakikisha unayo hesabi kamili.
· vifaranga wore kwenye maji ya glucose watoe nauwanyweshe wale wore ambao hawakunywa maji.
· Baada ya masaa mawili weka chakula kwenye vyombo hakikisha kuna mwanga saa 24 na joto la kutosha.
Maoni
Chapisha Maoni