Tumia ndimu na tangawizi kuondokana na tatizo la tumbo kujaa
Uhakika media/ 17 hours ago
Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai
ZIPO sababu nyingi zinazofanya chakula kishindwe kuyeyushwa ndani ya tumbo la binadamu na hivyo kuwa kiini cha matatizo mbalimbali ikiwemo maumivu ya tumbo.
Kula kupita kiasi, kula mara kwa mara hata kama huna njaa, kula kwa haraka bila kutafuna sawasawa na kutokuwa na muda rasmi wa chakula.
Unapogundua kuumwa tumbo, kichefuchefu, kujamba, kuharisha na tumbo kujaa hewa mara nyingi vinaweza kusababishwa na tatizo la uyeyushaji chakula kuwa na hitilafu.
Ukiona tatizo hilo anza moja ya tiba hizi; ndimu, tangawizi, kitunguu swaumu, msubili, komamanga na asali.
Ndimu na tangawizi
Kijiko kimoja cha juisi ya ndimu, changanya na kingine chenye ujazo huo cha tangawizi, kunywa mara tatu kwa siku kama tiba ya kujaa tumbo.
Kitunguu swaumu
Chukua punje 20 za kitunguu swaumu saga, tia katika nusu glasi ya maziwa, koroga vizuri, kunywa vijiko viwili vya mezani robo saa kabla ya kila mlo mkuu kwa siku. Tunza ndani ya freji kiasi cha mchanganyiko huo kinachobaki.
Msubili
Jani la msubili kata kipande cha nusu futi, likate vipande vidogo vidogo kula kama kachumbari.
Komamanga na asali
Juisi ya komamanga, changanya na kijiko cha asali, kunywa kwa ajili ya kutibu tumbo kujaa, tumia tiba hii mara mbili kwa siku kwa muda wa siku tatu.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.
Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepedkmandaitz@gmail.com ili kupataushauri au virutubisho vyetu.
Maoni
Chapisha Maoni