Tiangong-1: Chombo cha China kuanguka Kikiwa moto.
Uhakika media 2. 1hr ago
Haki FRAUNHOFER
Chombo cha anga za juu cha China kwa jina Tiangong-1 ambacho kimekuwa kikitumiwa kama maabara kinatarajiwa kuanguka duniani mwishoni mwa wiki.
Kina urefu wa mita 10 na uzani wa zaidi ya tani 8 na ni kikubwa zaidi ya vyombo vyote vilivyoundwa na binadamu ambavyo vimewahi kuanguka kutoka anga za juu.
China inasema imepoteza mawasiliano yote na chombo hicho jambo ambalo linamaanisha kwamba mwendo wake wakati kinadondoka kutoka anga za juu hauwezi kudhibitiwa.
Hata hivyo, wataalamu wanasema uwezekano wa vipande vya Tiangong ambavyo havitakuwa vimeteketea kabisa wakati vikifika ardhini kuanguka kwenye maeneo yenye watu wengi ni mdogo sana.
"Ukizingatia kwamba Tiangong-1 ina uzani wa juu sana, vipande vyao vimekazwa sana, kuliko ilivyo kwa vitu vingine ambavyo hurejea duniani kutoka anga za juu, kumekuwa na juhudi nyingi za kutumia mfumo wa rada kufuatilia mwendo wake na kukadiria ni wapi kitaanguka," anasema Richard Crowther, mhandisi mkuu katika Shirika la Anga za Juu la Uingereza.
"Sehemu kubwa ya chombo hiki inatarajiwa kuungua kikiingia ndani ya anga ya dunia kutokana na kushika kiwango cha juu cha joto. Uwezekano mkubwa ni kwamba vipande ambavyo vitasalia baada ya hapo vitaanguka mahali baharini," aliambia BBC.
Ni vigumu kujua mapema ni wapi kitaanguka na ni wakati gani
Kawaida, wataalamu huweza kubaini ni wapi saa moja kabla ya chombo kama hicho kuanguka
Sehemu kubwa ya chombo hicho itaungua chombo kitakapoingia kwenye anga ya dunia
Njia ya mzingo ya chombo hicho ina maana kwamba vifusi sana vitaanguka katika eneo moja
Pengine 20-40% ya chombo hicho itafika ardhini, ambayo ni tani 1.5-3.5 hivi
Uwezekano mkubwa ni kwamba vifusi hivi vitaanguka baharini
Njia ya kuanguka kwa vifusi hivyo ardhini inaweza kuwa na umbali wa mamia ya kilomiya
Tiangong ndicho chombo cha 50 kwa uzani kuanguka duniani kikiwa hakiwezi kudhibitiwa
Chombo hiki ambacho kilikuwa kikitumiwa kama kituo cha anga za juu kilirushwa angani mwaka 2011 na kutembelewa na wana anga sita wa China.
Tiangong kilifaa kusitisha shughuli yake ya kuizunguka dunia kwa utaratibu na mpangilio fulani.
Lengo lilikuwa kutumia vifaa vinavyokipa msukumo kukielekeza hadi maeneo ya mbali yasiyo na watu maeneo ya Bahari ya Kusini.
Lakini kabla ya hilo kufanyika, ghafla mfumo wa kukidhibiti ulikumbwa na hitilafu na wataalamu wa China wakapoteza udhibiti.
Kwa sasa, hakuna lolote linaloweza kufanyika kuzuia chombo hicho kisianguke popote.

Maoni
Chapisha Maoni