Lukuvi aombwa kutatua mgogoro wa ardhi
Uhakika media · 3 hours ago
Na James Timber, Mwanza
Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi Wiliam Lukuvi ameombwa na wananchi wa mitaa ya Ndofe, Mbugani na Ihushi Kata ya Igoma katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, kuwatatulia mgogoro unaowakabili unaotokana na madai ya uvamizi wa barabara ya mtaa ya St.Merry's-Buhongwa.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbugani Kulwa Titto, alisema awali barabara iliyokuwepo ina mita 24 lakini kwa sasa serikali kupitia Idara ya Mipango Miji imeamua kuongeza mita 16 hali ambayo itaathiri makazi ya watu zaidi ya 300 kutokana na kujenga kwa kuzingatia ramani ya barabara ya awali.
“Mwaka 1974 kishiri ilikuwa na usajili wa Mz/ Kij/ 618 Mwanza vijijini, lakini 1984 mwanza walikuja na usajili mpya wa 14 Mz/277022072/ PT town Plan, sasa huyu mkuu wa Idara anatuambia vijiji vilikufa mwaka 1952 hii hali 74 Kishili ilikuwa na usajili wa kijiji,” alisema Titto
Alisema hawapingani na serikali kwa suala la maendeleo lakini sasa wanatakiwa wahamishwe kwa fidia ili kuweza kutafuta sehemu nyingine ya kuishi na si kusema kuwa wao ni wavamizi hii hali wamekuwepo kabla ya masta plan.
Kwa upande wake Said Mchele alisema amekuwepo Kishiri toka vijiji vya ujamaa kwa zaidi ya miaka 70 na amerithishwa hayo makazi na babu zake suala la kuvamia barabara si kweli maana kwake ana makabuli ya marehemu babu zake waliofariki toka 1984.
Aidha Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibambamba kupitia barua yake kwa wenyeviti wa mitaa hiyo yenye kumb namba MCC/L/20/12/VOL.III/88, alisema marekebisho yatayofanyika yatategemea kukubaliwa na kuidhinishwa na mkurugenzi wa mipango miji ndipo yawe na nguvu kisheria.

Maoni
Chapisha Maoni