Uhakika media 2 · 3 hours ago
Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri amepata ushindi katika uchaguzi wa rais nchini humo kwa kupata asilimia 92 ya kura.
Wapigakura milioni 20 kati ya milioni 60 walioandikishwa walipiga kura katika uchaguzi huo uliofanyika kwa siku tatu na kumalizika jana Jumatano.
Tume ya uchaguzi ilitoa wito wa dakika za mwisho kwa watu kupiga kura, ikitaraji kuongeza wingi wa watu waliojitokeza kupiga kura hali ambayo Sisi anaiangalia kuwa muhimu kuhalalisha ushindi wake.
Uchaguzi huo uliofanyika kwa siku tatu ulikamilika jana na kurefushwa kwa saa moja, baada ya tume ya uchaguzi kutoa onyo kwa watu ambao hawatapiga kura kwamba watatozwa faini ya pauni za Misri 500 sawa na dola 30 za Marekani.

Maoni
Chapisha Maoni