Uhakika media 2 · 3 hours ago
Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Malala Yousafzai, amerejea Pakistan kwa mara ya kwanza tangu aliposhambuliwa na wanamgambo mwaka 2012 waliokasirishwa na hatua yake ya kuhamasisha elimu kwa wasichana.
Ulinzi uliiimarishwa wakati Malala mwenye umri wa miaka 20 na mwanafunzi wa chuo kikuuu alipowasili leo nchini humo.
Televisheni za nchi hiyo zimemuonesha mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel akiwa na wazazi wake kwenye eneo la mapokezi la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Benazir Bhutto na aliondoka uwanjani hapo akisindikizwa na msafara wa karibu magari 15 mengi miongoni mwa magari hayo yakiwa na askari polisi waliokuwa na silaha nzito.
Malala anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Pakstan baadaye leo.

Maoni
Chapisha Maoni