RIWAYA NA HADITHI ZA KUSISIMUA
Mtuhumiwa 06
Posted by uhakika media
Kwa furaha Jaka alitamani kumshukuru Osman kwa kumpa mkono, lakini hakufanya hivyo. Badala yake aliitazama ile bahasha taratibu na kugundua kuwa ilikuwa imefunguliwa hivyo akajua kuwa Osman alikuwa ameshaisoma. Aliangalia muhuri wa Posta wa siku barua ile ilipofika pale Dodoma, na kugundua kuwa barua ile ilikuwa imefika zaidi ya wiki mbili nyuma.
Alimtazama Osman kwa hasira ya wazi.
“Sasa si bora ungenisimulia tu yaliyoandikwa kwenye barua hii, unaonaje?” Alimwambia kwa hasira, kisha bila kusubiri jibu aligeuka na kuondoka.
Osman alibaki akiwa amefura kwa hasira.
4
Akiwa amebakiza miezi miwili akamilishe mwaka mmoja mjini Dodoma, Jaka alirejewa tena na ile ndoto ya yule msichana wa ajabu. Kwa muda wote uliopita alisahau kabisa kuhusu ndoto ile. Jambo lililomshangaza ni kwamba ndoto ile ilimrudia vilevile kama ilivyomjia mara ya kwanza.
Hili lilimpa taabu sana kulielewa.
Nini maana ya ndoto hii?
Ni utabiri wa aina fulani au…?
Vyovyote iwavyo hii si ndoto ya kawaida…si ya kawaida kabisa! Sasa kwa nini inanijia namna hii?
Alikuwa akiwaza mambo hayo huku akitembea jioni ya siku iliyoamkia usiku alioota ile ndoto kwa mara ya pili. Ilikuwa inapata saa moja kasoro robo hivi za jioni.
Alikumbuka maneno ya mzee Mnyaga mara alipomueleza habari za ndoto ile baada ya kumrudia tena asubuhi ya siku ile. Mnyaga alibaki mdomo wazi, na kwa muda mrefu alibaki kimya kabla ya kumwambia kuwa alikuwa na uhakika kuwa ndoto ile ilikuwa inambashiria mambo fulani ambayo yangemtokea baadaye au yaliyomtokea hapo awali. “…ila kwa hakika hiyo ndoto inakubashiria mafanikio fulani…” Mnyaga alimalizia huku akionyesha kuwa na mawazo mengi.
“Mafanikio? Kwa vipi anko?” Alimuuliza huku akionyesha kutoamini kabisa maneno yale.
Mnyaga aliguna kidogo kabla ya kumjibu.
“Kwanza kuna mwanga katika ndoto yako, ambayo ni ishara ya ufumbuzi fulani…halafu kuna mwamvuli…mwamvuli unaashiria kinga au ushindi wa aina fulani…” Mnyaga alisita kidogo, kisha akaendelea “…sijui lakini…ila nadhani vitu vyote hivyo vinaashiria mafanikio…ushindi dhidi ya matatizo, ambayo humo ndotoni yamekuja kama mvua ya maji moto na yule khabithi Osman Mgunya laana za manani zimuangukie milele!”
Jaka alimcheka sana kwa majibu yale, akimtania Mnyaga kuwa ni vyema angeanzisha biashara ya kutabiri ndoto.
Lakini sasa kila alivyozidi kulifikiria swala lile ndivyo lilivyozidi kumtia wasiwasi kwani lilionesha uhusiano fulani na jambo jingine ambalo kwa muda mrefu limekuwa likimkosesha raha. Kwa namna fulani amekuwa akipatwa na hisia kwamba kuna kitu au jambo fulani hivi, ambacho kingeweza kumtoa katika janga lile alilotumbukizwa…
Ni kitu gani basi?
Hakuweza kukiweka sawa akilini mwake kitu hicho, ingawa uwepo wake ulizitawala sana hisia zake. Ni kitu ambacho kilikuwepo muda wote tangu mwanzo.
Sasa na hii ndoto tena…
Mungu wangu ! Ni nini kinanitokea mimi?
Kwa nini mimi… ?
___________________
Maisha ya binadamu huweza kubadilika kwa namna ya ajabu kabisa na kwa namna ambayo hata binadamu mwenyewe hawezi kufanya lolote katika aidha kuyazuia yasibadilike au kuyafanya yabadilike na kuingia kwenye hali hiyo yanayobadilikia.
Ni sawa na jinsi alivyoeleza mwanafalsafa mmoja wa Ujerumani aliyeishi karne kadhaa zilizopita aliyeitwa Hegel. Yeye alisema kuwa binadamu hawezi kubadilisha au kuongoza matukio katika historia, bali mwanadamu huishi maisha yake kutekeleza yale ambayo matukio ya historia yametayarisha yamtokee mwanadamu katika maisha yake mafupi hapa duniani.Hivyo kadiri matukio yanavyobadilika na binadamu nae hulazimika kubadilika.
Sio watu wengi waliokubaliana na Hegel wakati ule alipokuwa akiandika falsafa zake hizo katika karne ya kumi na nane. Na pia sio wote wanaokubaliana nae leo hii katika karne hii tuliyonayo sasa.
Lakini bila shaka katika wale wachache watakaoweza kukubaliana na falsafa hii ya marehemu Geog Wilhelm Friedrich Hegel katika karne yetu hii, Jaka atakuwa ni mmoja kati yao hasa ukizingatia jinsi maisha yake yeye yalivyobadilika kwa namna ya ajabu k

Maoni
Chapisha Maoni