RIWAYA NA HADITHI ZA KUSISIMUA
mtuhumiwa 01
Posted Uhakika media
Jambazi hatari linalojishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya huko Marekani ya Kusini limefanikiwa kwa mara nyingine tena kuwatoroka askari wa Kikosi Cha Kupambana na madawa ya kulevya cha Marekani (D.E.A) baada ya askari hao kuizingira kambi yake.
Habari za kuaminika zinaeleza kwamba jambazi hilo, Claudio Zapata, liliwatoroka askari hao baada ya mapambano makali ya kutupiana risasi kati ya kundi lake na wana usalama wa D.E.A. Katika mapambano hayo, askari kadhaa walijeruhiwa na wawili waliuawa. Wafuasi wengi wa jambazi hilo waliuawa na wachache waliokuwa wamejeruhiwa walitiwa mbaroni.
Kutokana na hali hiyo, msako mkali wa kimataifa umeanza dhidi ya jambazi hilo hatari ukiongozwa na askari wa D.E.A
wakishirikiana na wana usalama wa FBI ambapo habari zisizo za uhakika mpaka sasa, zinaeleza kuwa jambazi hilo hivi sasa limejificha ndani ya nchi za Afrika ya mashariki.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania alikaririwa akisema kuwa panahitajika ushirikiano wa karibu sana baina ya Serikali ya nchi yake na nchi za Afrika ya Mashariki kwa ujumla kutokana na ukweli kwamba jambazi hilo linaweza kuwa ndani ya nchi yoyote miongoni mwa nchi za Afrika ya Mashariki . Chanzo chetu kingine cha habari kimedokeza kuwa tayari wana usalama wa FBI na D.E.A wameshaingia nchini Tanzania, kama jinsi walivyokwishaingia nchini Kenya, Uganda na hata kule Rwanda na Burundi katika harakati za kulisaka…
Disemba 15
Ndege kubwa ya Shirika la ndege la Uholanzi, KLM, ilitua kwa madaha kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (K I A) jijini Arusha. Ilikuwa ni saa nne za usiku, kiasi cha wiki mbili kabla ya sikukuu ya Noeli, na abiria wengi waliokuwa wakiteremka kutoka kwenye ndege ile walikuwa wamejawa bashasha zinazoambatana na maandalizi ya sikukuu ile mashuhuri.
Miongoni mwa abiria wale waliokuwa wakiteremka usiku ule alikuwamo Jaafar “Jeff” Bijhajha, mtu mmoja mrefu aliyejengeka kimichezo, hususan mchezo wa kikapu yaani basketball. Kwa mujibu wa hati zake za kusafiria, huyu jamaa alikuwa ni mwanafunzi wa shahada ya pili katika fani ya udaktari wa meno kutoka kwenye chuo kimoja cha kisichokuwa sana huko Uholanzi. Hati zake hizo pia zilibainisha kuwa mtu huyo alikuwa anaitwa Jaafar H. Bijhajha, mtanzania mzaliwa wa Machame huko Moshi, ingawa kabila lake lilikuwa ni Mfipa.
Iwapo angetokea mtu na kuamua kufuatilia ukweli wa maelezo haya, basi angegundua kuwa maelezo hayo yalikuwa ni kweli tupu kwa maana yalithibitishwa na vyeti vyote halali vinavyotambulika kitaifa.
Jamaa alikuwa amevaa suruali nzito aina ya Jinzi yenye rangi ya buluu na viatu vikubwa vya ngozi nyeusi vinavyofanana na vile vya wapanda milima huko Ulaya. Usoni alikuwa amevaa miwani ya kusomea iliyomletea ile taswira ya kitabibu haswa, na kichwani alikuwa amevaa kofia ya kepu au ‘Kapelo’ yenye lebo ya “Reebok”. Alikuwa amevaa shati zito la rangi ya buluu la mtindo wa drafti-drafti ambalo alikuwa amelichomekea vizuri sana ndani ya suruali yake. Begani alikuwa amening’iniza begi la wastani aina ya Ruksack.
Hakuwa na mzigo mwingine.
Kutokana na kazi zake, mtu huyu mrefu alilazimika kutumia majina mbalimbali kwa nyakati tofauti kutegemea na kazi anayokabiliana nayo katika wakati husika, na kwa kazi hii iliyomleta hapa Tanzania safari hii (ambapo ukweli ndio nchi yake hasa aliyozaliwa), jina lake lilikuwa ni Jaafar Bijhajha, mwenyewe akipendelea zaidi kujitambulisha kama “Jeff Bijhajha”.
Ingawa nia ya safari yake ilikuwa ni Dar es Salaam, mtu huyu mwenye ndevu zilizochongwa vizuri na kufanya umbo la herufi “O” kuuzunguka mdomo wake, alikata tiketi ya kuteremkia Kilimanjaro na ndivyo alivyofanya. Azma yake ilikuwa ni kusafiri kwa basi kutoka Kilimanjaro hadi Dar es Salaam siku iliyofuata.
Ukweli ni kwamba mtu huyu, ambaye kutokana na kazi yake ni nadra sana kutumia jina lake la halali alilopewa na wazazi wake kiasi cha miaka thelathini na minane hivi iliyopita, hakuwa mwanafunzi wala hakuwa akitokea Uholanzi masomoni.
Ingawa hati zake za kusafiria zilionyesha kuwa safari

Maoni
Chapisha Maoni