RIWAYA NA HADITHI ZA KUSISIMUA
Mtuhumiwa 05
Posted by Uhakika media
Na mara hiyo anasikia sauti kali ikimwita kwa jina lake kutoka kule walipokuwa wakielekea. Anainua uso wake kutazama ni nani anayemwita. Anamuona Osman Mgunya akiwafuata pale walipokuwa kwa mwendo wa haraka huku amekunja uso kwa ghadhabu zisizo kifani, mkono wake wa kulia ukiwa umeshika upanga mrefu ambao mara ile alipoinua uso wake kumuangalia yule mtu tu ule upanga ukatoa radi kubwa…upanga wa radi !
Osman Mgunya alikuwa akimwendea mbio huku akimwita jina lake mfululizo… Jaka!….Jaka!….Jaka!…..Jaka !
” … Jaka ! Jaka…! Jaka…amka, utachelewa kuripoti kituoni….saa mbili kasoro sasa!”
Jaka alishtuka kutoka kwenye usingizi na ndoto ile ya ajabu.
Kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka. Alifumbua macho kisha upesi akayafumba pale mwanga wa jua ulipompiga moja kwa moja usoni. Alijikinga uso wake kwa kiganja chake kutokana na mwanga wa jua lile na kuyafumbua tena macho yake taratibu.
Mnyaga alikuwa amemwinamia hali mkono wake wa kulia ukiwa begani kwake, akimtikisa.
“Anko leo umelala sana…nimeanza kukuamsha kitambo!” Mnyaga alimwambia.
” Unnnhh…aaankhh…nilikuwa naota….saa ngapi sasa?” Jaka alibwabwaja huku mwayo ukimtoka.
“Saa mbili kasoro kumi sasa!” Mnyaga alimwambia, naye akakurupuka na kuketi kitandani.
Jambo la kwanza lililomjia akilini mwake baada ya usingizi kumtoka ni kwamba sura ya yule binti aliyemuota kwenye ile ndoto haikuwa ngeni akilini mwake. Alikuwa na hakika kabisa kuwa ilikuwa ni sura ya mtu anayemjua…alishapata kuiona sura ile kabla ya ndoto ile…
Tatizo ni kwamba hakuweza kukumbuka ni wapi au lini. Alijiuliza sana ni nini maana ya ndoto ile katika wiki yote ile bila mafanikio. Jambo pekee alilokuwa na uhakika nalo ni kwamba yule askari aliyejiita Osman Mgunya hakuwa na nia nzuri kabisa naye. Hilo halikuwa na shaka hata kidogo akilini mwake.
______________________
Miezi minne baadaye alikuwa ameisahau kabisa ile ndoto, naye akawa ameshazoea hali ya pale Dodoma. Mara kwa mara alikuwa akienda sokoni pamoja na mzee Mnyaga na kumsaidia katika biashara zake za matunda. Katika moja ya siku hizo alipatwa na msukosuko ambao ulikuwa ni mpango wa Osman Mgunya katika kuhakikisha kuwa Jaka anafanya kosa litakalompa fursa ya kumchukulia hatua kisheria.
Siku hiyo alikuwa akiuza zabibu pale sokoni na mara wakaja jamaa wanne walioonesha nia ya kutaka kununua zabibu. Jaka alijaribu kuwakaribisha kwa uchangamfu na kuanza kuwatajia bei za mafungu mbalimbali ya matunda yale aliyoyapanga vizuri pale mezani.
Cha ajabu ni kwamba baada ya kukaribishwa, mmoja kati ya wale jamaa alichukua chana moja ya zabibu na kuikamua yote pale juu ya meza huku wale wenzake wakicheka kwa dharau na kebehi. Mara moja Jaka akabaini kuwa wale jamaa walikuwa wametumwa. Akaamua kunyamaza kimya.
“Vipi, mbona unagwaya wewe…huna ubavu nini?” Aliuliza kwa kejeli mmoja kati ya wale jamaa.
Kabla Jaka hajajibu, jamaa mwingine akamchapa kofi kali la uso. Kwa ghadhabu Jaka alitaka kumrukia yule jamaa lakini akawahi kujizuia. Mwingine akachukua chana mbili za zabibu na kuzitupa chini. Jaka akatoka nyuma ya meza yake na kwenda kuziokota. Vile anainama tu alipigwa ngwara kali sana kwa nyuma na kuanguka chali pale chini, na wale jamaa wakaendelea kumcheka kwa fujo.
Watu waliokuwa pale sokoni wakaanza kujaa huku wengine wakitaka kujua kulikoni.
Mara hiyo akatokea mzee Mnyaga, ambaye kwa hasira aliwafokea wale jamaa. Mmoja wa wale jamaa alitaka kumletea jeuri na Mzee Mnyaga akamtwanga konde zito lililompeleka moja kwa moja mpaka chini. Basi huo ukawa ndio mwanzo. Wafanya biashara wengine pale sokoni nao wakawavamia wale jamaa na kuwapa mkong’oto wa haja!
Na ni hapo ndipo Land Rover ya polisi ilipowasili kwa vishindo eneo lile huku askari wakiruka chini kwa jazba kuja kutuliza ghasia ile. Osman Mgunya alikuwa ndio kiongozi wa kundi lile la askari. Jaka alimtupia jicho kwa chati huku akendelea kupanga zabibu zake taratibu pale mezani na kumuona jinsi uso ulivyomshuka baada ya kuwaona wahalifu na kubaini kuwa Jaka hakuwa miongoni mwao.

Maoni
Chapisha Maoni