RIWAYA NA HADITHI ZA KUSISIMUA
Mtuhumiwa 04
Posted by uhakika media
Kutokana na hali hii basi, wakati Jaka alipolazimika kuuhama mji wa Dar es Salaam, mama yake kwa uchungu mwingi alimwambia aende Dodoma na akafikie kwa Anko wake Mnyaga ambaye alikuwa anafanya biashara ya kuuza matunda katika soko kuu la Dodoma. Baada ya kufika Dodoma Jaka hakupata taabu kumpata Mnyaga kwani tayari mawasiliano ya simu yalishafanyika tangu awali. Mnyaga alisikitishwa kwa Jaka kufika pale Dodoma katika mazingira yale. Baada ya Jaka kumueleza yaliyomsibu, akioanisha na maelezo aliyokwishapewa na mama Jaka hapo awali kwa njia ya simu, Mnyaga alisikitika maradufu na machozi yakamtoka kwa uchungu. Ndipo alipomkaribisha Jaka hapo kibandani kwake, katika eneo la Makole pale Dodoma mjini.
Alimuomba asijisikie mnyonge bali ajisikie kuwa yuko nyumbani na asiwe na wasiwasi kabisa kumfahamisha pindi atakapokuwa na tatizo lolote pale Dodoma kwani yeye sasa ni sawa na mzazi wake.
Jaka alimshukuru sana yule mzee na leo ndio siku ya nne tangu akaribishwe pale nyumbani kwa Mnyaga.
“Jaka…mbona hukula kile chakula nilichokuwekea pale mezani mwanangu?” Mnyaga alitoka ndani na kumuuliza. Safari hii Jaka alikuwa amesimama akiangalia barabarani huku mikono yake akiwa ameizamisha ndani ya mifuko ya suruali yake, na mabega yake akiwa ameyainua juu kwa kujikunyata kutokana na baridi kali la pale Dodoma.:
“Sijisikii kula kabisa leo Anko.” Jaka alimjibu bila kugeuka, jibu ambalo lilikuwa ni kweli tupu.
“Na lini unategemea kujisikia kula?” Mnyaga alimuuliza huku akimkazia macho kwa ukali. Tangu amefika Jaka amekuwa akikataa kula kwa sababu mbali mbali naye amekuwa akimlazimisha na kumbembeleza ili ale.
“Labda nitakula jioni…”
“Jioni si ndio hii…kuna jioni gani tena?”
“Nilikuwa namaanisha baadae kidogo, Anko.”
“Sikiliza Jaka…kula kwako ni muhimu sana hivi sasa. Wewe una mawazo mengi ambayo yanakula sana mwili wako…usipokula chakula utazidi kuihatarisha afya yako na mwisho wake utakufa…”
“Potelea mbali hata nikifa! Kwani kuna tofauti gani tena sasa?” Jaka alidakia kwa sautti ya ukali. Mnyaga hakubabaika. Alimjibu kwa upole huku akimtazama usoni kwa macho makali.
“Sidhani kama mama yako amekuagiza uje huku ili ufe, Jaka.”
“Wewe Anko kwako ni rahisi kusema hivyo kwa sababu hayajakukuta yaliyonikuta mimi…”
“Mimi yamenikuta kama jinsi ambavyo mama yako anavyoona yamemkuta…matatizo yako Jaka, ni yetu sote! Cha kufanya ni kusaidiana kuyakabili matatizo haya na sio kuongezeana mengine juu yake!”
Jaka hakuweza tena kuendelea kumjibu yule mzee, kwani alimheshimu sana.
“Samahani Anko…nilikuwa sijui nasema nini…”
“Naelewa Jaka. Huu ni wakati mgumu sana kwako…ila inabidi ukabiliane na hali hii kiume. Unakumbuka nilikwambia nini wakati ule bado uko mdogo? Siku uliporudi shuleni unalia njia nzima baada ya kupigwa na mwenzako?”
Jaka alimtazama yule mzee kwa muda bila ya kusema neno, kisha uso wake ukachanua kwa tabasamu pana.
“Hah! Yaani Anko bado unakumbuka mambo hayo?” Alimuuliza, halafu akacheka sana kwa sauti na Mnyaga nae akacheka huku akimshika mkono na kumuongoza ndani.
“Twende tukale bwana.” Alimwambia, na bila kupinga Jaka akaelekea ndani huku akiwa ameshikana mikono na Mnyaga. Kichwani mwake alikuwa akiyafikiria yale maneno aliyokumbushwa na Mnyaga. Zamani sana Mnyaga alimwambia maneno yale, lakini leo aliona ni kama jana tu wakati Mnyaga alipokuwa akimwambia maneno hayo…
Mwanaume kamwe hakabiliani na adui yake kwa machozi, bali hukabiliana naye kwa ngumi na hupigana mpaka mikono yake itumbukie mwilini mwa adui yake…na hapo mwanaume huanza kutumia miguu…
Jaka alikumbuka kuwa siku iliyofuata baada ya kuambiwa maneno yale na Mnyaga, alimtafuta yule mtoto aliyempiga na kumtaka wapigane. Mwisho pambano yule mtoto aliondoka analia akiwa na nundu kubwa kichwani huku akiacha meno mawili kwenye uwanja wa pambano. Jaka alirudi nyumbani akiwa mshindi.
3
Wiki mbili zilikuwa zimeshapita tangu awasili pale Dodoma, na amekuwa akienda kuripoti kituo cha polisi kila asubuhi na kila

Maoni
Chapisha Maoni