RIWAYA NA HADITHI ZA KUSISIMUA
Mtuhumiwa 02
Posted by uhakika media
Jamaa alijikuta ameshikwa kwa nguvu kutokea nyuma na hakuweza kufurukuta hata kidogo kwani mikono yenye nguvu ilipenya makwapani mwake na kufanya kabali kali kwa nyuma ya shingo yake.
“Unajifanya bingwa sio?” Yule gangwe aliyekuwa na kisu hapo awali alimuuliza kwa hasira huku akijichua sehemu chini ya jicho lake la kulia kwa kiganja cha mkono wake.
Pale pale Upara alikurupuka kutoka pale chini alipokuwa akigaragara kwenye tope na kumshindilia konde zito la mbavu kwa hasira yule jamaa.
Jamaa aligumia kwa uchungu, na yule binti akaachia kilio sambamba na pigo lile kama kwamba amepigwa yeye.
“Mshenzi sana ‘uyu!” Kama kwamba lile pigo lilikuwa halitoshi Upara aliongezea na tusi.
Jamaa alijikunja kwa maumivu huku akihisi nguvu zote zikimhama kama jinsi upepo unavyotoka kwenye puto lililotobolewa. Lakini mikono iliyokuwa imemshikilia ilikuwa imeshiba, hivyo akabaki ananing’inia tu.
“Jamani basi tusameheni…” Yule binti aliomboleza, na kuendelea, “…chukueni herini…bangili…pete…na hata nguo mkitaka mtuvue…maisha yetu tu mtuachie ndugu zetu!”
Jamaa alimgeukia yule binti, na hapo akaona kuwa na yeye pia alikuwa amedhibitiwa vilivyo na yule mtu aliyenyoa panki
“Ee jama ee…tufanye kweli tuishie jama…!” Mmoja wa wale watu wabaya alisema, na hapo Upara alianza kumvua pete za dhahabu yule binti kwa pupa, huku wale wenzake wakianza kulivua lile begi lililokuwa mgongoni kwa yule jamaa aliyeibuka ghafla kwenye uchochoro na kupamiana na yule binti aliyekuwa matatani. Lakini ghafla, kabla hawajafanikiwa kulitoa lile begi kutoka mabegani kwa yule jamaa, mwanga mkali uliwamulika wote pale.
“Mko chini ya ulinzi!” Sauti kali ya ki-askari ilisikika.
Si kizaa zaa hicho!
Wale waporaji wakawabwaga chini mateka wao na kuanza kutimua mbio. Lakini kule walipotaka kukimbilia nako mwanga mwingine mkali ukawamulika. Wakati huo huo yule jamaa aliyejitolea kumtetea yule msichana nae akatoka kasi sana kuelekea upande ambao kwake ulionekana kuwa ni salama. Lakini kabla naye hajafika popote alimulikwa na mwanga mkali usoni. Jamaa hakusimama. Alinyanyua mikono yake kuziba uso wake huku akiendelea kukimbia kuelekea kule kule mwanga ule ulipokuwa unatokea. Alichofanya ni kuikimbilia ngumi moja nzito ya uso, iliyompeleka chali kwenye tope.
Yule binti naye akatimua mbio kuelekea kwenye kona ya kutokea kwenye ule mtaa waliokuja nao, ambako ndiko mwanga wa mwanzo ulipotokea huku akipiga mayowe na kupayuka hovyo.
“Tusaidieni askari…tunauawa…watatuua! Heeeelllpp, for God’s Sake, jamaniii!”
“Tulia kama mlivyo! Tuna bunduki na tutavunja mguu mtu yeyote atakayejaribu kukimbia !” Sauti nyingine ya ki-askari ilifoka.
Wale majambazi wanne wakazingirwa mara moja na yule jamaa mwenye kibegi naye akaletwa na askari mwingine tayari akiwa ameshatiwa pingu. Askari wengine wawili walikuwa katika harakati za kuwatia pingu wale jamaa wanne, wakati askari mwingine alikuwa amemshikilia yule msichana kwa kumzungushia mkono wake mabegani kama ishara ya kumhakikishia usalama.
“Haya ndiyo tanayotu-distabu kira siku!” Mmoja wa wale askari alifoka kwa lafudhi ya ki-kurya huku akimtandika kofi kali la kisogo yule muhuni aliyenyoa panki.
Yule binti alishindwa kustahmili alipoona kuwa na yule jamaa aliyejitahidi kumsaidia naye ametiwa pingu kama wale wahuni.
“Afande huyu kaka sio mwenzao…tulikuwa wote katika balaa la hawa mabazazi…alikuwa akinisaidia huyo…”
“Waaacchaa! Mbona na renyewe ririkuwa rinajitahidi kuikimbia serikali, eenh?” Yule askari mwenye lafudhi ya ki-kurya alimkatisha yule binti kwa ukali.
“Kweli jamani…na yeye angeweza kuuawa na hawa jamaa…” Binti aliendelea kutetea.
“Hayo yote tutayajulia kituoni mama, sawa?” Aliingilia kati yule askari aliyemshika yule binti, ambaye ilionekama kuwa ndiye kiongozi wa doria ile.
Binti hakuwa na kauli zaidi.
Muda wote huo yule jamaa mwenye kibegi alikuwa kimya tu, uso wake akiwa ameuinamisha chini. Yule binti alimsogelea na kumshika bega kama ishara ya kumtoa hofu. Jamaa w

Maoni
Chapisha Maoni