RIWAYA NA HADITHI ZA KUSISIMUA
Mtuhumiwa 07
Posted by uhakika media
Mara alihisi akimwagiwa petroli mwili mzima.
Hah! Nachomwa moto hivi hivi sasa!
Alijikurupusha na kusimama kutoka pale chini, lakini akapigwa ngwara iliyorudisha tena ardhini kwa kishindo huku akisikia lile kundi la watu likiendelea kumpigia mayowe ya jazba. Akajua kuwa sasa mwisho wake ulikuwa umedhihiri. Hakuwa tayari kulikubali hilo. Kwa nguvu zake zilizosalia alijitahidi kujiinua kutoka pale chini ili aukwepe umauti ule uliokuwa ukimkabili. Hapo ikawa kama ndio amechokoza nyuki, kwani aliangushiwa mapigo makali kutoka kila upande. Alipigwa rungu la nguvu kichwani na akahisi fahamu zikimpotea taratibu.
“Lete kibiriti upesi tumuwashilie mbali kimburu huyu!” Sauti yenye jazba iliamuru.
Na mara hiyo lilitokea gari na kumulika lile eneo kwa taa zake kali. Jaka alihisi kuwa aliweza kuusikia mvumo wa gari hilo ila fahamu zilikuwa zinamhama kwa kasi. Taa za gari lile ziliwamulika wale watu waliokuwa tayari wameshawasha mwenge kwa makaratasi na kipande cha mti ili wamchome moto “kibaka” yule. Walipoona kuwa wamemulikwa na taa za lile gari, wale watu walitimua mbio na kumuacha Jaka pale chini akipigania fahamu zake zisimtoke.
Ukungu mzito ulitanda mbele ya macho yake. Alijitahidi kutambaa kwa tumbo kuliendea lile gari lakini hakujua iwapo alikuwa anafanikiwa au alikuwa akiendelea kujigaragaza tu pale pale alipokuwa. Aliona mlango wa lile gari ukifunguka karibu sana pale alipokuwa na akashindwa kuelewa kuwa hiyo ilitokana na juhudi zake za kulisotea lile gari au ni kutokana na lile gari kumsogelea yeye pale alipokuwa akigaragara.
“Msss…aaadah!”
Aliona miguu ya mtu ikikimbia kuelekea pale alipokuwa amelala…hakuweza kuelewa iwapo ilikuwa ni miguu ya mwanamke au mwanaume, lakini hakujali. Kiza kilikuwa kinazidi kuyafunika macho yake naye alikuwa akijitahidi kutazama kule ile miguu ilipokuwa inatokea…au alipohisi kuwa inatokea, lakini ilikuwa ni kazi ngumu mno.
Kitu cha mwisho alichoweza kukisikia, au kwa lugha fasaha, alichoweza kukinusa, kilikuwa ni harufu nzuri ya uturi, na baada ya hapo alijihisi akitumbukia kwenye shimo refu lenye kiza kinene….
Alipoteza fahamu.
____________________
Clara Wilfred Mashauri Zaza alikuwa ni mwanadada aliyeumbwa, akaumbika. Si kama hakukuwa na wasichana wengine ambao wangeweza kupewa sifa kama hiyo. La hasha. Bali Clara alikuwa ni miongoni wa wale waliokuwa matawi ya juu kabisa katika kundi hilo.
Alikuwa mrefu. Urefu ambao ni athari ya kizazi chake ambacho hakikuwa cha kitanzania halisi bali chenye mchanganyiko wa damu ya kitanzania na ya kizungu. Ni mchanganyiko wa mbali kidogo na Clara mwenyewe hakupenda kabisa kujinasibisha na mchanganyiko huo. Badala yake alipenda kutambulika kama mtanzania halisi, na hivyo ndivyo alivyojitahidi kuyaweka maisha yake.
Mama yake Clara ndiye hasa aliyekuwa na mchanganyiko huu wa mzungu-mtanzania.
Joanna Salvatori alikuwa ni mwanamke ambaye baba yake alikuwa mzungu wa damu kabisa kutoka Italia aliyeitwa Rocco Salvatori. Rocco aliamua kuoa binti mzuri wa kizaramo na kuhamia kabisa Tanzania.Wakati huo Tanzania ilikuwa bado iko katika makucha ya wakoloni na mzee Rocco Salvatori alikuwa akimiliki shamba kubwa la mkonge kule Tanga. Jinsi alivyokutana na binti huyo wa kizaramo haijulikani, lakini alimpenda na kumjali sana mke wake huyo.
Hawa ndio waliomzaa mtoto Joanna ambaye ndiye akaondokea kuwa mama yake Clara.
Joanna alijaaliwa vitu vitatu; urefu, ambao aliurithi kutoka kwa baba yake mzee Rocco Salvatori, weupe ambao uliuzidi hata ule wa baba yake, na busara ya hali ya juu.
Wazazi wake hao walifariki katika ajali mbaya ya ndege wakati wakirejea Tanzania kutoka Uingereza ambako mzee Rocco Salvatori alikwenda kwa matibabu ya ini, na Joanna akajikuta ameachiwa utajiri mkubwa sana, utajiri ambao uliambatana na jukumu la kumlea mdogo wake wa kiume aliyeitwa Deogratius.
Pamoja na huzuni kubwa iliyowakumba yeye na mdogo wake kutokana na vifo vya wazazi wao, msichana Joanna hakutetereka hata kidogo. Hekaheka za kuanzishwa kwa siasa za vyama vingi zilipokuwa zinazidi

Maoni
Chapisha Maoni