Swala la wadudu waharibifu kupatiwa ufumbuzi na EAC
IMECHAPISHWA: 27 MACHI 2018
Published by uhakika media
NCHI za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinatafuta njia ya kuwa na Sera itakayoweka utaratibu katika kusimamia dawa za kuulia wadudu kwenye mazao ili kusaidia ukanda huo kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo huku zikielezea uharibifu wa mazao ulivyokuwa awali.
Moja ya wadudu ambao wataanza kuwekewa mikakati ya pamoja kukabiliana nao ni viwavijeshi vinavyosababisha njaa kwa watu zaidi ya milioni 300 katika bara la Afrika kwa kukabili nchi 45 kati ya 55 za Afrika.
Kwa mujibu wa Shirika la Kilimo na Chakula (FAO), wadudu hao wameathiri mamilioni ya hekta za mashamba ya mahindi. Wataalamu wa masuala ya kilimo wamesema kuweka mikakati ya kusimamia dawa hizo itasaidia kupunguza zinazotokana na wadudu hao waharibifu, kukuza biashara na kulinda afya za wanadamu na mazingira.
Kaimu Katibu Mkuu wa EAC anayesimamia uzalishaji na masuala ya kijamii, Christophe Bazivamo amesema, kwa kutumia sera hiyo ya kuwianisha usajili, ukaguzi, matumizi na usimamizi wa dawa hizo, itasaidia kupunguza gharama katika nchi wanachama kwa kushirikiana kwa ajili ya matokeo bora.
Amesema, sera hiyo itapelekwa kwa Baraza la Kilimo Mei na baadaye kupitishwa na Baraza la Mawaziri Novemba mwaka huu. Nakala ya sera hiyo inapendekeza kuwepo kwa usajili wa mtandao utakaoanzishwa, kurahisisha upatikanaji wa maelezo kuhusu usajili wa dawa hizo katika nchi zote sita wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
Mara nyingi dawa hizo za kuua wadudu, huingizwa katika nchi hizo kutoka nje ya ukanda huo. Bazivamo alisema kukosekana kwa sera madhubuti katika usimamizi wa dawa hizo, kunasababisha kuingizwa kwa dawa zisizo na ubora, hivyo kusababisha hatari kwa afya za binadamu.
“Nguvu ya pamoja inatakiwa ili kuepuka kutuma kwa dawa zisizo na ubora, kwani kukosekana kwa sera ya pamoja, dawa feki ikiingia katika nchi moja mwanachama ni rahisi kutawanywa katika nchi nyingine,” alisema Bazivamo.
Alieleza kuwa kwa kutumia sera ya pamoja, ikiwa bidhaa itasajiliwa katika nchi moja, hakuna sababu ya kusajiliwa kwa nchi nyingine bali itatumika katika nchi zoate. “Hii itasaidia pia kubana matumizi ,kwani ukaguzi utafanywa kwa pamoja ,kwa kuaminiana itakuwa rahisi na kupunguza gharama kwa kuwa hakuna sababu ya kurudia ukaguzi”alisema.
Ofisa Mkuu wa Kilimo katika nchi za EAC na Waziri wa Mambo ya ndani wa Uganda, Teddy Asio, alisema kuhakikisha dawa hizo zinasimamiwa ipasavyo ni vema kufanya majaribio katika nyakati za mvua na Ukame katika maeneo mbalimbali.
Alisema wataalamu wameshauri ni vema kuweka mkazo katika kufanya majaribio katika aina mbalimbali ya mazao, kama kilimo cha mabondeni na milimani cha mazao ya mahindi, mchele na mengineyo.
Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Kilimo Rwanda (RAIDA), Evariste Safari, alisema programu ya kuanzishwa kwa sera ya dawa za kuua vijidudu katika nchi za EAC, itasaidia kurahisisha kupima, usajili na biashara ya dawa hizo.
“Nafikiri kuna orohda ya sawa ambazo zimeruhusiwa au kupigwa marufuku katika nchi moja huku nchi nyingine hazifanyii kazi orodha hizo, hivyo kuwa na hatma ya pamoja itasaidia mawakala, serikali na sekta binafsi na wakulima kwa sababu itawezesha kutumia dawa zilizobora kwa wakulima”alisema.

Maoni
Chapisha Maoni