Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

Report ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali


RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17, imegusa mambo makubwa saba, ikiwemo udhibiti mkubwa na matumizi mazuri ya fedha za umma.


Kwa mujibu wa CAG, ofisi yake imetoa hati 561 ambapo hati 502 sawa na asilimia 90 zinaridhisha, hati 45 sawa na asilimia 8 zina mashaka, hati 7 sawa na asilimia 1 haziridhishi na hati 7 sawa na asilimia 1 ni mbaya.

Ripoti hiyo pia imebainisha kutolewa kwa hati chafu kwa baadhi ya halmashauri, utendaji mzuri wa Serikali Kuu na Deni la Taifa.

Maeneo mengine ni mamlaka za serikali za mitaa, utendaji wa mashirika ya umma, miradi ya maendeleo na ukaguzi maalumu.

Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad alimkabidhi Rais John Magufuli vitabu 6 vya ripoti hiyo, Ikulu, Dar es Salaam jana.

Ripoti hizo ni pamoja na ripoti ya Serikali Kuu, ripoti ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ripoti ya Mashirika ya Umma, ripoti ya miradi ya maendeleo, ripoti ya Ukaguzi na Ufanisi na ripoti 10 zinazohusu ukaguzi wa ufanisi katika sekta mbalimbali.

Profesa Assad alisema serikali imeendelea kufanya vizuri, kwani kumekuwa na hatua nzuri ya kuongeza hati zinazoridhisha na kupunguza hati za mashaka na mbaya.

Alibainisha kuwa mashirika ya umma, yamepata hati safi kwa asilimia 96, Mamlaka ya Serikali za Mitaa asilimia 90 na Serikali Kuu imepata asilimia 86 kwa sababu ndani yake kuna vyama saba vya siasa ambavyo hakukuwa na makubaliano juu ya hesabu zake.

Baadhi ya vyama hivyo, kwa mujibu wa CAG, ni Tanzania Labour Party (TLP), Alliance for Tanzania Democratic Change, Demokrasia Makini na Chama cha Sauti ya Umma. Alisema sheria inamtaka kuvikagua vyama vyote vya siasa bila kujali kama vinapata ruzuku au la.

Serikali za Mitaa Baadhi ya halmashauri zilipata hati chafu. Halmashauri hizo ni Kigoma-Ujiji, Kigoma Vijijini na Pangani. Baada ya taarifa hiyo ya CAG, Rais Magufuli alimwagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo kuwasimamisha kazi wakurugenzi wa halmashauri hizo tatu kutokana na halmashauri zao kupata hati chafu.

Serikali Kuu Kwa mujibu wa Profesa Assad, kwa upande wa Serikali Kuu, kati ya taasisi 217 zilizokaguliwa, taasisi 204 zilipata hati safi ambayo ni sawa na asilimia 86; taasisi 22 ambazo ni sawa na asilimia tisa zimepata hati zenye shaka, wakati asilimia mbili ya taasisi hizo zikipata hati zisizoridhisha.

Aidha, katika eneo hilo pia, Prof Assad alisema kuwa kuna kesi za rufaa ya kodi zenye thamani ya Sh trilioni 4.4 ambazo mpaka sasa bado hazijafanyiwa uamuzi na Mahakama, wakati pingamizi za kodi zikigharimu Sh bilioni 739.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Rais Magufuli alimuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kujadiliana na Jaji Mkuu ili kesi hizo ziamuliwe haraka.

Kwa mujibu wa CAG, walibaini kuwepo kwa mitambo ya kuchenjulia madini mkoani Mwanza, Shinyanga na wilayani Kahama kufanya kazi bila ya kuwa na leseni, hivyo kuingiza hasara ya Sh bilioni 232. Deni la Taifa Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, deni la Taifa limeongezeka kutoka Sh trilioni 41 mwaka uliopita hadi kufikia Sh trilioni 46 sasa.

Alisema kuwa kuna ongezeko la shilingi trilioni tano ambazo ni sawa na asilimia 12.

Mamlaka za serikali za mitaa Katika eneo hilo, CAG alisema kuwa Serikali za Mitaa 146 hazikupata Sh bilioni 582 kama sehemu ya bajeti ya maendeleo ya Serikali za Mitaa.

Aliongeza kuwa Sh bilioni 532 sawa na asilimia 51 ya fedha maendeleo, pia hazikupelekwa kweye serikali za mitaa 167. “Lakini pia fedha za miradi ya ndani kwenye Serikali za Mitaa hazikukusanywa aidha kwa kuwatumia mawakala au halmashauri zenyewe.

Serikali za Mitaa 140 hazikukusanya Sh bilioni 116 sawa na asilimia 22 ya mapato yake. Pia Profesa Assad alieleza kuwa vitabu 379 vya mapato hakuviona, hivyo hajui ni kiasi gani cha mapato kimepotea, lakini pia miradi mitatu yenye thamani ya Sh bilioni 1.6 kwenye Halmashauri za Biharamulo, Karagwe na Mpwapwa, imechelewa kukamilishwa.

Udhai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

PAKUA PICHA ZENYE UJUMBE WA MAPENZI HAPA

KWA WALE WAPENZI WA PICHA ZENYE UJUMBE WA MAPENZI BASI HIZI HAPA Uhakika media 

Dawa 8 zinazo tibu kipanda uso kwa haraka

Uhakika media Dawa za asili 8 zinazotibu kipanda uso kwa haraka Dawa za asili 8 zinazotibu kipanda uso kwa haraka   Kipanda uso ni ugonjwa gani?   Kipanda uso ni maumivu ya kichwa ambapo kichwa kinagonga kweli kweli na mara nyingine inaweza kuwa sehemu ya mbele au upande mmoja wa kichwa ndiyo unapatwa na maumivu haya.   Maumivu haya yanaweza kubaki kwa saa 4 mpaka saa 72. Vile vile dalili za ugonjwa huu zinatofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine.   Dalili za Kipanda Uso:   Unaweza kupata baadhi ya ishara za ugonjwa huu kama vile; 1. Kujisikia uvivu, 2. Kutapika, 3. Mauzauza, 4. Kusikia kelele sikioni nk. Wakati mwingine kabla ya kipanda uso watu wengine wanaweza kupatwa na miwasho, shingo nzito, kupiga miayo, kusikia njaa nk Sababu za kutokea kipanda uso mara nyingi ni pamoja na: 1. Mfadhaiko wa akili (stress) 2. Kelele nyingi kuzidi 3. Kuluka kula mlo 4. Pombe 5. Siga...

SIMULIZI NZURI NA ZA KUSISIMUA sehemu ya 1

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 1 Uhakika media SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA Mwandishi: SEID BIN SALIM SEHEMU YA KWANZA Mwaka mmoja ukiwa umepita tokea binti mwenye umri wa miaka 24 lucky ajiunge na chuo kikuu cha dar es salam UNIVERSITY OF DAR ES SALAM. Marafiki zake aliokuwa anakaa nao chumba kimoja katika hostel waliojulikana kwa majina ya Mariam, Tunu, na amina. Asubuhi na mapema ya wiki end waliamua kumkalisha chini rafiki yao huyo kwa ajili ya kuongea nae mambo flan, kutokana na jinsi walivyokuwa wanaishi nae katika hali ya unyonge na kuonekana hapend kushirikiana na mtu yoyote kimasomo hd starehe za hapa na pale. waliishi nae kama sio mwenzao, walipoitaji ushirikiano wake hakuitaji kuwa nao, muda mwingine walimshuhudia akikaa kiupweke hadi kutoa machozi kwa muonekano wa kuwaza mambo mazito aliyonayo moyoni mwake, walimuonea huruma hasa kwa sababu wao ni watu waongeaji, walimkalia vikao vya kimya kimya walipopata nafasi ya kipeke ya...

NJIA 10 ZA KUTONGOZA KWA MACHO ZINAZO FANYA KAZI

Njia 10 za Kutongoza Kwa Macho Ambazo Hufanya Kazi Uhakika media   Je wataka kujifunza jinsi ya kutumia macho yako kupitisha ujumbe wa kuonyesha umevutiwa na mtu fulani? Kutumia macho kama mbinu ya kutongoza ni njia rahisi ya kupitisha ujumbe kutoka kwako hadi kwa yule unayemzimia kwa urahisi bila hata kutamka neno lolote. Mwanzo mchezo wa kutumia macho kama mbinu ya kutongoza huwa ina raha yake kiasi flani. Uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa ni rahisi kufahamu kiwango gani mtu amevutiwa nawe bila kuwauliza kuwatoa out. Pili ni kuwa uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa unamjulisha unayemzimia na mapema ya kuwa umewavutia hivyo kujitayarisha na mapema iwapo atakubali kufanya maongezi na wewe. So ni mbinu zipi hizo unazoweza kutumia kumvutia unayempenda bila kuonekana kama fala? Njia za kutongoza kwa kutumia macho Utafanya nini iwapo umemuona yule aliyekupendeza katika mkahawa ama katika party ulioalikwa na marafiki zako? Kama hujui la kufanya basi tumia macho yako kumtongoza...

Hatua za kufuata wakati wa tendo la ndoa

USIJE UMBUKA, SOMA HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA KUFANYA MAPENZI....! Uhakika media Wapnzi na wanandoa wengi hivi leo wanapoingia kitandani tayari kwa kuianza safari ya kupeana haki zao za msingi hushindwa kufurahia tendo na hasa hali hii hujitokezwa kwa wanawake kwani mwanaume huwa na haraka iliyopitiliza!   Mwanaume atamkumbatia na kumbusu mwanamke kwa muda mfupi na kabla hata hamasa ya mapenzi ya mwanamke ahaijashika hatama, atamwingilia na ndani ya dakika sekunde ama dakika zisizozidi 3, mwanamme hufika mshindo. Katika hali ya kusikitisha baada ya mwanaume kujitosheleza hujongea pembeni bila kujali mwenza wake hajafika mwisho wa safari hali inayosababisha mwanamke kupoteza hamu ya tendo endapo endapo tabia hiyo ya mwanaume itaendelea. Kunahatua nne muhimu ambazo wapendanao wakizishika na kuzitekeleza ipasavyo basi watafanikiwa kujitosheleza kila wanapokutana na kwa hakika watakuwa miongoni mwa watu wachache wanaofurahia faragha kila wakutanapo! Hatua ya kwanza ni...

Dawa mbadala ya kutibu uke mkubwa au ulio legea

DAWA MBADALA ZINAZOTUMIKA KUREJESHA UKE MKUBWA AU ULIOLEGEA Jinsi gani ya kukaza uke au ni namna gani kufanya uke uwe mdogo tena ni mada au somo lisilopendwa kuzungumzwa na watu wengi. Ikiwa wewe ni mmoja wa waathirika na tatizo hili basi tumia muda wa kutosha kusoma makala hii sasa hivi, irudie mara nyingi mpaka umeielewa. Kwenye makala hii nakwenda kukuonyesha baadhi ya mbinu za jinsi gani ya kurudishia tena uke mkubwa au uliolegea na kuwa mdogo tena ukiwa nyumbani bila kuhitaji kutumia matibabu mengine ya bei kubwa. KINACHOSABABISHA UKE KULEGEA Uke kulegea au kuwa mkubwa zaidi unaweza kutokea kutokana na sababu nyingi. Kumbuka pia kushiriki tendo la ndoa mara chache siyo suluhisho la kuwa na uke mdogo. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kuwa na uke mkubwa na kushiriki tendo la ndoa mara nyingi. Pia hakuna uhusiano wa umri na ukubwa wa uke. Wapo wamama watu wazima wana uke mdogo pia kuna wasichana wadogo kabisa wana uke mkubwa kupitiliza. Watu wengine huamini kuwa mwanamke mw...

Madawa mbadala 6 ya kutibu ganzi ya mikono na miguu

Dawa mbadala 6 zinazotibu ganzi mikononi na miguuni Published by fadhili on 17/11/2017 DAWA MBADALA 6 ZINAZOTIBU GANZI MIKONONI NA MIGUUNI Ganzi mikononi na miguuni inamaanisha kukosekana kwa fahamu katika sehemu hizo. Hisia ndiyo inakosekana sababu kunakuwa hakuna damu na neva zinakosa mawasiliano rya moja kwa moja na ubongo. Ni jambo la kawaida linalowapata watu wengi sana miaka ya hivi karibuni. Kinachosababisha ganzi mwilini ni pamoja na: 1. Shinikizo la muda mrefu kwenye miguu na mikono 2. Kuwa karibu na vitu vyenye baridi sana kwa kipindi kirefu 3. Mabadiliko ya muda mfupi kwenye neva 4. Ajali kwenye neva 5. Kunywa pombe kupita kiasi 6. Uvutaji wa sigara na bangi 7. Uchovu sugu 8. Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara 9. Ukosefu wa vitamini B12 na Magnesiamu 10. Ugonjwa wa kisukari nk Kwa kawaida ganzi inayotokea kwa dakika kadhaa na kupotea huwa haina shida yoyote lakini onana na daktari mapema ikiwa inakutokea mara kwa mara na pia ikiwa inakutok...

Jinsi ya kurudisha hisia za mapenzi zilizo potea

Jinsi ya kurudisha hisia za mapenzi zilizopotea uhakika media 2  · 9 hours ago Tunaishi kwenye ulimwengu unaoenda kasi sana kiasi kwamba usipokuwa makini, unaweza kujikuta ukimpoteza mtu uliyempenda sana maishani kwa sababu tu ya kutojua namna ya kwenda naye sawa. Inafahamika kwamba mapenzi ni hisia lakini ni wachache wanaoweza kueleza jinsi ya kufanya hisia za mapenzi ziendelee kuwa hai. Siku hizi ndoa nyingi zinaendelea kuwepo kwa sababu ya kudra tu, unakuta mume na mke wanaishi kwa sababu ya mazoea tu lakini si kwa sababu ya mapenzi! Wengine wanakwambia kabisa, ‘mapenzi yalikuwa wakati tunaanzana’! Wanaishi tu ilimradi siku zinaenda, ilimradi wanawalea watoto lakini si kwa sababu ya upendo kati yao. Wengine wanafikia hatua hata ya kulala mzungu wa nne au kutengana vyumba kabisa! Au kwenda kulala vyumba vya watoto, watu haohao Kwa nje mnawaona kama wanapendana lakini kumbe ndani kuna ufa mkubwa kati yao, hakuna tena mapenzi kati yao. Cha ajabu, utakuta watu hawahaw...

VIDEO: Mbwembwe za Joti aingia uwanjani kisa Samatta nusra akamatwe na polisi' refa amtoa

VIDEO: Mbwembe za Joti aingia uwanjani kisa Samatta nusra abebwe na polisi, refa amtoa Uhakika media 1  · 12 hours ago Joti ambae ni msemaji wa team Samatta leo ameonyesha vituko vya aina yake ambapo imepelekea baadhi ya mashabiki kuachwa midomo wazi kwa kitendo cha kuingia uwanjani wakati mpira uneendelea baada ya Mbwana Samatta kufanyiwa madhambia kwenye eneo la hatari  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

MBINU 10 ZA KUONGEZA MBEGU ZA KIUME

Mbinu 10 za kuoongeza mbegu za kiume (sperm count) Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua milioni 20, chochote chini ya hapa kinaweza kuwa sababu ya kutokutungisha ujauzito. Ikitokea umegundulika kuwa na mbegu chache, ni nyepesi sana na hazina nguvu za kukimbia vya kutosha basi makala hii itakupa maelezo juu ya mbinu 10 zinazoweza kukusaidia kuongeza uwingi wa mbegu zako bila gharama yoyote. Visababishi vya mbegu kuwa chache: Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, kwa bahati nzuri vingi ya vitu hivyo tunao uwezo wa kuvidhibiti kwa kupunguza matumizi yake. Vitu hivyo ni pamoja na: • Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume. Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta. Unashauriwa kutokuweka ...