Uhakika media 2 · 38 minutes ago
Leo ni siku ya pili wananchi wa Misri wamepiga kura katika uchaguzi wa urais, ambao rais wa sasa Abdel Fattah al-Sisi anatarajiwa kumshinda mpinzani wake ambaye hajulikani sana kisiasa.
Idadi ndogo ya wapiga kura imeshuhudiwa leo katika vituo vingi vya kupigia kura licha ya Mamlaka nchini humo kuendelea kuhamasisha raia kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye upigaji kura huo utakaochukua wa siku tatu.
Mgombea pekee anayeshindana na Al Sisi ni Bwana Moussa Mostafa Moussa ambaye anadaiwa kuwa mfuasi mkubwa wa rais Al-Sisi ambaye anaangaliwa kama msindikizaji tu katika uchaguzi huo.
Wagombea wengine walijiondoa kabla ya kuidhinishwa na tume ya uchaguzi, baadhi wakishikiliwa kwa tuhuma mbalimbali.

Maoni
Chapisha Maoni