Dodoma kubadilika
IMECHAPISHWA: 28 MACHI 2018 by uhakika media
KUANZIA Alhamisi Machi 29 mwaka huu, njia za daladala Dodoma zitabadilika kwa kurefushwa pamoja na kufuta stendi ya Jamatin, badala yake zitatakiwa kuishia NaneNane, stendi mpya ya mabasi.
Ofisa Mfawidhi Kanda ya Kati wa Sumatra, Conrad Shiyo amesema, njia hizo ndefu zimepangwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi, Manispaa ya Dodoma na Chama cha Wamiliki wa Daladala Dodoma (UWEDO).
Shiyo alisema katika marekebisho hayo, daladala zinazofanya safari kati ya Udom na Veyula zitakuwa zikitoka Udom zinapita kwa Waziri Mkuu, Posta, General Hospital, Independence, Sango na kupita NBC na kwenda Veyula na wakati wa kurudi Kuyoks Veyula zitapita Paradise, Nyerere, Posta hadi Udom.
"Daladala kutoka Nala zitapita Sango, Hospitali ya Mkoa, Posta hadi Benjamin Mkapa Hospitali na kurudi kwa kupitia Posta, General Hospital, Independence hadi Nala," alisema.
Kutakuwa na njia ya Veyula hadi Nanenane, daladala zikitoka huko zitapita Paradise, Nyerere, CBE hadi Nanenane na kurudi kupitia CBE, Carnival, General, Independence, Sango, NBC na kurudi Veyula.
Daladala kutoka Chang'ombe hadi Nanenane, zitapita Paradise, Nyerere, CBE hadi Nanenane zitapita CBE, Carnival, Genereal Hospital, Independence, Sango na kurudi Chang'ombe.
Magari ya kutoka St Gema hadi Swaswa au Nanenane, zitapita Paradise, Nyerere, CBE hadi Swaswa na Nanenane na kutoka huko Nanenane zitapita CBE, Carnival, General, Independence, Sango, NBC kurudi St Gema.
"Daladala za Nkuhungu zitapita vituo vya Sango, General, CBE hadi Nanenane na kurudi kwa kupitia kituo cha CBE, Carnival, Independence, Sango hadi Nkuhungu," alisema.
Daladala kutoka Mkonze zitapita vituo vya Kikuyu, Majengo, General, CBE hadi Nanenane na wakati wa kurudi zitapita vituo ni CBE, Carnival, General, Majengo, Kikuyu hadi Mkonze.
Daladala za kutoka Swaswa, Uzunguni na Nanenane na kurudi huku kupitia vituo vya CBE, Carnival, kisha njia ya uelekeo wa barabara ya sabasaba hadi D.Center (Makole) kisha kutokea mbele ya CBE na kurudi yalikotokea.

Maoni
Chapisha Maoni