Staa wa soka wa Ureno club ya Real Madrid ya HispaniaCristiano Ronaldo usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kushinda tuzo ya pili mfululizo ya mchezaji bora wa taifa laUreno 2017.
Tuzo hiyo Ronaldo anashinda ikiwa ni miaka mitatu imepita toka shirikisho la soka Ureno litangaze kumpa tuzo ya heshima ya mchezaji bora waUreno wa muda wote.
Ronaldo ameshinda kwa asilimia 65 huku Patricio akipata asilimia 18 naBernardo Silva wa Man City akipata asilimia 17, baada ya ushindi huo Ronaldo aliulezea mwaka 2017 kuwa ni moja kati ya miaka yake mizuri kisoka.
“Binafsi mwaka 2017 ni mwaka ambao hauwezi kusahaulika kwangu baada ya kuiwezesha Ureno kufuzu kucheza Kombe la dunia na kushinda mataji matano nikiwa na Real Madrid”>>> Ronaldo
Maoni
Chapisha Maoni