Aliyekutwa na mihuri ya baraza la mitihani mikononi mwa polisi
Uhakika media / 3 days ago
JESHI la polisi linamshikiria Selemani Masoud (68), mkazi wa Yombo Kilakala Dar es Salaam kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka mbalimbali za serikali ikiwemo kughushi mihuri na vyeti feki vya vyuo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Mambosasa amesema Machi 13, mwaka huu jeshi hilo lilipata taarifa za Kiitelijensia kuwa kuna kundi la watu linalojihusisha kutengeneza vyeti feki, mihuri na nyaraka mbalimbali za serikali katika eneo hilo.
Makachero wa kikosi kazi cha polisi walifika eneo la nyumba ya mshukiwa na kuanza upekuzi kwa kushirikiana na uongozi wa serikali ya mtaa kufanikisha kumkamata mtuhumiwa na nyaraka hizo.
Mtuhumiwa alikutwa na mihuri 53, ukiwemo wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), wa Chuo cha Ufundi Stadi (Veta), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM, Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua), Chuo cha Bandari, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Mtwara University, Muhuri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Muhuri wa cancelor wa UDSM, Chuo cha Usafirishaji (NIT),Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM), Bodi ya uhasibu (NBAA), Chuo cha Tumaini(TUDARCO), Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Rita, Health Laboratory, JKT Makao makuu na Marine Association of certified.
Mwingine wa ni wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam, Chuo cha uhasibu Arusha, Chuo cha utumishi wa umma, wa Wizara ya Maliasili na utalii, Mkurugenzi wa Jiji Eastern London, Mkuu wa shule Marangu, Mkuu wa shule ya Songambele, Mbagala Nursing, Msajili wa Ndoa, Shule ya Magereza, Medical Board of Tanganyika, Mkuu wa shule Kaselya Sec, Glory of Nursing, Director of Tanzania public service, Shule ya Sekondari Kibasila, ofisa elimu mkoa wa Kilimanjaro, Mwalimu mkuu shule ya Msingi Mgulani na mkuu wa shule ya sekondar Kyaka.
Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kubaini mtandao mzima anaoshirikiana nao ili kuhakikisha linawatia mbaroni wote hata kama ni watumishi wa umma.
Maoni
Chapisha Maoni